Geeque
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 936
- 316
Hukumu iliyotolewa na hakimu wa mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam ikiwataka viongozi wa Chadema walipe faini ya shilingi milioni 350 itumike kuwalipa fidia wazazi wa marehemu Akwilina Akwiline. Haingii akilini hii pesa kurudi serikalini wakati waathirika wakubwa wa mauaji hayo yaliyofanywa na jeshi la Polisi la Tanzania ni familia ya marehemu Akwilina.
Ni muda muafaka kwa familia ya marehemu Akwilina kutafuta mwanasheria mzuri na kufungua kesi ya madai ya kifo cha mtoto wao mpendwa dhidi ya Jeshi la Polisi Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kesi hii ya madai ilenge kudai fidia kutokana na pesa zitakazopatikana kupitia faini hiyo.
Rais Magufuli amekuwa akijipambanua kuwa yeye ni rais wa wanyonge, basi huu ndio muda muafaka kuonyesha kwa vitendo upendo wake kwa wanyonge kwa kuagiza pesa zote zitakazopatikana kutokana na faini dhidi ya viongozi wa Chadema zilipwe kwa familia ya marehemu Akwilina Akwiline.