Ipo wapi ile bongofleva?

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
IPO WAPI ILE BONGO FLEVA?

Mpaka sasa mjadala mkali unaendelea kuhusu nani hasa aliyeupa jina la "bongo fleva"muziki wa kizazi kipya.Wengine wanamtaja mtangazaji mkongwe wa radio, Mike Mhagama kama mhasisi wa jina hili miaka ya tisini alipolitaja kwa mara ya kwanza.

Lakini pia,lipo kundi lingine wanamtaja Mkongwe mwingine, Taji Liundi(Master T) kama muasisi wa jina hili la muziki huu ulioanzia miaka ya 1990,huku baadhi wakiwataja kina Joseph Kusaga Boniface Kilosa( Dj Boni Love).Hakuna ushahidi nani aliyetamka kwa mara ya kwanza neno "bongo fleva"kuwakilisha muziki huu mpaka sasa.

Lililo wazi katika historia ya muziki huu huwezi kuyakwepa majina ya wasanii kadhaa kama Adili au Nigga One,Salehe Jabri aliyetumia mdundo wa wimbo wa "Vanila Ice,Ice,"Ice Ice Baby",kisha kughani kwa lugha ya Kiswahili.

Au ,kinaOtham Njaidi,Eliud Pemba,Columba Mwingira,Sindila Assey,Joseph Mbilinyi(2 proud wakati huo),Sygon,Pamela kama baadhi ya waasisi na waanzilishi wa muziki huo.

Muziki huo ulioshika hatamu miaka ya 2000 ukichagizwa na album bora ya wakati wote ya kundi la H.Blasters likiundwa na wasanii Nigga J(sasa hivi Prof J),Fanani na Big Willy.

Album hoyo inayoaminika kuleta mapinduzi makubwa ya kimtazamo kwa jamii kutokana na vibao vyake vikali ikiwemo Ma Msapu,Niamini,Bongo Dar-es-Salaam iliyobeba jina la album,hauonekani tena kujifinyanga na jamii ya kitanzania kama kipindi cha nyuma.

Wakati ule wa uhai wa bongo fleva katika jamii ya watanzania hakukua na fungiafungia ya nyimbo za wasanii wa muziki huu toka BASATA kama ilivyo sasa.Ilizoeleka kusikia Baraza hilo la sanaa nchini likipambana na wasanii wa filamu.

Ungewezaje kufungia wimbo kama "wauguzi" wa Wagosi wa kaya?au "mama mubaya"wa Mataluma na pengine "Malumbano" wa Twenty percent a.k.a Twenty Paaa a.k.a Amilalile?na ukaeleweka.

Bundi wa mashairi ya nyimbo za bongofleva kujitenga na masuala kuntu ya jamii alitua rasmi juu la paa la muziki huu baada ya kuingia kwa "watu wa kati"maarufu kama meneja wa msanii.

Hawa wameivuruga kama sio kuiondoa kabisa taswira kubw iliyobebwa muziki huo miaka ya nyuma kati ya muziki huo na jamii ya watanzania kutokana na kuufanya muziki huo kua na malengo ya kibiashara zadi kuliko maadili na ujumbe wenye kuikanya jamii ama kuipa tahadhari katika mambo mbali mbali yakiwemo magonjwa kama ukimwi,matumizi ya madawa ya kulevya nk.

Hebu fumba macho yako rudisha nyuma masikio yako zikumbuke nyimbo hizi:- Mshkaji mmoja(Jose line),Kama ntapata Ukimwi(Afande Sele),Majobless(BIG DOG POZ),Ana miaka chini ya 18(2 proud), Maisha ya Boarding(Jay Moe).

Usifumbie bado endelea na :-Machoni kama watu(Lady Jay Dee ft A.Y),Mke wa mtu ni sumu(LWP),Tutakukumbuka (Crazy Gk ft T.ID,)Alikufa kwa ngoma (Mwana Fa),Kazi yake Mola(Madee),Kamanda(Daz Nundaz),Kosa la Marehemu(Uswahilini Matola),Mwanangu huna nidhamu(Dudu Baya),Ntoke vipi(Bwana misosi),Nipende kama nilivyo(Chelea man)

Fumbua macho vuta pumzi kwa nguvu ndani,washa redio yako sikiliza nyimbo hizi Nampa Papa(Gigi Money),Hakunaga Ushemeji (Manifongo),Kibamia(Rostam),Nyegezi (Diamond ft Rayvan),Ntakupwelepweta(Ya Moto Band),Kijuso(Queen Darlin).

Umegundua nini? jibu ulilolipata ndio sababu iliyofanya tusisikie wimbo wa msanii wa bongo fleva wa kizazi cha sasa hata mmoja ukipigwa wakati rais alipotangaza siku nne za maombelezo kutokana na kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere ziwa Victoria tarehe Septemba 20 mwaka jana.

Nyimbo zote zilikuwa zinapigwa redion katika siku nne za maombolezo ni za wasanii wa bingofleva kundi la kwanza .Wasanii wa kipindi wapo mbali na jamii yao.

Wasanii wa sasa wamejitengenezea dunia yao peke yao ambayo haina kifo ndo mana hawatungi nyimbo kuhusu vifo, haina njaa wala ukimwi ndo mana hawaoni umuhimu wa kutunga wimbo kama usinitenge ya Profesa Jay,kwa nini waimbe madawa ya kulevya mabaya kwenye dunia yao ya vibamia?Ukikuta wimbo wenye muktadha wa kijamii au taifa basi ni"project"maalum

Wapo kilometa nyingi sana toka jamii yao ilipo, wamemezeshwa maneno na mameneja wao kwamba nyimbo za mapenzi peke yake ndizo zinazolipa na kutamba.

Huu hutumwa wa pesa kwa nini mnaifanya kuisaliti familia zenu zinazotaka muwakumbushe wenzenu juu ya ukimwi?Kama kila biashara yoyote inayolipa ni sahihi kuifanya kwa nini biashara ya madawa ya kulevya inakatazwa?Kuna tofauti gani kati ya mfanyabiashara wa madawa ya kulevya na msanii anayepanda mambo ya hovyo katika vichwa vya jamii yake?

Uasi mkubwa uliofanywa na mameneja katika mziki huu ni kuubadlisha mfumo wake kutoka kwenye kuuza albamu na kua muziki unaotegemea biashara ya matamasha.Na hili halikufanyika bahati mbaya.

Mauzo ya albam yalikua hayana faida kwa meneja zaidi ya msanii mwenyewe na msambazaji.Badiliko hili likaondoa focus ya wasanii kutunga nyimbo wakiiwaza jamii yao na badala yake wanatunga nyimbo za kuwafurahisha watakaokuja ukumbini,wanyanyue mikono juu,watingishe kama imekwisha na mambo mengine ya pale kati patamu tamu.

Ukumbini haiwezekani ukaeleweka kama utawaimbia watu"Nikianguka" wa Afande Sele,nani atake umuimbie Swahiba wa marehemu Jebi badala ya Kababa ye na wowowo?.

Hii ni sababu ya wasanii karma, Nash Mc,Songa na wengine kama kina Nick Mbishi hawawezi kua na mameneja kwa utaratibu wao wa kuendelea kufanya biashara ya muziki kwa kuuza albam.

Meneja gani hakuruhusu utunge wimbo kama barua wa Das Nundaz wakati kuna wimbo wa "katika",uandike mashairi yenye verse nne kama wimbo wa simu yangu wa Solo Thang mbele ya Konk yenye verse moja na nusu wa Dudu Baya? .

Ni kweli mambo yanabadilika sawa lakini ni bora kusiwe na mabadiliko kama mabadiliko hayo hayana tija kwa jamii.Tunatambua kam muziki huu umetoa ajira kubwa sana kwa vijana wengi pasipo kutengeneza heshma ajira hizo hazitakua na maana yoyote.

Nguzo Noel.R.
 
Mkuu umechambua vizuri sana,hadi roho imeniuma,ni kweli kwa sasa wapenzi wa muziki wa bongo fleva ambao tumekula chumvi kidogo tumebakiwa mayatima,zile burudani hazipo tena..mabepari wa muziki wamekuja kuusambaratisha utamaduni wetu:confused::confused:
 
Mimi ninazo nyingi sana,maana tangu radio za FM ziingie mjini,na huu muziki ukafa,nikaacha kuzisikiliza...so wajanja tulishajiandalia maktaba zetu...maana huu uzi bila kusindikizwa na hizi burudani itakuwa kazi bure...mwingine kama nae anazo tushee hapa...
 
Attachments

  • A_Y_ft_Mwana_FA-Nangoja_ageuke.mp3
    6.8 MB · Views: 21
  • Afande_Sele-Kwa_vyovyote.mp3
    4.4 MB · Views: 20
  • life ya uswazi-gangwe mob.mp3
    1.6 MB · Views: 24
  • Mb dog - Ina maana.mp3
    3.5 MB · Views: 23
  • Oten - SIFA KUMI ZA DEMU.mp3
    3.6 MB · Views: 24
  • Manzese Crew - Maisha Ubishi.mp3
    4.1 MB · Views: 27
  • Niaje MANDOJO & DOMOKAYA feat J.NATURE.mp3
    3.3 MB · Views: 19
  • Pig Black -Nini Mnataka.mp3
    2.5 MB · Views: 24
  • Park lane - Nafasi nyingine.mp3
    4.5 MB · Views: 25
  • SGF -Mechi kali.mp3
    9.5 MB · Views: 23
  • Waswahili -Yupi bora.mp3
    4 MB · Views: 24
  • Rama_Dee_feat_Mapacha_Kuwa_Na_Subira.mp3
    4 MB · Views: 24
  • TAMARA-HARD MAD.mp3
    11.3 MB · Views: 22
  • tid - zeze.mp3
    3.8 MB · Views: 24
  • Wachuja nafaka - Yaleo kali.mp3
    5.1 MB · Views: 22
Mimi ninazo nyingi sana,maana tangu radio za FM ziingie mjini,na huu muziki ukafa,nikaacha kuzisikiliza...so wajanja tulishajiandalia maktaba zetu...maana huu uzi bila kusindikizwa na hizi burudani itakuwa kazi bure...mwingine kama nae anazo tushee hapa...
Ahsante mkuu.
 
Ongezea mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IPO WAPI ILE BONGO FLEVA ?

Mpaka sasa mjadala mkali unaendelea kuhusu nani hasa aliyeupa jina la "bongo fleva"muziki wa kizazi kipya.Wengine wanamtaja mtangazaji mkongwe wa radio, Mike Mhagama kama mhasisi wa jina hili miaka ya tisini alipolitaja kwa mara ya kwanza.

Lakini pia,lipo kundi lingine wanamtaja Mkongwe mwingine, Taji Liundi(Master T) kama muasisi wa jina hili la muziki huu ulioanzia miaka ya 1990,huku baadhi wakiwataja kina Joseph Kusaga Boniface Kilosa( Dj Boni Love).Hakuna ushahidi nani aliyetamka kwa mara ya kwanza neno "bongo fleva"kuwakilisha muziki huu mpaka sasa.

Lililo wazi katika historia ya muziki huu huwezi kuyakwepa majina ya wasanii kadhaa kama Adili au Nigga One,Salehe Jabri aliyetumia mdundo wa wimbo wa "Vanila Ice,Ice,"Ice Ice Baby",kisha kughani kwa lugha ya Kiswahili.

Au ,kinaOtham Njaidi,Eliud Pemba,Columba Mwingira,Sindila Assey,Joseph Mbilinyi(2 proud wakati huo),Sygon,Pamela kama baadhi ya waasisi na waanzilishi wa muziki huo.

Muziki huo ulioshika hatamu miaka ya 2000 ukichagizwa na album bora ya wakati wote ya kundi la H.Blasters likiundwa na wasanii Nigga J(sasa hivi Prof J),Fanani na Big Willy.

Album hoyo inayoaminika kuleta mapinduzi makubwa ya kimtazamo kwa jamii kutokana na vibao vyake vikali ikiwemo Ma Msapu,Niamini,Bongo Dar-es-Salaam iliyobeba jina la album,hauonekani tena kujifinyanga na jamii ya kitanzania kama kipindi cha nyuma.

Wakati ule wa uhai wa bongo fleva katika jamii ya watanzania hakukua na fungiafungia ya nyimbo za wasanii wa muziki huu toka BASATA kama ilivyo sasa.Ilizoeleka kusikia Baraza hilo la sanaa nchini likipambana na wasanii wa filamu.

Ungewezaje kufungia wimbo kama "wauguzi" wa Wagosi wa kaya?au "mama mubaya"wa Mataluma na pengine "Malumbano" wa Twenty percent a.k.a Twenty Paaa a.k.a Amilalile?na ukaeleweka.

Bundi wa mashairi ya nyimbo za bongofleva kujitenga na masuala kuntu ya jamii alitua rasmi juu la paa la muziki huu baada ya kuingia kwa "watu wa kati"maarufu kama meneja wa msanii.

Hawa wameivuruga kama sio kuiondoa kabisa taswira kubw iliyobebwa muziki huo miaka ya nyuma kati ya muziki huo na jamii ya watanzania kutokana na kuufanya muziki huo kua na malengo ya kibiashara zadi kuliko maadili na ujumbe wenye kuikanya jamii ama kuipa tahadhari katika mambo mbali mbali yakiwemo magonjwa kama ukimwi,matumizi ya madawa ya kulevya nk.

Hebu fumba macho yako rudisha nyuma masikio yako zikumbuke nyimbo hizi:- Mshkaji mmoja(Jose line),Kama ntapata Ukimwi(Afande Sele),Majobless(BIG DOG POZ),Ana miaka chini ya 18(2 proud), Maisha ya Boarding(Jay Moe).

Usifumbie bado endelea na :-Machoni kama watu(Lady Jay Dee ft A.Y),Mke wa mtu ni sumu(LWP),Tutakukumbuka (Crazy Gk ft T.ID,)Alikufa kwa ngoma (Mwana Fa),Kazi yake Mola(Madee),Kamanda(Daz Nundaz),Kosa la Marehemu(Uswahilini Matola),Mwanangu huna nidhamu(Dudu Baya),Ntoke vipi(Bwana misosi),Nipende kama nilivyo(Chelea man)

Fumbua macho vuta pumzi kwa nguvu ndani,washa redio yako sikiliza nyimbo hizi Nampa Papa(Gigi Money),Hakunaga Ushemeji (Manifongo),Kibamia(Rostam),Nyegezi (Diamond ft Rayvan),Ntakupwelepweta(Ya Moto Band),Kijuso(Queen Darlin).

Umegundua nini? jibu ulilolipata ndio sababu iliyofanya tusisikie wimbo wa msanii wa bongo fleva wa kizazi cha sasa hata mmoja ukipigwa wakati rais alipotangaza siku nne za maombelezo kutokana na kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere ziwa Victoria tarehe Septemba 20 mwaka jana.

Nyimbo zote zilikuwa zinapigwa redion katika siku nne za maombolezo ni za wasanii wa bingofleva kundi la kwanza .Wasanii wa kipindi wapo mbali na jamii yao.

Wasanii wa sasa wamejitengenezea dunia yao peke yao ambayo haina kifo ndo mana hawatungi nyimbo kuhusu vifo, haina njaa wala ukimwi ndo mana hawaoni umuhimu wa kutunga wimbo kama usinitenge ya Profesa Jay,kwa nini waimbe madawa ya kulevya mabaya kwenye dunia yao ya vibamia?Ukikuta wimbo wenye muktadha wa kijamii au taifa basi ni"project"maalum

Wapo kilometa nyingi sana toka jamii yao ilipo, wamemezeshwa maneno na mameneja wao kwamba nyimbo za mapenzi peke yake ndizo zinazolipa na kutamba.

Huu hutumwa wa pesa kwa nini mnaifanya kuisaliti familia zenu zinazotaka muwakumbushe wenzenu juu ya ukimwi?Kama kila biashara yoyote inayolipa ni sahihi kuifanya kwa nini biashara ya madawa ya kulevya inakatazwa?Kuna tofauti gani kati ya mfanyabiashara wa madawa ya kulevya na msanii anayepanda mambo ya hovyo katika vichwa vya jamii yake?

Uasi mkubwa uliofanywa na mameneja katika mziki huu ni kuubadlisha mfumo wake kutoka kwenye kuuza albamu na kua muziki unaotegemea biashara ya matamasha.Na hili halikufanyika bahati mbaya.

Mauzo ya albam yalikua hayana faida kwa meneja zaidi ya msanii mwenyewe na msambazaji.Badiliko hili likaondoa focus ya wasanii kutunga nyimbo wakiiwaza jamii yao na badala yake wanatunga nyimbo za kuwafurahisha watakaokuja ukumbini,wanyanyue mikono juu,watingishe kama imekwisha na mambo mengine ya pale kati patamu tamu.

Ukumbini haiwezekani ukaeleweka kama utawaimbia watu"Nikianguka" wa Afande Sele,nani atake umuimbie Swahiba wa marehemu Jebi badala ya Kababa ye na wowowo?.

Hii ni sababu ya wasanii karma, Nash Mc,Songa na wengine kama kina Nick Mbishi hawawezi kua na mameneja kwa utaratibu wao wa kuendelea kufanya biashara ya muziki kwa kuuza albam.

Meneja gani hakuruhusu utunge wimbo kama barua wa Das Nundaz wakati kuna wimbo wa "katika",uandike mashairi yenye verse nne kama wimbo wa simu yangu wa Solo Thang mbele ya Konk yenye verse moja na nusu wa Dudu Baya? .

Ni kweli mambo yanabadilika sawa lakini ni bora kusiwe na mabadiliko kama mabadiliko hayo hayana tija kwa jamii.Tunatambua kam muziki huu umetoa ajira kubwa sana kwa vijana wengi pasipo kutengeneza heshma ajira hizo hazitakua na maana yoyote.

Nguzo Noel.R.
Mkuu,umetisha hii makala,inabidi iwekwe kwenye kitabu kabisa,ichapishwe tufanye lamination,itakuwa rejea mwanana sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ninazo nyingi sana,maana tangu radio za FM ziingie mjini,na huu muziki ukafa,nikaacha kuzisikiliza...so wajanja tulishajiandalia maktaba zetu...maana huu uzi bila kusindikizwa na hizi burudani itakuwa kazi bure...mwingine kama nae anazo tushee hapa...
Kaka,umetisha,hizi ndio zilikuwa zetu,enzi hizo 2000,
Kipindi hicho,ikitoka mtoto wa geti Kali,unasikia bongo DSM,Mara Mimi na mabinti damdam!!acha kabisa,
Sio siku hizi,utasikia msambwanda,Mara ikikutana yako na yangu,shida tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hongera kwa makala mahiri na fikirishi.
Imenikumbusha nyuma, kipindi hicho msamiati "Msanii Kioo cha Jamii" uliibuliwa kutokana na matendo ya wasanii wakati huo yaligusa/kuakisi moja kwa moja maisha ya kila siku ya jamii.

Siku hizi msamiati huo umekufa kimya kimya kutokana matendo ya wasanii wa sasa.
 
Mkuu umewaza mbali sana. Niwashukuru sana WASAFI FM hakika leo Mchana wamegonga ngoma zoooooooote unazozijua wewe za Bongo Fleva ya wakati huo. Nitavizia tena Jpili nione kama zitagongwa.
 
Ka DJ Lucky ndiyo ka moto kwenye hizo hits hapo Wasafi ana mixes kali kweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom