Polisi nchini Uganda inawashikilia wahudumu wawili wa afya kwa madai ya kuhusika kuwachoma takriban watu 800 chanjo feki za corona mwezi uliopita.
Mtu mmoja, ambaye ni daktari, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika kuwachoma watu hao chanjo katika mji wa Kampala kati ya Mei 15 na Juni 17...