chadema

CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.

Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.

Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.

Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
  1. JamiiForums Tanzania CHADEMA hamkujua kwamba Ulinzi wa Magereza ni kama Ulinzi wa Ikulu? Wangetoroka wafungwa kwenye maandamano yenu nani angewajibika?

    Nashindwa kuelewa nini maana ya siasa kwamba inafikia hatua watu wazima na akili zao wanashindwa kujua mipaka ya majukumu yao. Kwanini msitambue wala kujua mambo hatari kwenye usalama wa nchi? Vyovyote mfanyavyo, msivuke msitari mwekundu, si tu mtaumizwa bali pia mtauliwa kabisa na kutoweshwa...
  2. JamiiForums Tanzania Mchanganuo wa michango iliyokusanywa na CHADEMA ili kuwalipia faini viongozi wao

    MCHANGANUO WA MICHANGO ILIYOKUSANYWA NA CHADEMA ILI KUWALIPIA FAINI VIONGOZI WAO. 1. Rais Magufuli 38,000,000/= 2. Watanzania 30,000,000/= 3. Ndugu wa Mch. Msigwa 2,000,000/= 4. Hamphrei Polepole 30,000,000/= 5. Mkopo (Precision Air Tanzania) 250,000,000/= Jumla ya Michango yote ni...
  3. J

    JamiiForums Tanzania Inawezekana makamanda wa Chadema waliohamia CCM ni magarasa na turufu bado zimebaki Ufipa maana bado wanaonyesha Ufundi!

    Nimesikiliza kauli moja tu ya mtumishi wa Mungu Mchungaji Msigwa akikiri kuwa ana undugu na Rais Magufuli. Na zaidi Mchungaji Msigwa akasema kama wanafamilia "wao" wana namna wanavyoshughulikia mambo yao. Nilichojiuliza ni kwanini Mchungaji Msigwa hajawahi " Kujimwambafy" kwamba yeye ana...
  4. D

    JamiiForums Tanzania Wazo nzuri kuchangisha Tsh 350m kuwaokoa na kifungo viongozi CHADEMA ilikuwa pamoja na Mashinji. Itakuwa uungwana zaidi Tsh 30M kuirudisha CCM

    CHADEMA mlionesha uugwana mkubwa sana kwa kutuchangisha Tsh 350m kwa wahukumiwa wote hata aliyekuwa katibu Mkuu wenu aliyewakimbia. Hii iliwajengea heshima kubwaa kwa kuonesha kuwa mlithamini mchango wake na isitoshe kesi aliyohukumiwa ilitokana na kuwa kiongozi wa CHADEMA kipindi hicho...
  5. JamiiForums Tanzania CHADEMA anamuumiza kichwa Dr wa Majipu

  6. JamiiForums Tanzania Ushauri : Viongozi wa Chadema waliofungwa Segerea wakapimwe kama wamewekewa Sumu

    Mjumbe hauawi na huu ni ushauri kutokana na mashaka juu ya usalama wa wahusika ambao walinusurika kwenye mauaji ya kupangwa na baadaye kugeuziwa kibao na kuhukumiwa mahakamani , katika hukumu iliyojaa dhuluma. Mungu ibariki Chadema
  7. JamiiForums Tanzania Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe atoka Magereza

    Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe Ametoka Magereza na kusindikizwa na polisi pls mod naomba msiunge Thread Updates
  8. JamiiForums Tanzania CHADEMA mna mpango wa kujinasua mlipokwama?

    Nyie ndio chama kikuu cha upinzani kwa sasa, lakini inaonena hali si shwari kabisa. Wanachama wanawakimbia nyie mnatoa kisingizio kuwa wananunuliwa(ushahidi haupo) Viongozi wenu wanahukumiwa kwa kosa la jinai nyie mnaleta propaganda,mara account zimefungwa, tumechangiwa na wananchi n.k...
  9. J

    JamiiForums Tanzania DPP: Bado naitafakari hukumu ya Viongozi wa CHADEMA, naweza kukata rufaa

    DPP Biswalo amesema amepokea nia ya CHADEMA ya kukata rufaa lakini hata yeye bado anaitafakari hukumu hiyo na isipomridhisha atakata rufaa. DPP amesema kisheria muda bado upo wa yeye kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo ya Mbowe na wenzake. Chanzo: ITV habari! Pia soma > Mahakama ya Kisutu...
  10. JamiiForums Tanzania Segerea: Wabunge wa CHADEMA Ester Bulaya, Ester Matiko na Halima Mdee waachiwa. Wasema sasa ni saa ya ukombozi Tanzania

    Viongozi watatu; Halima Mdee (Mb), Esther Bulaya (Mb) na Esther Matiko (Mb), wametoka magereza asubuhi ya leo na watazungumza na wanahabari leo katika Ofisi za CHADEMA makao makuu Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Polisi wamewablock viongozi wa CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee...
  11. JamiiForums Tanzania Mbona Kabendera hakuchangiwa? (maswali tata michango CHADEMA)

    Wakati hukumu ya mwanahabari Eric Kabendera imetoka na kuamuriwa Alipe zaidi ya fedha za kiTanzania milioni mia mbili sikuona wanaharakati, wanahabari wala wafadhili wakichangisha fedha. Kwa hukumu hiii iliyotoka dhidi ya viongozi waandamizi wa chama kikuu cha upinzani nchini nimeona ni ajabu...
  12. JamiiForums Tanzania Humphrey Polepole usipotoshe umma, waliofanya maandamano wote walikuwa CHADEMA

    Polepole wewe ni Mkristu na huu ni mwezi wa Kwaresima, kabla hujasema uongo kwaajili ya tumbo lako muogope Mungu.
  13. JamiiForums Tanzania Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Akwilina: Padri Mayanga ataka aliyeua awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania

    WASIFU WA AKWILINA AKWILINI Akwilina Akwilini alizaliwa tarehe 1 April, 1996 katika Kijiji cha Olele-Marangu, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, akiwa ni mtoto wa sita kati ya watoto nane wa familia ya mzee Akwilini Shirima. Akwilina alipata sakramenti mbalimbali katika kanisa Katoliki la...
  14. JamiiForums Tanzania Viongozi wa CHADEMA walioko gerezani waachiwe mara moja bila masharti

    Wanajamvi, Baada ya kumuona ndugu Polepole akikenua meno baada ya kumlipia Dr Mashinji milioni 30 na kutoka gerezani, nimeona kama vile hii hukumu kuna kamchezo fulani hivi kalichezwa ambako kana ukakasi hasa ukizingatia umuhimu wa uhuru wa mahakama pamoja na haki za kisheria za viongozi hao...
  15. JamiiForums Tanzania Umaarufu wa CHADEMA ndani na nje ya nchi wapanda mara nne zaidi kwa masaa 24 tu

    Huu ndio ukweli uliotamalaki nchini Tanzania na nje ya nchi na hasa Ulaya na Marekani , Hakika kila penye giza iko namna ya kupata mwanga . Kwa wale tuliopita vijijini kuna wakati tunachelewa mahali fulani hadi usiku lakini tunalazimika kuendelea na safari kwenye usiku huo wa giza nene...
  16. S

    JamiiForums Tanzania Viongozi wa Chadema msikate tamaa; hata Nyerere, Mandela nk walihukumiwa kwenda jela na serikali zilizokuwa madarakani - na leo tunajua haikuwa halali

    Historia ina mambo ya ajabu sana. Binafsi huwezi kunishawishi hata chembe kwamba kweli viongozi wa Chadema walifanya makosa, na hata kama kuna chembe ya makosa katika mambo waliyoshitakiwa, walistahili adhabu walizopewa. Ninaamini kwa dhati kwamba adhabu walizopewa, kama hazina maagizo kutoka...
  17. JamiiForums Tanzania Mbuge wa CHADEMA, Catherine Ruge apata ajali asubuhi ya leo akitokea Dar

    Mbunge wa CHADEMA na Mhazini wa Bawacha Mhe Catherine Ruge amepata ajali mbaya asubuhi hii akitokea Dar es Salaam kwenye kesi fake za Viongozi wa Chadema Taarifa za awali Mhe. Ruge anamaumivu makali kwenye Mguu pamoja na kifuani. ======= Mbunge Catherine Ruge (CHADEMA) ambaye pia ni Mhazini wa...
  18. JamiiForums Tanzania Faini ya Milioni 350 dhidi ya viongozi wa Chadema itumike kuwalipa fidia wazazi wa Akwilina

    Hukumu iliyotolewa na hakimu wa mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam ikiwataka viongozi wa Chadema walipe faini ya shilingi milioni 350 itumike kuwalipa fidia wazazi wa marehemu Akwilina Akwiline. Haingii akilini hii pesa kurudi serikalini wakati waathirika wakubwa wa mauaji hayo yaliyofanywa...
  19. JamiiForums Tanzania Lucas Mwampiki, na Hussein Wasoha Madiwani wa Chadema Mkoa wa Mbeya wamehamia CCM

    Wakati tunaendelea kupata taarifa za hukumu kutoka Mahakama ya Kisutu Napokea taarifa kutoka Mbeya kuwa Madiwani wawili wa CHADEMA, Lucas Mwampiki wa Kata ya Mwakibete ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa madiwani wa Chadema mbeya pamoja na Ndugu Hussein Wasoha ambaye alikuwa diwani wa kata ya...
  20. JamiiForums Tanzania Michango kuwanusuru viongozi: CHADEMA imekubali hatia?

    Hili jambo linafikirisha. Nimefuatilia mwenendo wa kesi ya mauaji ya Akwilina tangu mwanzo mpaka hukumu yake iliyotolewa leo katika Mahakama ya Kisutu, Dar. Kukubali kulipa faini bila kukata rufaa, ni kwamba viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekubaliana na hukumu kwamba wanayo hatia ya...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…