Zitto Kabwe anavyoteseka na kivuli cha Tundu Lissu

njundelekajo

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
310
Reaction score
228
KIVULI CHA TUNDU ANTIPASY LISSU KINAVYOMTESA ZITTO ZUBERY KABWE.

Wakati ule umri wake ukiwa hautoshi kikatiba kugombea urais Zitto alifanya siasa za kiungwana sana akijaribu kujenga hoja na ushawishi wa aina mbalimbali ndani na nje ya bunge.

Bahati mbaya sana umri wake ulipotosha amekuta soko la siasa za upinzani bidhaa inayouzwa sana katika nafasi ya mgombea wa kiti cha urais ni Tundu Lissu.

Bahati ya mtende aliyoipata Zitto,Tundu Lissu hayupo Tanzania.Kwa mazingira hayo amepata fursa ya kujitengeneza ili ili kulishinda bidhaa inayoitwa Lissu kwenye siasa za upinzani.

Na kwakua kilichomuweka juu Lissu ni siasa zake za kiharakati kumemlazimu Zitto abadili aina ya siasa zake .

Zitto wa sasa ni wa kushinda mahakamani kama Lissu,Kabwe wa sasa haamini tena kwenye hoja kuliko utunzi wa matukio yatakampa umaarufu wa huruma.

Wakati flani mwaka 2016 Tundu Lissu alijibanza kwenye viunga vya mahakama ya Dodoma kudai kwamba kuna njama za kutaka kumkamata.Mwaka 2017 Zitto akajibu mbinu hiyo kujificha kudai anasakwa.Unasakwa alafu unaongea na vyombo vya habari hukamatwi?

KunaMwanaharakati wakati natamani kumuingiza Zitto wa wakati huu kwenye kundi la wanaharakati.Lakini nipaorejea tafsiri ya mwanaharakati ni nani na harakati ni nini tasfiri ninayoipata inapwaya kwa Zitto.

Kada na mwanachama wa siku nyingi wa Chadema Yericko Nyerere katika moja ya maandiko yake amepata kuandika kuwa, Mwanaharakati hunyooka kama kamba.

Akaendelea kuwa ,mwanasiasa hutembea katika fursa za kisiasa.Mwanasiasa si muumini wa uzalendo ni adui wa uzalendo.

Zitto Zuberi Kabwe hatoshi kwenye hata moja kati ya zote zilizotajwa na Yericko Nyerere kati ya mwanasiasa na mwanaharakati.Vijana wangesema hayupo duniani wala mbinguni.

Mwanafalsafa wa kiajemi Murtadha Mutahhari anasema harakati huanzishwa na wanyongea kielezea nadharia hii katika mojawapo ya matoleo yake anasema, harakati zisizojikita kwenye mahusiani na jamii zimekosa sifa ya kuitwa harakati.

Hivyo hivyo, katika harakati mwishowe hubainika wazi kuwa hufanywa na kundi la wanyonge wenye hisia ya kukosa haki, kudhulumiwa na kukandamizwa dhidi ya tabaka la juu hata kama hapo awali taswira hiyo itakuwa haikujitokeza au kugundulika .

Kuna nadharia nyingi juu ya sababu zinazoweza kupelekea kuzuka kwa harakati za kudai haki. Kuna uwezekano pia harakati zikawa na hisia za kibinadamu endapo zina msingi wa kupigania uhuru na msingi wa siasa, wala siyo zikiwa zina msingi wa uchumi pekee. Kwani inawezekana kuondoa njaa kwa kadri kubwa, lakini wakati huo huo watu wakawa hawana uhuru wa kuabudu, kuhubiri dini zao, uhuru wa kusema, uhuru wa kukosoa na uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Katika mtazamo huu wa Murtadha Mutahhari, Zitto hafanyi harakati wakati huohuo hafanyi siasa.Kadri afya ya Tundu Lissu inavyoimarika na kuonesha dalili ya kurejea Tanzania ndivyo Zitto anavyozidi kuibua matukio ya kulazimisha azungumzwe na kubaki kwenye kurasa za mbele za magazeti.

Tafuta lini Zitto alikamatwa na polisi na mara ngapi katika kipindi chote umri wake hauku tosha kugombea urais linganisha na anavyokamatwa kamatwa wakati huu .

Zitto yule asiyekua anawaza urais alikua mjenzi hasa wa hoja kwa nini akamatwe?Huyu wa sasa ameonekana kutaka kufanana na Tundu Lissu

Alikamtwa Oktoba 31 2017 kwa kutamka maneno ya uchochezi kwenye kampeni,akakamatwa tena Jumatano Oktoba 31 2018 kwa kusema zaidi ya watu 100 wameuawawa mkoani Kigoma kabla yaFebruary 18,2018 mkoani Morogoro,kukamatwa tena kwa kukusanyika bila kibali mkoani Morogoro

Zitto wa Buzwagi sio huyu wa "anayetishiwa kuuwawa" Zitto yule mwenyekiti wa PAC sio huyu anayeshinda mahakamani siku hizi.Huyu wasasa kiu yake ya kutaka kugombea urais mwaka 2020 imempofua macho na staha yake ya kisiasa aliyoijenga miaka kenda.

Mbunge huyo wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT wazalendo hivi karibuni amenukuliwa akisema ana mashaka na uhuru wa mahakama.

Ametoa kauli hiyo baada ya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kukwama kwa mashauri aliyowasilisha mahakama kuu.

Ikumbukwe tarehe 16 January,2019 mahakama kuu ilikataa kupokea kesi ya kikatiba na mbunge huyo kuhoji uhalali wa spika wa bunge ,Job Ndugai kumuita kwenye kamati ya bunge mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Prof Musa Assad.

Uamuzi huo wa mahakama ni wa pili ndani ya kipindi kifupi baada ya ule wa kwanza ambao zito na wenzake waliitaka mahakama kuzuia bunge kujadili muswada wa vyama vya siasa.

JE KATIKA UONGOZI WA MAGUFULI WAPINZANI HAWAJAWAHI KUSHINDA KESI MAHAKAMANI?

KILIMANJARO -Chadema mwaka 2017 (Magufuli akiwa na miaka 2 madarakani) ilishinda kesi mahakama ya kuu kanda ya Moshi.

Rufaa hiyo namba 52 ya mwaka 2017 ambayo jamhuri iliwakilishwa na na wakili Damas Kyauke.

MANYARA -Mwaka 2015 mahakama ilitengua matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji 16 wa mdogo wa Mererani .

Katika kesi hiyo Chadema walishinda pamoja na matokeo ya ya uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji cha Lobosireti wilayani Kiteto.

DAR-ES-SALAM-Abdalah Mtolea wa CUF alitangazwa mshindi na mahakama kuu kanda ya Dar-es-Salaam.Mtolea alishinda rufaa hiyo dhidi ya aliyekua mbunge wa jimbo hilo Abas Mtemvu wa CCM.

Aidha,Machi 30,2017 Mahakama kuu kanda ya Dar-es-Salaam ilimuachia huru Mbunge wa Kilombero kupitia Chadema Peter Lijua Likali.

Mbunge huyo aliyekua akitetewa na wakili Tundu Lissu ambaye pia ni kiongozi na mbunge wa Chadema alichiwa huru baada ya mahakama hiyo kukubalina na rufaa yake.

Wakati Tundu Lissu na Lijua likali wanashinda kesi hiyo ambayo jamhuri iliwakilishwa na wakili Faraja Nchimbi .

Kesi zote mbili zilizowapa upinzani ushindi Tanzania ilikua chini ya Chama cha Mapinduzi na rais ni Dr John Pombe Magufuli.Mahakama hakuonekana kuingiliwa?

MWANZA- Mwaka 2016 jaji Lameck Mlacha wa mahakama kuu kanda ya ziwa alifuta amri ya jeshi la polisi na kutoa ruhusa kwa familia ya marehemu Alfonce Mawazo kuendelea na shughuli za maziko.

Alfonce Mawazo alikua mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita.Katika shauri hilo namba 11 la mwaka 2015 Chadema iliibwaga jeshi la polisi katika serikali hii Magufuli akiwa na mwaka mmoja madarakani.Mahakama hakuinekana kuingiliwa?

MOROGORO- Mwaka 2016 Wabunge Suzani Kiwanga na Peter na Lijua likali walishinda kesi ya kupinga ubunge wao iliyofunguliwa na Aboubakar Assenga na wanzake.Mahakama hakuonekana kuingiliwa?

MBEYA-Agost 10,2018 Kesi namba 117 ya mwaka 2017 .Mbunge wa Mbozi kupitia Chadema ,Pascal Haonga na wanzake wawili walishinda kesi.Mahakama haikuonekana kuingiliwa?

Mbunge huyo wa Chadema na katibu wake Wilfred Mwalusanya walishtakiwa kwa kufanya makosa matatu likiwemo kuwazuia polisi kutumiza majukumu yao.Mahakama haikuonekana kuingiliwa?

KIGOMA-Agost, 2017.Aliyekua mbunge wa jimbo la Kakonko kupitia Chadema , marehemu Bilago Kasuku alishinda kesi ya kupinga ubunge wake iliyofunguliwa na Christopher Chiza wa CCM.

Hukumu hiyo iliyotolewa mapema August 2017 iliitimisha rasm ubunge wa Chiza wa CCM.Mahakama haikutiliwa mashaka na Zitto?

Kwa orodha hiyo fupi ya ushindi wa vyama vya upinzani dhidi ya serikali ama watu wa chama cha mapinduzi ni wazi kauli ya Zitto inathibitisha anavyosumbuliwa na"sisira" la Lissu.

Ndio maana kauli hii imetolewa baada ya Tundu Lissu kusema anarudi Tanzania na atagombea urais kupitia umoja wa vyama vya upinzani.

KWA NINI ZITTO WA SASA SI YULE WA NYAKATI ZILE?

Pasi na shaka hata chembe ndani ya vyama vyoye vya upinzani anayemkaribia Tundu Lissu kwa umaarufu kwa sasa hayupo.

Zitto amegundua hili ni kikwazo katika nia yake ya kugombea Urals na sasa anatengeneza uzito wa kukaribiana na Lissu.

Anafahamu mbinu ziliyomfikisha Tundu Lissu katika umaarufu wa alionao sasa ni pamoja na kuanzisha migogoro na mahakama polisi,taasisi ,na idara nyingine za serikali.

Haishangazi sana kuona Lissu mpaka sasa amekamatwa na polisi zaidi ya mara 8.

Mwishoni mwa mwaka jana kuthibitisha anavyouwaza utais Zitto,alibuni kauli mbiu ya "KAZI NA BATA" kama moja ya namna atakavyoingoza serikali yake.

Baadae "akajistukia" kwa kunetroulize asionekane amakamia sana kugombea,post inayofuata akawataja Tundu Lissu,Benard Membe,Lowassa kwamba kama nafasi ya kugombea itadondokea kwao wakumbuke. "KAZI NA BATA"

JE AINA HII YA SIASA ZA ZITTO ZITAMSAIDIA?

Ingawa kipindi cha nyuma siasa yake ya kutojihusisha na virugu hasa kwa kutoshiriki operesheni kadhaa za Chadema kama Operesheni Sangara,M4C na nyinginezo kulichangia aonekane msaliti,lakini ilimtofutisha sana na wanasiasa wengi wa upinzani.

Siasa ya kiungwana ya Zitto ndio hasa iliyojenga jina la sasa la Zitto.Ni siasa hiyo iliyomfanya abaki bungeni mwishoni mwa mwaka 2011 wakati wabunge wa upinzani walipotoka bungeni kwa mara ya kwanza ishara ya kutomtambua rais Kikwete.

Ni siasa ile ya ujenzi wa hoja iliyomfanya arudi bungeni kupitia chama kichanga cha ACT wazalendo akiwa mbunge pekee wa Madam chama hiko.Nje ya siasa ile simuoni Zitto wa kesho.

Amechelewa mno katika aina hii ya siasa aliyoichagua sasa.Itamfanya si tu asieleweke lakini kumpotezea wafuasi wengi waliomini katika siasa zake za hoja na kuibua mijadala yenye sura ya kitaifa.

Chadema sio wageni na tabia za Zitto anapolitaka jambo lake liwe.Wanmkumbuka alipoutaka uenyekiti wa chama hiko kabla ya kumfukuza.

Nguzo Noel.R.
20/1/2019
 
Mawazo yako tu.Una haki ya kucharaza hata kurasa mia nne kumchambua mtu utadhani weye ni mama yake au mke wake.Merde!
 
Binafsi nimekuelewa kwa nilivyokuelewa mkuu
 
Umesahau kuweka namba ya simu.

Kwa taarifa yako Zitto yuko sawa tena alichelewa sana kufanya anayoyafanya sasa. Kwa kugundua kutokufanya wajibu wake kama mpinzani, sasa ni kama anarekebisha makosa yake. Kama anataka urais hilo sio kosa, na wala hafanyi haya kushindana na Lissu, kwani kila mtu ana chama chake, hivyo kila mmoja anaweza kupata tiketi ya kugombea urais kupitia chama chake.
 
Zito anamshinda cv ,lisu. Kwenye kazi na matokeo yaliyotokea bungeni.Lisu yeye mahakamani hana mpinzani hakuna japo lisu bungeni amewahi kuliibua na kushinda japo ni machachari.
 
Back
Top Bottom