Wazo nzuri kuchangisha Tsh 350m kuwaokoa na kifungo viongozi CHADEMA ilikuwa pamoja na Mashinji. Itakuwa uungwana zaidi Tsh 30M kuirudisha CCM

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
CHADEMA mlionesha uugwana mkubwa sana kwa kutuchangisha Tsh 350m kwa wahukumiwa wote hata aliyekuwa katibu Mkuu wenu aliyewakimbia. Hii iliwajengea heshima kubwaa kwa kuonesha kuwa mlithamini mchango wake na isitoshe kesi aliyohukumiwa ilitokana na kuwa kiongozi wa CHADEMA kipindi hicho.

Naamini hata kama CCM wasingewahi kumlipia naamini mngetumia michango tuliyowachangia mngemlipia kabla hata ya Mbowe kama mlivyofanya kwa viongozi wengine. Ushauri wangu kwa kuwa akaunti ya CCM inajulikana ingizeni 30m sehemu ya michango yetu iliyobaki kwenye akaunti ya CCM kama kuwarudishia pesa yao. Kama hakuna salio tuchangisheni tena.

Atendaye mema hulipwa na Mungu na malipo yake ni makubwa. Nawasilisha.
 
CCM wangekuwa waungwana hela zote zingepelekwa CHADEMA ili walipiwe kwa pamoja wao wakafanya ubaguzi! Zile za Msigwa walizodai wameliwa wao kupitia ndg Mh Rais basi wafuatilie ili wapunguze hata wakulima wa korosho
 
Muandiko wa Chakubanga.
FB_IMG_1583233843914.jpg
 
Zilichangwa kwaajili ya pocket money ya mashinji ama kuwatoa magereza?
Kuwa serious na vitu vya msingi. Pesa ifikishwe ilipokusudiwa.
Ilikua ni deni ama? Licha ya ccm kuwabagua wengine akiwemo cousin wa taifa msigwa bado unashauri apatiwe 30m kama nani na kwaajili ya nini
Na pesa imechangwa kuyokana na mahitaji. Kwqmba unatuambia tuendelee kuchanga ama ili ipatikane 30?
Aaagghh bye


Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA mlionesha uugwana mkubwa sana kwa kutuchangisha Tsh 350m kwa wahukumiwa wote hata aliyekuwa katibu Mkuu wenu aliyewakimbia. Hii iliwajengea heshima kubwaa kwa kuonesha kuwa mlithamini mchango wake na isitoshe kesi aliyohukumiwa ilitokana na kuwa kiongozi wa CHADEMA kipindi hicho. Naamini hata kama CCM wasingewahi kumlipia naamini mngetumia michango tuliyowachangia mngemlipia kabla hata ya Mbowe kama mlivyofanya kwa viongozi wengine. Ushauri wangu kwa kuwa akaunti ya CCM inajulikana ingizeni 30m sehemu ya michango yetu iliyobaki kwenye akaunti ya CCM kama kuwarudishia pesa yao. Kama hakuna salio tuchangisheni tena. Atendaye mema hulipwa na Mungu na malipo yake ni makubwa. Nawasilisha.
Pesa zimechangwa 312m siyo 350 kama unavyodai. Kama unataka nenda ikawhimize watu wachange then uwapelekee ccm
 
Back
Top Bottom