Zitto arudi na siri ya mabilioni ya Uswisi

Zitto arudi na siri ya mabilioni ya Uswisi

Yaani pesa inayofichwa nje ni mara mbili ya misaada inayoingizwa? Umaskini sijui tutaumalizaje kwa style hii?

kwa style hii umasiki utazidi kwa familia nyingi huku zingne zikiwa maisha ya kifahari kupita kiasi kama ilivyo sasa.

kuwa matajiri wote ni ndoto lakini waboreshe maisha kwa jamii nzima.... na sio kuwa na miradi mikubwa isiyoweza saidia mtanzania wa kawaida na ambayo inanufaisha wachache, mfano migodi nk.
 
nadhan kwa faida ya chadema na wapenda mabadiliko ya kweli zitto ni muda muafaka wa kumuondoa chaman arud ccm..... alishachukua pesa ya umeme wa kuzalisha wa diesel akakaakimya humsikii tena wakat mwazno alikua ndio wa kwanza kupiga vita tanesco kuzalisha umeme kwa mafuta.

alafu amekua akijinasabisha zaidi yeye kama yeye na si chama... ktk mapamabano ya kuwatoa ccm madarakan nguvu ya wengi ndio inahitajika kama yeye anajihisi ni muhimu kuliko chadema he can just go!!!

ameshapoteza credibility kwa wana chadema wa ukweli!!!
 
Eti ataitisha press conference ..Kweli dogo umekwisha sahivi umebaki unawayawaya ka kuku aliyekatwa kichwa,chama chako umekiweka kando,wanachama wenzako hauna habari nao wewe kutwa unacheza ngoma za CCM huku ukifikiri watanzania hawakuoni,wametulia wanakuona unavyogeuka popo huku wakijua mwisho wako

Kwetu kuna ka msemo kanasema 'Ekagenda yonka yahaba',tafuta maana mwenyewe... pesa ulizohongwa ndo zinageuka kitanzi kwako make ulikubali kutumika na wajanja wakakupakata miguuni mwao.
 
Eti ataitisha press conference ..Kweli dogo umekwisha sahivi umebaki unawayawaya ka kuku aliyekatwa kichwa,chama chako umekiweka kando,wanachama wenzako hauna habari nao wewe kutwa unacheza ngoma za CCM huku ukifikiri watanzania hawakuoni,wametulia wanakuona unavyogeuka popo huku wakijua mwisho wako

Kwetu kuna ka msemo kanasema 'Ekagenda yonka yahaba',tafuta maana mwenyewe... pesa ulizohongwa ndo zinageuka kitanzi kwako make ulikubali kutumika na wajanja wakakupakata miguuni mwao.

Anapakatwa haswa
 
Eti ataitisha press conference ..Kweli dogo umekwisha sahivi umebaki unawayawaya ka kuku aliyekatwa kichwa,chama chako umekiweka kando,wanachama wenzako hauna habari nao wewe kutwa unacheza ngoma za CCM huku ukifikiri watanzania hawakuoni,wametulia wanakuona unavyogeuka popo huku wakijua mwisho wako

Kwetu kuna ka msemo kanasema 'Ekagenda yonka yahaba',tafuta maana mwenyewe... pesa ulizohongwa ndo zinageuka kitanzi kwako make ulikubali kutumika na wajanja wakakupakata miguuni mwao.

Watanzania wakaskazini hawawezi liona hilo ispokuwa wazalendo.
 
Kwa nini zitto na sio kamati yake au chama chake?

Jibu ni moja tu...ni mnafiki na mpenda sifa!

...Ata kusoma hujui?ebu rudia tena kuisoma hiyo habari....

...kwanini Zitto...mashirika hayo yasiyo ya kiserikali ya nchi 19 za Ulaya yalimuona Zitto kuwa ni mtu mwenye sifa stahiki kuongoza jopo la wataalamu hao...



Zitto aliteuliwa mwezi uliopita kuongoza jopo la wataalamu kutoka Eurodad, ambao ni Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo 48 kutoka nchi 19 za Ulaya, ambayo yanajihusisha na masuala ya kufutia madeni nchi zilizoendelea, misaada yenye maana na kodi za haki, kufanya uchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi.

Mashirika hayo yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea.

Uchunguzi huo uliofanywa katika nchi za Ulaya, ulianza Oktoba 20 na ulitarajiwa kukamilika Novemba 5, mwaka huu kwa kuandika ripoti yake.

 
Ngoja tuone labda safari hii kitafika mwisho na kutuwezesha Watanzania kujua siri ya haya mabilioni. Namshangaa lakini kwa nini hakuwashirikisha Viongozi wenzake ndani ya CHADEMA katika kufuatilia hili!? Mtu kama Lissu ni mwanasheria anayeifahamu sheria vizuri sana ingekuwa bomba sana kumshirikisha katika ufuatiliaji wa haya mabilioni yaliyotoroshwa nchini. Mnyika pia ni mtu makini sana sioni naye kwanini hakushirikishwa. Haya mambo ya kutoshirikiana na viongozi wenzako ndani ya chama hayasaidii kabisa katika kuleta mshikamano ndani ya CHADEMA.

Mkuu: hicho anacho kifanya zito ni kuzuga akili za watu na kuwatoa kwenye agenda muhimu watanzania...Kwasasa tunazungumzia mchakato wa Katiba na sheria ya mabadiliko ya Katiba lakini ilikucheza na akili za watu mara tunaambiwa sijui Mawaziri wa kumbwa na kimbunga...mara sijui zito na siri nzito mara sijua azimio la kumuondoa spika...Wakuu tuwe na msimamo hayo yote yasubiri kwanza tunataka tuyaone marekebisho ya sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili tujue kama kile kilichozungumzwa ikulu kimetimiza vinginevyo lazima tuelezane ukweli ...tusikubali kuendeshwa na matukio haya yasiyo kuwa na shingo wala miguu.

Hayo mafedha tukipata uongozi mzuri mwenye kujali maslahi ya Taifa mbona kuyarudisha ni kazi rahisi kama kumsukuma mlevi aliye lewa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Anafanya kazi poa, but usaliti wake na kupenda misifa binafsi kuliko chama ndo ki2 kinafanya wapenda mabadiliko 2nawish ahamie ccm, na cku zito akiondoka cdm au akitimuliwa wapo wana cdm wengi sana 2tatoa sadaka ya shukrani coz weng hu2mwelew wala ha2mkubali
 
Tukishajua tufanyaje sasa? Watanzania hatujui kudai haki zetu. Hata ukiyaambia hayo makampuni yarudishe hizo hela hayarudishi
 
shida haipo kwenye kujua zipo kiasi gani nje, shida kubwa ni hayo makampuni yatarudisha hizo pesa au changa la macho?

zitto asicheze na akili zetu
 
Wana jf, nashangazwa na uchangiaji wa wengi wenu katika habari tajwa hata baadhi yenu kuhoji kwa nini Zitto hajawashirikisha watu fulani fulani katika kuzisaka fedha zilizofichwa nje. Sijui kama mmeisoma hiyo habari yenyewe mpaka mwisho. Zitto amechaguliwa kuongoza jopo la wataalamu kutoka Eurodad, ambao ni mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali yapatao 48 kutoka nchi 19 za ulaya ambayo yanajihusisha na masuala ya kufutia madeni nchi zilizoendelea, misaada yenye maana na kodi za haki, kufanya uchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi. Mashirika hayo yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea. Ndio maana Zitto hachunguzi tu majina ya WaTanzania binafsi, bali pia mashirika na makampuni ya kigeni.
 
Tatizo ni kuwa watu wamesahau umuhimu wa Mh Zitto ktk mageuzi Tanzania,Kabla zitto hajaingia Bungeni Mwaka 2005 chadema kilikuwa na wabunge wachache sana pamoja na kuwa Slaa alikuwepepo tangu mwaka 2000.

Hoja madhubuti za kitaifa zilizoibuliwa na kijana huyu,zilimfanya kuonekana shujaa mbele ya macho ya watanzania,ilipofika mwaka 2010 Zitto tulimtumia kama mtaji kwa chama alitembea nchi nzima kukinadi chama na kwakuwa jamaa alikuwa na mvuto aliweza kuwashawishi vijana wengi kupenda siasa na kuona kuwa kumbe vijana wanaweza,amesababisha kamii yetu kituamini vijana tofauti na zamani ambapo vijana tulionekana wahuni na hivyo hatustahili kuingka Bungeni.

Amewanadi vijana wengi bila hata kinyongo,na inasemekana alitumia muda mwingi kuwanadi wanachadema wenzie na akafanikiwa kuwashawishi vijana kuwaunga mkono vijana wenzao.

Sasa kazi nzuri aliyofanya Zitto imeanza kunajisiwa na vijana wasiojitambua kwa kuanza kuturudisha huko tulikotoka. vitendo vya kihuni vinavyofanywa na baadhi ya wabunge ni kuwaharibia vijana wasiaminiwe tena na jamii kama ilivyokuwa zamani.na haya yanafanyika huenda kwa kutokujua.

Matarajio ya vijana wengi ilikuwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha zitto anafunikwa ili na wao waonekane mashujaa mbele ya macho ya watanzania.sasa wanatumia njia haramu kumpoteza zitto. hawa vijana wamesahau kuwa Zitto nsio chachu ya wao kuaminiwa na mwisho kuchaguliwa na jamii.hawapendi wanapoona Zitto akiendelea kufanya mambo yanayo mpatia umaarufu na kumfanya aendelee kuwa kuwa mwanasiasa bora ambae ni kijana,kiukweli Zitto bado ni kijana lkn namsifu kwa ubunifu wake anapojenga hoja,zitto amekuwa na vyanzo vingi vya taarifa nyeti za kitaifa ikiwemo baadhi ya maafisa wa serikali,Wenzake wanapomuona yuko karibu na nao huzusha kuwa wanamtumia wakati watu hao hawamsaidii zitto peke yake,Slaa amekuwa akipata nyaraka nyingi za siri toka serikalini ,hii ni ktk utaratibu kama wa zitto,vihana wenzake ktk chama na hata viongozi wa juu ktk chama wanamchukia kwakuwa anaonekana mtu muhimu sana kiasi cha kutishia nyadhifa zao ktk chama.

Tumwache zitto awatumikie watanzani kama wengi tunavyoamini,Zitto atafika mbali sana kutokana na kujiwekea malengo makubwa kisiasa,tusimkatishe tamaa kwa kengo la kumvunja nguvu.

Mwisho nawaomba wanachadema mkumbuke na kufuatilia historia ya lema ktk siasa kahama vyama vingapi na nini kilimfanya ahame,kwa kumbukumbu zangu ni kuwa lema alianzia ccm,akakimbilia Nccr mageuzi,kisha akakimbilia TLP na sasa yupo chadema, huyu lema hana tofauti Mlema ambae anatumika kama kibaraka wa ccm.tumtazame Lema kwa jicho la tatu,ni mtu hatari kwa ukombozi wa kweli wa Taifa letu.

nawasilisha.
 
Jamani mbona watu akili zenu zinatapatapa? Kwani zitto huko uraya kajipeleka? Na hili jopo la wataalam kwawatafuta yeye? Taarifa inaonyesha ni jinsi gani taifa linapoteza fedha nyingi ambazo zingepunguza umasikini tanzania, sasa watu ningetegemea wangetoa mawazo ni jinsi gani ya kufanikisha kurudisha fedha hizi sasa walio wengi wanakuwa na chuki zisizo na maana.
 
Hii news conference ni aje!? Watanzania wengi wanaisubiri kwa hamu kubwa sana.
 
Back
Top Bottom