Wakati mwingine ubora au kinachoitwa udhaifu wa mwandishi husababishwa na mtazamo wa msomaji.Kwa mfano Shaniki wa Yanga ni mara chache sana kuona makala inayoisifia Simba haina makosa...Hivyo hivyo kwa mwanachama wa ccm anayesoma makala inayohusu Chadema
Wiki iliyopita mmoja wa manguli wa siasa za upinzani Zanzibar ,na aliyekua katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharifu Hamad alihamia chama cha Act wazalendo .
Maalim Seif alihamia chama hiko baada ya mahakama kumpa ushindi hasimu wake Prof Ibrahimu Haruna Lipumba na kuhitimisha...
Ni mwezi huu klabu ya Simba imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika,timu ya taifa imekata tiketi ya kushiriki mashindano ya mataifa ya Afrika na bondia mtanzania Hassan Mwakinyo amemdunda bondia Sergio Eduardo Gonzalez nchini Kenya kwa Knockout(KO) round ya...
KIFO CHA RUGE MUTAHABA KITUFUNDISHE KUJITAFUTA.
Mimi ni mmoja kati ya mamilioni ya watanzania waliofatilia kwa ukaribu sana mazishi ya aliyekua mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliyefariki February 26,2019.
Katika siku tano nilizofatilia mazishi yake...
KWA NINI TUSIWE NA AINA YETU YA DEMOKRASIA?
Tafsiri ya demokrasia kama ilivyotolewa na Abraham Lincoln kuwa ni utawala wa watu kwa ajili ya watu inaukakasi hasa kama watu wengi ni wajinga basi ni kuruhusu wajinga kuchaguana.
Lakini demokrasia ikitafsiriwa kama uwepo wa uhuru wa watu ,haki za...
"THE LAW OF SUBSTITUTION "
Vyura sita walikua wanatembea kwa kuruka ruka kwenye gogo kubwa lililowekwa juu ya shimo lilichimbwa na binadamu.Bahati mbaya vyura wawili wakatumbukia kwenye shimo hilo refu lililoandaliwa kwa ajili ya kutengenezea choo.
Vyura wa nne waliobaki wakasikitika sana na...
UKIWA HUNA MAONO YA KISIASA UTABEZA HATA VIONGOZI WA DINI
Chama cha siasa ni muungano wa watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi flani au zao binafsi.
Ili kufikia lengo hilo la...
MWAMBIENI MWINYI ZAHERA,KUFUNGWA KWA YANGA HAKUJATOKANA NA UCHOVU.
Nimemsikia kocha wa Yanga Mkongomani Mwinyi Zahera akizungumza na waandishi wahabari 22 Januari ,2019 baada ya timu yake kufungwa magoli 3-2 na timu ya Kariobang Shork toka nchini Kenya kwenye mashindano yanayoendelea...
MAHOJIANO YA TUNDU LISSU BBC DHIDI YA DHANA KUHUSU UKWELI
Januari 21 mwaka huu ,Mbunge wa Singida mashariki alihojiwa katika kipindi maarufu kinachorushwa na Shirika la habari la Uingereza BBC idhaa ya Kiingerezwa cha Hard Talk.
Katika mahojiano hayo mbunge huyo aliyepigwa risasi September...
IPO WAPI ILE BONGO FLEVA?
Mpaka sasa mjadala mkali unaendelea kuhusu nani hasa aliyeupa jina la "bongo fleva"muziki wa kizazi kipya.Wengine wanamtaja mtangazaji mkongwe wa radio, Mike Mhagama kama mhasisi wa jina hili miaka ya tisini alipolitaja kwa mara ya kwanza.
Lakini pia,lipo kundi...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.