Viongozi wa Chadema msikate tamaa; hata Nyerere, Mandela nk walihukumiwa kwenda jela na serikali zilizokuwa madarakani - na leo tunajua haikuwa halali

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Historia ina mambo ya ajabu sana. Binafsi huwezi kunishawishi hata chembe kwamba kweli viongozi wa Chadema walifanya makosa, na hata kama kuna chembe ya makosa katika mambo waliyoshitakiwa, walistahili adhabu walizopewa.

Ninaamini kwa dhati kwamba adhabu walizopewa, kama hazina maagizo kutoka juu, basi zimetolewa katika mazingira ambayo yametawaliwa (kuwa influenced) na aidha ushabiki wa kisiasa au kijipendekeza kwa uongozi wa awamu ya tano kwa mhimili wetu wa Mahakama. NInakumbuka sana kisa cha hukumu ya Sugu, ambapo hakimu aliyetoa hukumu dhidi ya Sugu alikuwa so unprofessional alipaswa hata kufukuzwa kazi. Sidhani kama hilo lilifanyika. In the case of Sugu, the magistrate was simply so keen, naive and hasty in showing his allegiance to the ruling party that he completely forgot to be professional.

Hukumu hii imenikumbusha kwamba kuna wakati Nyerere alikamatwa na serikali ya kidhalimu ya wakoloni na kwa kutumia sheria zilizokuwapo kwa jinsi walivyotaka, walimtia hatiani Nyerere. Vile vile kwa Mandela, serikali ya Makaburu kwa kutumia sheria zilizokuwapo walivyotaka, walimtia Mandele na wengine hatiani.

Kwa hiyo si ajabu kwamba leo hii, mhimili wa Mahakama unaweza kutumia sheria za Tanzania zilizopo wanavyotaka ili kuwatia viongozi wa Chadema hatiani. Hilo liko wazi.

Ndio maana basi, kwa kuwa mimi ni uamini mkubwa wa kuwa na serikali zenye kufuata haki na usawa, na ninaechukia sana mtu yeyote kuonewa, natoa wito kwa viongozi wa Chadema kutokata tamaa kuwapigania wananchi. Ukweli ni kwaba ni wengi waiojua kwamba viongozi wa Chadema si tu wanawapigania wanachama wao wa Chadema, bali hata wale wa CCM na Tanzania kwa ujumla. Huenda siku moja hilo litakuja kuwa wazi.

Nina uhakika kwamba hukumu hii dhidi ya viongozi wa Chadema imewatia hasira Watanzania wengi, hata wale ambao si wanachama wa Chadema. Ni hukumu ambayo imetoa mtikisiko hata nje ya mipaka ya nchi yetu. Ni hukumu ambayo kwa wengi imewafanya waanze kuona rangi halisi (true colours) za serikali ya Tanzania iliyopo madarakani. Ni hukumu ambayo inaweza ikawa imeweka chachu mpya ya mkabiliano wa kisiasa dhidi ya chama tawala cha CCM. Ni hukumu ambayo si hukumu dhidi ya Chadema tu, bali pia dhidi ya CCM na serikali yake ya awamu ya tano.
 
Mashinji alipiwa Milioni 30 na CCM “Tunaenda kumtoa gerezani” (+video)

Pascal Mwakyoma TZA · 10 minutes ago

[https://millardayo]
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kufata utaratibu, wa kulipa faini ya Sh milioni 30 ili kumnusuru Dr. Vicent Mashinji aliyetiwa hatiani jana.
Polepole amefikia hatua hiyo baada ya Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwatia hatiani viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe na wenzake wanane.
“Tayari tumeshapewa control namba, tunaenda kulipa kisha tutarudi Mahakama ya Kisutu ili tupewe utaratibu wa kwenda kumtoa gerezani” Polepole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Historia ina mambo ya ajabu sana. Binafsi huwezi kunishawishi hata chembe kwamba kweli viongozi wa Chadema walifanya makosa, na hata kama kuna chembe ya makosa katika mambo waliyoshitakiwa, walistahili adhabu walizopewa.

Ninaamini kwa dhati kwamba adhabu walizopewa, kama hazina maagizo kutoka juu, basi zimetolewa katika mazingira ambayo yametawaliwa (kuwa influenced) na aidha ushabiki wa kisiasa au kijipendekeza kwa uongozi wa awamu ya tano kwa mhimili wetu wa Mahakama. NInakumbuka sana kisa cha hukumu ya Sugu, ambapo hakimu aliyetoa hukumu dhidi ya Sugu alikuwa so unprofessional alipaswa hata kufukuzwa kazi. Sidhani kama hilo lilifanyika. In the case of Sugu, the magistrate was simply so keen, naive and hasty in showing his allegiance to the ruling party that he completely forgot to be professional.

Hukumu hii imenikumbusha kwamba kuna wakati Nyerere alikamatwa na serikali ya kidhalimu ya wakoloni na kwa kutumia sheria zilizokuwapo kwa jinsi walivyotaka, walimtia hatiani Nyerere. Vile vile kwa Mandela, serikali ya Makaburu kwa kutumia sheria zilizokuwapo walivyotaka, walimtia Mandele na wengine hatiani.

Kwa hiyo si ajabu kwamba leo hii, mhimili wa Mahakama unaweza kutumia sheria za Tanzania zilizopo wanavyotaka ili kuwatia viongozi wa Chadema hatiani. Hilo liko wazi.

Ndio maana basi, kwa kuwa mimi ni uamini mkubwa wa kuwa na serikali zenye kufuata haki na usawa, na ninaechukia sana mtu yeyote kuonewa, natoa wito kwa viongozi wa Chadema kutokata tamaa kuwapigania wananchi. Ukweli ni kwaba ni wengi waiojua kwamba viongozi wa Chadema si tu wanawapigania wanachama wao wa Chadema, bali hata wale wa CCM na Tanzania kwa ujumla. Huenda siku moja hilo litakuja kuwa wazi.

Nina uhakika kwamba hukumu hii dhidi ya viongozi wa Chadema imewatia hasira Watanzania wengi, hata wale ambao si wanachama wa Chadema. Ni hukumu ambayo imetoa mtikisiko hata nje ya mipaka ya nchi yetu. Ni hukumu ambayo kwa wengi imewafanya waanze kuona rangi halisi (true colours) za serikali ya Tanzania iliyopo madarakani. Ni hukumu ambayo inaweza ikawa imeweka chachu mpya ya mkabiliano wa kisiasa dhidi ya chama tawala cha CCM. Ni hukumu ambayo si hukumu dhidi ya Chadema tu, bali pia dhidi ya CCM na serikali yake ya awamu ya tano.
FB_IMG_1583859428848.jpg
 
Du Nyerere kanyong'onyea hadi anatia huruma. Na hao ndio wanasheria waliokuwa wakimteteta? Hata hivyo hakukata tmaa, na alikuja kuwa raisis. Labda Chadema na watatoa raisi siku moja, wasikate tamaa!

1583920681523.png
 
Back
Top Bottom