Hivi wewe umezaliwa na mwanamke kweli? Huna hata heshima kwa mama yako mzazi. Tena wewe ni mshamba uliekosa exposure kabisa. Unawezaje kusema wanawake badala ya kusema baadhi ya wanawake?huu u - primitive wako unapiga honi kabisa. Karne ya 21 bado unazungumzia kumpiga mwanamke! Pole weee, naona...
Chadema mtakufa na pressure mwaka huu. Zitto mmemfukuza wenyewe lakini bado mmebaki na jinamizi. Mlivyokuwa na upeo finyu mlifikiri kumfukuza kwenye chama chenu utakuwa ndio mwisho wake kisiasa. Kwa haraka sana mliyasahau yote mazuri aliyoyafanya alipokuwa Chadema.
Inashangaza sana kuona kuwa...
Baba yake Faraja alifariki miaka mingi iliyopita. Kama hujui jambo nyamaza kuliko kuzua uzushi. Faraja Kota ni Mbondei wa Muheza na wala siyo Mnyaturu wa Singida. Naona JF kumejaa uzushi tu siku hizi.
Masahihisho kidogo. Jina lake kamili lilikuwa BENJAMIN KIKOROMA. Nilikutana nae Bukoba wakati wa vita vya Kagera, na alikuwa mstati wa mbele wakati ule akiripoti mambo ya vita, akiwa anaandamana na mpiga picha wetu mashuhuri wa wakati ule marehemu VINCENT URIO.
Asili ya jina Tanganyika limetokana na lugha ya kabila la Wabondei. Kwa Kibondei tanga maaa yake ni shamba. Siku za zamani sana kabla ya ujio wa Wajerumani, wakulima wa Kibondei walikuwa na mashamba mbali na vijiji vyao na huko kulikuwa na mapori. Wakulima hao walipokua wanakwenda shamba...
Sasa zile mbwembwe zote za Yeriko zilikuwa za nini? Watu wengine bwana. Yeriko umesahau kabisa ile amri ya 'Usimtendee mwenzako usilotaka kutendewa wewe" Hivi unauhakika gani wewe ' beyond any reasonable dought ' kuwa mh. Zitto ni msaliti? Na kama ikiwa unavyoamini na kufikiria sivyo, utaweza...
Ndugu yangu Fuso, nadhani huna historia sahihi ya mchango wa Winnie wakati wa harakati za ukombozi. Alipofungwa Mandela, hakuna mtu ye yote yule aliyeweza kulitangaza jina lake kama Winnie. Walter Sisulu ambae alikuwa akifanya kazi pamoja na Mandela na ambae alikuwa akifahamika sana vile vile...
Wana Jf wenzangu, Chonde, chonde, chonde. naomba naomba sana, sana, sana, mtu ye yote asijaribu kufanya meditation ya aina yo yote ile bila chini ya uangalizi wa mwalimu, ama mtu aliebobea kwenye elimu hiyo. Mimi kwa mara ya kwanza nilifahamu kuhusu meditation mwaka wa 1973, kupitia vitabu vya...
Wana jf, nashangazwa na uchangiaji wa wengi wenu katika habari tajwa hata baadhi yenu kuhoji kwa nini Zitto hajawashirikisha watu fulani fulani katika kuzisaka fedha zilizofichwa nje. Sijui kama mmeisoma hiyo habari yenyewe mpaka mwisho. Zitto amechaguliwa kuongoza jopo la wataalamu kutoka...
Kwa kuwa hakuna mwanadamu aliekamilika, mzee Mengi anaweza kuwa na mapungufu yake, lakini kwa hili namuunga mkono kabisa. Kwa msimamo ambao Serikali imeuchukuwa, ina maana mpaka umri kiama WaTanzania hatutakuja kuchimba gesi wala mafuta sisi wenyewe. Kwa leo tunasema hatuna uwezo, lakini je...
Utafiti wako wote umekamilika kwa mifano ya wanawake wawili tu katika ulimwengu mzima? Kweli uwezo wako wa kufikiri ni finyu mno. Sasa nakuambia, 'No research, no right to speak '. Wanawake unaowajua duniani ni Ana Makinda na Getrude Mongela tu. Poor you!. Unapozungumzia jinsi mara zote haifai...
Sisemi muende Kigoma kuchukua hiyo dawa, maana sijui kama kweli wanayo, lakini nimeona kwa macho yangu mwaka 2010 huko Asaba, Delta State Nigeria. Nilikua natoka Zenith Bank kuchukuwa pesa kutoka kwenye VISA Card yangu, mara nikasikia milio ya risasi nje ya Bank. Jamaa mmoja alietoka hapo Bank...
Huyu sio mtoto. Huyu ni mtu mzima kabisa. Hakuna mtoto ye yote awe wa mwanadamu ama wa nyani ambae huzaliwa na ukubwa huu. Hebu tazama miguu yake ilivyo mikubwa. Kama ni viatu basi si chini ya namba tano. Mtoto gani anazaliwa na ukubwa huo? Tazama ukubwa wa nyonga na makalio yake. Tuseme labda...
Ally Kombo, Kuwa na vifaa bora sio kuwa na umakini ama ufanisi bora. Mimi mwenyewe mwezi uliopita nilinunua juice ya Azam ya boksi, aina ya 'pineapple' kwa Kiswahili, nanasi. Kwa kuwa nilikuwa na njaa sana, niliibugia hii juice kwa haraka na nilikuwa nainywa kwa mrija baada ya kuitingisha...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.