Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama tawala nchini Tanzania na chama cha pili kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya Chama cha True Whig cha Liberia. Kilianzishwa mwaka 1977, baada ya kuunganishwa kwa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar.
Nimepitia mitandao ya kijamii leo, na habari zilizotamalaki ni makada wa CCM kuchukua fomu. Ni wazi sasa wimbo wa "Tunazima zote, tunawasha kijani" leo umepata maana halisi.
Mwitikio huu mkubwa unatoa uthibitisho wa ukweli wa takwimu kuwa hiki ndicho chama chenye wanachama wengi zaidi nchini...
Prof. Adolf Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amechukua fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Rombo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025
Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Rombo, Massoud MeliMeli
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Catherine Magige amechukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kuwakilisha wanawake kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025
Catherine amekabidhiwa fomu hiyo leo Jumamosi, Juni 28, 2025...
Mapema leo Abdallah Said Kirungu alifika Ofisi za CCM Wilaya ya Ulanga iliyopo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuchukua fomu ya kutia nia ya ubunge katika Jimbo la Ulanga.
Imefika kipindi tukubaliane jambo moja tu, kuwa nchi hii haiongozwi tena kwa Katiba na Sheria bali utashi wa watu binafsi.
Kama si hivyo basi tukubaliane tu jambo moja kuwa wananchi wote wa Tanzania ni vigaragosi na mazwazwa kiasi kwamba Viongozi wanaweza jifanyia jambo lolote lile bila kuogopa...
Hemed Shabani Nkunya, Mfanyabiashara na Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbweni Mpiji mkoani Dar es Salaam ametia nia ya kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kawe mkoani humo kwa tiketi ya CCM.
Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu...
Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma, leo ameibuka katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita kwa lengo la kuchukua fomu ya kuwania ubunge kwa awamu nyingine.
Musukuma aliwasili katika ofisi hizo majira ya saa 9:35 alasiri, akiwa ameambatana na Katibu...
Ubunge wa kupewa, kama ambavyo iliotwa na NCCR Mageuzi mwaka 2020, ni kitu kisichotekelezeka; japokuwa ahadi yake huwa ni tamu sana masikioni mwa vyama vya upinzani visivyotaka kuchutama ili kuokota vya chini.
Sababu kubwa ya ni kwanini hichi kitu ni kigumu kutekelezeka ni kwamba, ndani ya...
Mwenyekiti wa Ccm Mbeya Mjini Humphrey Nsomba amechukua Fomu kugombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025...
Wakati uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa wanaotaka kugombea ubunge na udiwani, ukianza leo Jumamosi, Juni 28, 2025 kwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), harufu ya mchezo mchafu imeanza kusikika.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wagombea wanaokwenda kwenye ofisi za CCM kwa ajili ya kuchukua fomu...
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe Bwana Aloyce Mwenda amechukua fomu kuomba ya Ubunge katika Jimbo la Lupembe.
Bwana Mwenda amesema Yupo tayari kuwatumikia Wananchi wa Jimbo La Lupembe endapo Chama Cha Mapinduzi(CCM) kitampa ridhaa ya kuwa Mgombea Ubunge.
Chanzo: Uplands Fm
Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amechukua fomu ya kuwania ubunge katika Jimbo la Ilongero mkoani Singida.
Nyalandu amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo zamani likiitwa Singida Kaskazini kwa vipindi viwili, amekabidhiwa fomu hiyo mapema leo Juni 28, 2025 na Katibu wa...
Aliyekuwa Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Mtumba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akieleza kuwa endapo atapata ridhaa ya chama, atakuwa tayari kuwania nafasi hiyo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
Akizungumza mara...
Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Iringa Fadhili Ngajilo ametangaza nia ya kutaka kugombea Ubunge Kuelekea katika uchaguzi Mkuu wa Oct 2025.
Ngajilo ametoa azma yake ya kulitaka Jimbo la Iringa Mjini mara baada ya kujitokeza katika Ofisi za CCM Wilaya ya Iringa Mjini Leo kuchukua Fomu ya Ubunge na...
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Naghenjwa Kaboyoka amejiunga na chama cha ACT Wazalendo leo Juni 28 Dar es Salaam.
Kaboyoka aliyewahi kuwa Mbunge wa Same Mashariki 2015-2020 amepokelewa leo na Kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu kwenye ofisi za makao makuu Magomeni.
Mwaka 2020 Kaboyoka...
Rais wa Klabu ya Yanga Injinia Hersi Said leo Juni 28, 2025 amechukua rasmi fomu ya kuwani Ubunge katika Jimbo la Kigamboni lilipo Jijini Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Hersi amekua miongoni mwa watu mashuhuri wanaokubalika katika jamii kutokana na uongozi wake...
Ndugu zangu Watanzania,
Nimeona niweke uzi huu uwe maalumu kwa ajili ya matukio yote ya uchukuaji na urejeshaji wa Fomu za Ubunge kupitia CCM Katika Majimbo yote Tanzania Bara.
Hii itasaidia kufahamu nani na nani wamechukua Fomu sehemu Fulani. Lakini pia baadaye kutakuwepo na Uzi wa Majina...
Aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini 2010 - 2020 Mchungaji Peter Msigwa amechukua fomu za kugombea Ubunge Jimbo la Iringa Mjini katika ofisi za CCM wilaya na kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa mjini Hassan Makoba.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu Mchungaji Msigwa alisema kuwa...
Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kilosa kimetoa onyo kwa wagombea wa nafasi ya Udiwani na Ubunge ndani ya Chama hicho kutojihusisha na Vitendo vya rushwa kwani ni kosa kufanya hivyo.
Wito huo umetolewa na Katibu wa CCM Wilaya hiyo Jonus Mfaume wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.