CHADEMA hamkujua kwamba Ulinzi wa Magereza ni kama Ulinzi wa Ikulu? Wangetoroka wafungwa kwenye maandamano yenu nani angewajibika?

Sep 4, 2019
94
1,000
Nashindwa kuelewa nini maana ya siasa kwamba inafikia hatua watu wazima na akili zao wanashindwa kujua mipaka ya majukumu yao.

Kwanini msitambue wala kujua mambo hatari kwenye usalama wa nchi?

Vyovyote mfanyavyo, msivuke msitari mwekundu, si tu mtaumizwa bali pia mtauliwa kabisa na kutoweshwa Duniani.

Miongoni mwa mambo ya hatari ni pamoja na kuandama kwenda Ikulu au Magereza bila kibali, msirudie kabisa.
 
jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
3,949
2,000
Kama ccm wanaruhusiwa kuingia ndani ya gereza kutoa mtu wao kwanini chadema wanyimwe haki ya kusogelea mlango wa gereza? chanzo cha tatizo ni ccm na serikali yake.
 
chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
13,433
2,000
Nani aliandamana? Je kufika kwa wingi nje ya gereza kumpokea mwenyekiti wetu ni maandamano? Unaelewa maana ya maandamano.

Kwa kigalatia je unaweza kutofautisha protests vs demonstrations vs welcome home?
 
nkese

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
2,403
2,000
Huwa napata shida sana kupata maneno sahihi ya kuelezea mtu mwenye mawazo na fikra kama huyu jamaa. Sijui hizo shule na kwingineko walikopita pita na kusoma soma walofaulu, walihitimu au walimaliza!
Hivi usalama kuwa hatarini ni watu fulani tu kuonekana sehemu hizo na wengine ni sawa tu au?

Kweli bora usionje hata hiyo nusu elimu ya ki-ccm itolewayo kwenye makambi ya kigaidi kuliko kuwa kama huyu. Ni hatari zaidi ya corona.
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
6,833
2,000
Na bado ksma viongozi wa CHADEMA hawatatumia busara za kiutu uzima na uongozi.

Mchungaji aliyewatembelea E.Bulaya H. Mdee bospitali wanakotibiwa majereha waliyoyapata katika hekaheka ya kumpokea M/Kiti wao kutoka gerezani, ni ujjmbe tosha wa kuzingatia. Msikilize.

Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
21,850
2,000
Ungetegemea Wabunge wawe na busara zaidi, Halima si alitoka kabla ya wenzake sasa alifuata nini tena kule gerezani? Kiherehere chake kimemponza. Serikali zote duniani kama hufuati sheria utakula mkong'oto.
Eti ili wapate picha za huruma wampelekee Lisu azisambaze kwa wazungu wake waweze kuchukua dola, ha ha ha. Ukweli ni kwamba wataendela kutandikwa kama wahalifu wengine tu.
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,573
2,000
Nashindwa kuelewa nini maana ya siasa kwamba inafikia hatua watu wazima na akili zao wanashindwa kujua mipaka ya majukumu yao.

Kwanini msitambue wala kujua mambo hatari kwenye usalama wa nchi?

Vyovyote mfanyavyo, msivuke msitari mwekundu, si tu mtaumizwa bali pia mtauliwa kabisa na kutoweshwa Duniani.

Miongoni mwa mambo ya hatari ni pamoja na kuandama kwenda Ikulu au Magereza bila kibali, msirudie kabisa.
Wenzako walihitaji spotlight, na wameipata😂😂
 
Mudi ayub

Member
Jul 15, 2019
55
125
Achakuandika ujinga. Viongozi hawa walisharuhusiwa kuingia gate la kwanza walipokuwa wanaelekea gate no 2 umbali km mita 500 ndipo wakaanza kushambiliwa. Ss jiulize kwann waliwaruhusu kupita n magari yao gate no 1?

Na hapa huwezi kupita mpaka ujiandikishe kisha gate lifunguliwe. Acha ujinga. Hii ilipangwa. Halafu watu hawa hawakuwa n silaha. Ni ubishi gani Halima anawezakufanya mpaka kuvu kubwa itumike ya kumvunja mkono kivile?
 
blance86

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
1,364
2,000
Mkuu nani amekuambia chadema waliandamana?hivi ulimuona polepole alivyoingia pale segerea?kama vyote hivi hukuviona bc kaa kimya tu.Chadema walikuwa wanasubiri mbowe atolewe nje waondoke nae ile furaha ya kumuona tu wakaanza kushangili ndio kipigo kilipoanzia hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
5,445
2,000
Nani aliandamana? Je kufika kwa wingi nje ya gereza kumpokea mwenyekiti wetu ni maandamano? Unaelewa maana ya maandamano.

Kwa kigalatia je unaweza kutofautisha protests vs demonstrations vs welcome home?
Acha ujinga jomba...Yani hata taratibu za usalama unataka ufundishwe. Kheeee...tumia akili yako ya kuzaliwa..taratibu mnaelezwa bado hamzitaki Basi tungeni za kwenu ndio mnapokutana na mkono wa sheria
 
Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
5,445
2,000
Niliwahi kusema ukitaka kumnasa Ester Bulaya subiri alipo halima mdee. Cheki alivyonasa. Atakufa atamuacha Mdee.

Ye haoni kina Esther Matiko, Joyce Mukya, Suzan Kiwanga na wamama wenzao wametulia. Ye mapenzi yanampelekesha hadi hajui ashike nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hehehehehe nimepita tu..kumbe ndio maana
 
dolomon

JF-Expert Member
Jun 5, 2018
546
1,000
Mbona haujiulizi walipotoka mwanzo mbona hawakupigwa? Mbona Mbowe ambaye ndio alikuwa muhusika mbona hakuguswa?

Ukikaidi amri,baya litakufika tu.
Kama ccm wanaruhusiwa kuingia ndani ya gereza kutoa mtu wao kwanini chadema wanyimwe haki ya kusogelea mlango wa gereza? chanzo cha tatizo ni ccm na serikali yake.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom