Katika pita-pita zangu nimekutana na vijana wanaouza mishikaki kwa kutumia vitoroli vyenye matairi mawili na jiko la mkaa kwa juu, hapo hapo juu kwa pembeni wanaweka mishikaki iliyochomwa tayari. Wanauza mishkaki ya ng’ombe, maini, figilisi, kuku na soseji, vyote kwa jero jero na mara nyingi...