Kama ingekuwa ni mpira wa miguu, basi tungesema CDM walikosa nafasi nyingi za kufunga kuliko CCM, kibaya zaidi nyingi zilikuwa penati lakini wapigaji wakapaisha mipira au wakampasia kipa badala ya kufunga. Nafasi kama hizi ni nadra sana kujirudia. hakika CDM mtaujutia mwaka 2011.
Soma signature yangu hapo chini, JK kasimama mwenyewe golini lakini CDM mnapewa penati kila kukicha lakini mnashindwa kufunga magoli, nani alaumiwe yule aliyeko golini au nyie mnaokosa magoli ya penati.
Chukueni hatua kama mnaona hafai siyo kulalamika kwenye keyboards
Kwani hao wananchi wamechukua hatua gani zaidi ya kumtukana? wakiambiwa waandamane hawatoki wanaogopa mabomu, wengine wanabaki kuchezea keyboard zao na matusi kibao. kwa nini msiige Misri, Tunisia na Libya?
Fikiria angekuwa Mwalimu Julius Nyerere, watu wampande mpaka Kichwani kama wanavyofanya kwa JK, angalau Mwinyi kidogo mngemchokonyoa angevumilia, lakini Mzee BM thubutu.
JK anaongoza nchi ikiwa na upinzani uliokomaa angalau kwa kiasi kikubwa kuliko pale mwanzo kwa sababu ya CDM kujaza wasomi...
CDM wabunge wa shoka wanawake hawazidi watano wengine wote walipata ubunge wao kwa vimemo na mashinikizo.
Nawataja, Regia, Halima, Rose Kamili, Lucy Kiwanga na mmoja nimemsahau.
Ungalijua ninachomaanisha usingeandika ulichoandika. Je Lowasa ni muislamu? Je kanisa kumpatia utukufu huku nchi nzima akituhumiwa ufisadi ni sahihi? au kanisa nalo liko kwa ajili ya matajiri na mafisadi kama Lowasa?
Mkuu Luteni, Tatizo ni huo muda wa kumobilize watu utatoka wapi kama hatumalizi huu mgogoro? miaka minne iliyobaki inakimbia kama, haitusubiri. na kama ukifikiri kwa umakini, hiyo ni janja ya CCM ili wapate nyundo ya kuwatwangia 2015. Malizeni huu mgogoro ili mpate muda wa kumobilize wananchi...
Watakuchagua tu kama watakuelewa, isije ikaja semwa ya Heri ya Misri kuliko kuishi hapa Jangwani. angalizo tu mkuu, wananchi wa huku kwetu Maganjo wanasema hapendwi mbunge bali maendeleo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.