CHADEMA Sumbawanga Mjini yakanusha upotoshaji uliofanywa na Stella Manyanya na CCM mkoa wa Rukwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Sumbawanga Mjini yakanusha upotoshaji uliofanywa na Stella Manyanya na CCM mkoa wa Rukwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ptz, Dec 27, 2011.

 1. P

  Ptz JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Heshima yenu wanaJf! Chama cha Demokrasia na Maendeleo Sumbwanga mjini kimekanusha upotoshaji uliofanywa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa bw Matete kuwa bw Godfrey Shayo iliyekihama Chama hicho na kujiunga na CCM alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA wilaya. Taarifa za uhakika toka ofisi ya CHADEMA Sumbawanga mjini ni kuwa bw Shayo alishawahi kushika wadhifa wa mwenyekiti wa baraza la Vijana “BAVICHA” Sumbawanga mjini tena siyo wilaya nzima ya Sumbawanga kwani wilaya ya Sumbawanga ina wenyeviti wawili wa BAVICHA akiwepo wa Sumbawanga mjini na Sumbawanga vijijini. Kumbukumbu zinaonesha kuwa katika kipindi cha uongozi wa bw Shayo kama mwenyekiti wa BAVICHA Sumbawanga mjini alibainika kuwa mdanganyifu kwa kutumia mamlaka yake kuchangisha pesa toka kwa wafadhiri na kuzichakachua. Kwa mjibu wa Katibu wa CHADEMA wilaya bw Kasikila upo ushahidi uliyomtia bw Shayo hatiani wa kuchangisha kiasi cha Tsh 48,000/ na kuzitafuna, ni kwa ubadhirifu huo ndo kikao rasmi cha BAVICHA Sumbawanga mjini cha tarehe 16/07/2011 kiliamua kwa manufaa ya chama na kwa kauli moja kumvua uongozi bw Shayo baada ya kupoteza sifa za kuwa kiongozi. Mhutasari wa kikao cha kutokuwa na Imani na Bw Shayo. Tazama kiambatanisho nimeambatanisha na makala hii.

  Katika hafla kubwa yenye sura ya kimkoa iliyoandaliwa na CCM Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya kumkaribisha bw Shayo CCM na kurushwa na Sumbwanga Tv, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa bw Matete alikaririwa akitamka kwa ujasiri mkubwa kuwa bw Shayo ametokea CHADEMA kama mwenyekiti wa wilaya na kuongezea kuwa zaidi ya kuwa mwenyekiti wa wilaya Sumbawanga pia alikuwa akiongoza wilaya ya Nkasi kwa wadhifa huo huo, Taarifa sahihi ni kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Sumbwanga ni bw Godfrey Katata, na mwenyekiti wa sasa wa BAVICHA tangu tar 18/07/2011 ni bw Conwell Kakwaya, kwa mjibu wa mjumbe wa Baraza la vijana CHADEMA taifa mkoa wa Rukwa bw Frank Joseph Fumpa huu ni upotoshaji wa hali ya juu kwani bw Shayo baada ya kuvuliwa uongozi alibaki akitapatapa mara baada ya kukosa platform CHADEMA na kwa maana hiyo ndiyo maana akaona ni bora ahamie CCM, rekodi sahihi ni kuwa bw Shayo amehamia CCM kama mwanachama wa kawaida wa CHADEMA tena mwanachama mwenye doa au kovu la utaperi. CCM wanapongezwa kwa kuandaa hafla kubwa iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyaya, wakuu wa wilaya, wabunge, watendaji wakuu wa mkoa, na halmashauri zote za mkoa, (Mpanda, Nkasi, Sumbawanga vijiji na Manispaa) kwa ajili ya kumkaribisha bw Shayo, lakini wajue si sahihi sana kufanya hivyo kwa sasa kwani kutokana na hali mbaya ya maisha wanayokabiliwa wanarukwa ni fedheha kwa CCM na Serikali kwa ujumla. Ikumbukwe kuwa mkoa wa Rukwa una wenyeji wanaotegemea kilimo lakini kwa sasa pamoja na kuwepo na sera ya kilimo kwanza wakulima wanashindwa kununua pembejeo, kwa sasa mfuko wa mbolea Sumbwanga ni 50 elfu @ kilo 50 (mbolea ya Ruzuku) na mbolea y a kuuzwa tu kwa kawada ni shilingi 82 elfu hadi 90 elfu, barabara ni mbovu hazitumiki kwasasa, mafuta ni shida siku ya x mas lita moja ya mafuta ya petroli ilifikia shilingi elfu 7. Namuomba Stella Manyanya ayafanyie kazi haya na si propaganda za kisiasa, ni vema kama ana nia ya kuendeleza mkoa hizo awaachie wakina Tambwe Hiza
  CHADEMA Sumbawanga mjini imekanusha pia upotoshaji mwingine kuwa bw Shayo ameihama CHADEMA eti kwa sababu ya ukabila na udini, upotoshaji huo unajibainisha kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, viongozi wa madhehebu ya kikristo walijiingiza katika kampeni makanisani kwa kumpinga mgombea wa CCM bw AESHI kwa kuwa ni muumini wa kiislam, hoja hii inahitimishwa kwa kusema kuwa CHADEMA Sumbwanga ni chama cha wakristo, Hoja hii si sahihi na kwamba udini Sumbwanga mjini haupo kwa vyama vyote viwili yaani CCM na CHADEMA. Chachu ya udini Sumbawanga iliingizwa kwa wapiga kura katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana na viongozi wa kampeni wa CCM bw Matete( mwenyekiti CCM mkoa),bw Tung’ombe (katibu mwenezi wilaya), bw Aeshi (mgombea wa ubunge), na wengineo. Hali ilikuwa mbaya sana pale bw Aeshi mgombea wa ubunge CCM alipoishiwa sera kwa wapiga kura na kujinadi katika mikutano kadhaa ya hadhara yeye kama YESU, na kumwita Kikwete MUNGU na Madiwani ROHO MTAKATIFU, jambo hili lilionekana kama fedheha na dharau kubwa kwa wakristo, kanisa katoriki lilitoa onyo kali kwa bw Aeshi na kutoa ujumbe wa kuombwa msamaha kwa dharau hiyo, jambo ambalo halikuwezekana, hali iliendelea kuharibiwa zaidi pale bw Matete kutumia advantage ya yeye kusoma seminari na mapadre wa kikatoriki na kuwa karibu nao kwa muda na kutumia mikutano ya kampeni kuwaita mapadre wahuni na wazinzi na kuwa yeye anawafahamu vizuri. Kauli hizi alizipata mh Pinda na kuwaamuru wahusika waombe msamaha kwa makanisa, kwa bahati mbaya hawa kufanya hivyo. Mh Pinda aliamua mwenyewe kuja Sumbawanga kuongea na viongozi wa dini wa kikristo kadhaa na kuamua mwenyewe kuapanda jukwaani katika uwanja wa Rukwa high school na kueleza yote kwa kujaribu kumtetea bw Aeshi kwa kusema alikuwa alijaribu kuomba kura kwa kutumia mafiga matatu akajisahau akatamka YESU,MUNGU na ROHO MTAKATIFU, lakini Pinda alikiri kuwa ni kosa kubwa na hasa kwa Aeshi ambaye si dhehebu hilo, mwishowe mh Pinda aliomba msamaha kwa niaba ya CCM na wote waliohusika.Mh Pinda aliondoka, lakini bado wahusika hawakukoma na hadi sasa kama ilivyoelezwa na bw Shayo bado hoja hii iko katika kauli za viongozi wa CCM mkoa. CHADEMA Sumbawanga mjini inatamka kuwa haihusiki kwa hili la udini, CHADEMA iko imara na itaendelea kuwa imara zaidi Sumbawanga mjini. Naomba kuwasilisha wakuu.
   
 2. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  "mchawi anapokaribia kufa husema mabaya yote aliyoyatenda" nenda shayo nenda....!
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Ccm wakifanikiwa kumpata mwanachama mmoja toka chadema wanashangilia sana na kufanya sherehe kubwa za mapokezi.
  Hii ni dalili ya wazi kwamba chadema imewakalia kooni kiasi kwamba hawana pa kutokea. Lakini kwakuwa shayo ameonyesha tabia inayopendwa na ccm hawaoni taabu kumkaribisha kwa mikono miwili.

  Sasa shayo anaituhumu chadema kwa ukabila baada ya kutimuliwa, kwani siku hizi kuna ukoo wa shayo kwa wafipa?tena hela yenyewe sh. 48,000 huyu mangi anaonekana alikuwa na njaa kali sana.
   
 4. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  amefika kwa mafisadi wenyewe.wamfundishe kazi sasa
   
 5. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  jina lake ni shayo, atakuwa amewatapeli kwamba yeye ni mwenyekiti ili apate dau kubwa, kifupi ccm wameingizwa mjini na mangi huyo, na bado mtaliwa sana pesa zenu kuelekea uchaguzi wa 2015, maana mnaweweseka na nguvu ya cdm, kwahiyo mkisikia fulani ni kiongozi wa cdm mnapanda dau kubwa bila ya kufanya utafiti kwanza, jamani kuweni makini na kina shayo, hizo mnazowahonga ni pesa zetu mnazozifuja hali yetu si mnaona ni mbaya? muwe na huruma jamani
   
 6. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  msiwajibu kupitia JF bali fanyeni mikutano ya hadhara au vyombo vya habari Vya hapo Sumbawanga coz inawahusu sana watu wa Sumbawanga, Mungu awabariki.
   
 7. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashukuru mkuu kwa kutujuza. Inaonesha wameishiwa sera na sasa wanataka kujihalalisha kwa kuwatumia watu kuonesha wanapenda. Ushauri ni kuwa timizeni(ccm) wajibu wenu kwa watz tu basi inatosha hizo mbwembwembwe hazileti tija yoyote. wananchi tunaanda hukumu subirini 2015
   
 8. t

  tweve JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 696
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Magamba tunawajua siku hizi ,wakibanwa sana kwenye siasa wanaanza kupandikiza udini,ukabila na hata ukanda,washindwe na walegee! Shame on magamba!
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  CCM Hawana aibu kila siku wanaumbuliwa kwa uongo wa hao wanaowapokea inapokuja kujulikana walikuwa hawana vyeo hivyo,wanapokea Viwavi wa Kisiasa ,mtindo umepitwa na wakati huo Komaeni mumdai fedha walizotumia kwenye sherehe huyo bibi Kipeperete Stella Manyanya ,Fedha zenu hizo kama anataka kutoa shukrani kwa Kikwete au Pinda amejiabisha walijaribu kumvalisha suti oversize huyo bwana Shayo aonekane wa maana lakini unamwona kabisa alikuwa anaogopa hapo Sumbawanga mjini pana ukubwa gani mpaka watu wasijue kwamba Shayo ni Stellah Manyanya ni matapeli wa Kisiasa
   
 10. T

  Typhord Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kumwangalia tu, unajua jamaa tapeli. sijui kwa nini Eng. Manyanya hakulitambua hilo.
   
 11. P

  Ptz JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Ukanushaji wa upotoshaji huu unafanyika kila mahala palipotumika kupotoshea, kumbuka hapa jamii forum kuna thread mbili zilitaja bw Shayo kuwa kapokelewa CCM kutokea CHADEMA kama mwenyekiti wa wilaya, juhudi zilianza tangu juzi kutumia sumbawanga tv waliorusha hafla ya kukaribishwa bw Shayo na kesho kuna viongozi Wa CDM wameahidiwa kufanya hivyo. Pia watafanya imefanyika kwa Radio ya Chemchem iliyopo Sumbawanga. Ubarikiwe nawe pia.
   
 12. j

  jigoku JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hongera Shayo kwa kuchagua chama kilicho mahiri kwa mambo ya kitapeli na ufisadi,na kwa bahati nzuri najua mpaka sasa umeshawapiga kiasi kadhaa na utawapiga sana komaa huko huko,CDM mziki mnene usiohitaji tune ya kifisadi na utapeli.Nashangaa hata huyo wanaemsemega Eng Manyanya sijui vitunguu hakujua hili na mpaka ukafanikiwa kuwaliza hao Magamba-CCM wa Sumbawanga.
  wanaalikana mkoa mzima kumpata mtu asie mwadilifu na wala hana national influence,je ingelikuwa kumpata Mh Mnyika ingelikuwaje,nadhani serikali ya ccm ingetangaza siku saba za mapumziko na sherehe kwa kwenda mbele,mshindwe na mlegee magamba nyie.
   
 13. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Shayo mwenyewe anaonekana ana njaa vile, kwani hata Mkoti wenyewe umempwaya. Halafu pia hata uso wake unaonyesha kwamba taarifa aliyowasilisha CCM si sahihi. wewe angalia tu uso wako unavyosomeka.
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Ukiona CCM wanafanya sherehe kwa kumpata mwanachama mmoja tena dhaifu wa CDM ujue wameshikwa pabaya mno...vinginevyo nitamshangaa mtu anayeamia CCM kwasasa,na nadhani hata watanzania watamshangaa sana...
   
 15. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  USHAURI>
  Naomba ufanye yafuatayo kama wewe kweli ni kiongozi wa Wanasumbawanga na kuwa unapenda CDM iendelee kuwa rohoni mwa jamii hiyo:-

  1. Ita vyombo vya Habari vyote vya hapo Sumbawanga, waeleze ukweli kama ulivyoeleza humu ndani ya JF
  2. Kama UNAUHAKIKA na USHAHIDI wa hayo aliyoyatenda Bw Shayo akiwa CDM yamwage hadharani ili watu wajue kuwa hajafanya kosa kujiunga na CCM maanake, amerudi kundini kwa wenzake
  3. Hebu waeleze wanasumbawanga waelewe makosa ambayo CCM inayafanya ya kufanya sherehe ya kumkaribisha mtu mmoja ktk chama kwa pesa za Watanzania. Najua CCM haina pesa itakua imechukua pesa aidha toka Halmashauri au Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kufanya ujinga huo. Fedha hizo ni za Wananchi WOTE bila kujali itikadi.
  4. Mkuu wa Mkoa huyo Mama, anafanya makosa (najua yeye ni kada wa CCM) lakini angetenda mambo ya kiserikali zaidi kwa ajili ya Sumbawanga na hiyo kazi akamwachia M/kiti wa CCM wilaya manake hata M/kiti CCM Mkoa ni mkubwa hatakiwi kwenda kumpokea huyo NYANG'AU!

  Kwaheri kwa sasa.
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kama wewe ni mwizi, fisadi, tapeli, mwongo, na mbakaji kimbilio lako ni CCM. Huko siyo tu utapokelewa kwa vifijo bali utahakikishiwa usalama na ulinzi dhidi ya raia wema. CCM, duh !
   
 17. w

  watundawangu JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kuna furaha kubwa kwa CCM kama fisadi mmoja (kama alivyo bwana Shayo) akijiunga na chama hiki cha mafisadi kuliko, welidi 100 wanaobaki wanaobaki kwenye upinzani. sasa kwa nini wasimfanyie sikukuu ikiwa wameongeza mwizi mwingine? Huyo mkuu wa mkoa si kitu si chochote, aliteuliwa tu kutokana na kujuana na mkuu wa kaya. Aibu inakula kwao sasa.
   
 18. k

  kindafu JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
   
 19. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2011
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Wanazoa matapishi ya wengine na kuyaweka mezani kama chakula.
   
 20. k

  kkitabu Senior Member

  #20
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Washindwe na walegee kwa jina la Mwenyezi Mungu anayeishi na kutawala siku zote. Kwa Mwenyezi Mungu upotoshwaji hauna nafasi. Nawasilisha kada wa Chadema.
   
Loading...