Tanzia: Ben Kiko afariki dunia

Tanzia: Ben Kiko afariki dunia

Jina lake halisi alikuwa no BENJAMIN KIKOTI. Umaarufu wake ulikuwa mkubwa Wakati wa vita yetu na Uganda. Huyo jamaa alikuwa anaripoti akiwa mstari wa mbele. RIP Kikoti

Masahihisho kidogo. Jina lake kamili lilikuwa BENJAMIN KIKOROMA. Nilikutana nae Bukoba wakati wa vita vya Kagera, na alikuwa mstati wa mbele wakati ule akiripoti mambo ya vita, akiwa anaandamana na mpiga picha wetu mashuhuri wa wakati ule marehemu VINCENT URIO.
 
Ben Kiko; Rest in peace our war time broadcasting hero!

Tanzia
Aliekuwa Mtangazaji maarufu wa radio Tanzania (TBC) mzee BEN KIKO amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo 31/10/2014 kwenye hospital ya jeshi mirambo Tabora.

benKiko.jpg

R.I.P BEN

 
Namkumbuka ben kiko enzi hz rtd, ilikuwa rtd kweli,siyo hawa wahuni wa sk hz,ben akisoma habari ya majanga au maafa mwili unakusisimka, waandishi ninaowakumbuka ni situnga steven, jacob tesha paul, karim besta,ahmed kipozi,sala dumba,malima ndelema kipindi chake cha mkoa kwa mkoa,bujaga kizengo kadago,
UMEWASAHAU dominic chilambo ,masoud masoud na sekioni kitojo
 
Jina lake halisi alikuwa no BENJAMIN KIKOTI. Umaarufu wake ulikuwa mkubwa Wakati wa vita yetu na Uganda. Huyo jamaa alikuwa anaripoti akiwa mstari wa mbele. RIP Kikoti

jina lake halisi ni HAMIS KIKOLONZI kikolonzi ni ubin wake sasa alikuwa anajiita ubini wake BEN KIKO alikuwa mrefu mtu wa huko tabora alipo kuwa dodoma alikuwa mcheshi kwa kila mtu polen watani zangu wa Tabora

Hapana alikuwa anaitwa Bernard Kikoloma.alale pema.


anaitwa Ben Hamis Kikoromo na sio hivo ulivomuita

Huu mkanganyiko wa jina la marehemu utatatulika vipi..?

RIP Ben Kiko..
Binafsi ninakikumbuka kisa kimoja alichokiripoti kupitia kipindi cha Majira kuhusu Mchunga ng'ombe kipofu aliemuua mtoto kwa kumpiga fimbo akidhani ni ng'ombe huko Dodoma..
 
nitamkumbuka sana alivyokuwa ana report vita ya uganda.
My condolence
r.i.p
benedict kikoti.
 
RIP Jembe Ben Kiko...

Nyie ndio mlikuwa watangazaji wa ukweli, sio hawa wakata viuno akina Gerald Hando...
 
Mnaikumbuka kesi ya Kaizerege, jamaa alikuwa anaripoti hiyo kesi miaka hiyooo
 
R.I.P. Ben Kiko. Hatutakusahau jinsi ulivyokuwa unatuhabarisha kuhusu vita vya Kagera.
 
Dah Mzee alikuwa hakosi "report" kipindi cha Majira na Harakati, mzee wa kupamba na kuyavuta maneno!

Lala Salama Ben Kiko
 
Mtangazaji wa zamani wa iliyokuwa Radio Tanzania,Benn Kiko amefariki dunia saa 8 za usiku katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Benn Kiko aliwahi kutangaza vita ya kagera.

CHANZO:TBC 1
 
Dah....Jamani Baba Yangu Akisikia atasikitika Sana kwani wakati tukikua miaka ya 96 kila usiku wa saa tatu tulikuwa tukiwasha radio tanzania maswafya ya short wave 1225/6 kusikiliza kipindi cha majira na mzee alikuwa akimpenda sana ben kiko, martha ngwila, richard leo n.k.

Mungu Amlaze Mahali Pema Peponi Amina.
 
Back
Top Bottom