Mfikishieni Mwinyi Zahera

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
MWAMBIENI MWINYI ZAHERA,KUFUNGWA KWA YANGA HAKUJATOKANA NA UCHOVU.


Nimemsikia kocha wa Yanga Mkongomani Mwinyi Zahera akizungumza na waandishi wahabari 22 Januari ,2019 baada ya timu yake kufungwa magoli 3-2 na timu ya Kariobang Shork toka nchini Kenya kwenye mashindano yanayoendelea nchini ya Sport Pesa.

Akieleza sababu ya timu yake kufungwa kocha huyo ingawa amekataa kusema moja kwa moja kama mwamuzi alichangia timu yake kupoteza mechi hiyo,ameonekana kuamini pia mwamuzi alikua sehemu ya wao kufungwa.Alichokisema moja kwa moja ni YANGA IMEFUNGWA KWA SABABU YA UCHOVU.

Mwambieni Zahera sababu si uchovu kama anavyoamini.Ukweli ni kwamba Yanga ni timu ya kawaida sana .Ushindi wake wa michezo zaidi ya 19 hautokani na ubora wa kikosi hiko bali ni udhaifu wa Ligi ya Tanzania.Tuna ligi dhaifu mno inayomfanaya Makambo aongoze kwa ufungaji bora.

Mwambieni , ligi ya Tanzania ni dhaifu mno mbele ya ligi za nchi nyingine.Sio ajabu kabisa kwa udhaifu huo Kariobang Shork inayoshika nafasi ya tano ligi kuu ya Kenya kuifunga Yanga inayoongoza ligi ya Tanzania.Ndio maana hakuna anayeshangaa kwa Banadari inayoshika nafasi ya pili Kenya kuifunga Singida United ya nafasi 13,hiyo ni hali halisi.

Papaa Mwinyi aambiwe, ligi ya Bongo ni maarufu tu na ina pesa kushinda ligi kadhaa za Afrika lakini umaarufu huo sio ushahidi wa ubora wake.Lazima iwe maarufu kama katika watanzania milioni 50 zaidi ya watanzania milioni 39 wanamiliki simu za mkononi.Hawa ndio wanaosambaza umaarufu wa soka la bongo kupitia Youtube,whatsapp,blogs nakadhalika.Wana uwezo wa kumpamba Makamabo akawa bora kuliko Lukaku wa Manchester United.

Akumbushwe Simba ilikua lazima ifungwe mbele ya timu inayocheza ligi ya Kongo iliyowatoa Benick Afobe(AFC Bournemouth),Yannick Bolasie(Everton),Elias Kachunga(Huddersfield Town),Chancel Mbemba(Newcastle United),Arthur Masuaku (West Ham United) dhidi ya mcheazaji pekee aliyezalishwa na ligi ya Tanzania anayesumbua Ulaya Mbwana Samatta wa Fc Genk?.

Mwambieni “mutu ya Kongo” Simba yenye Pascal Wawa ,Meddie Kagere,Okwi,Juurko Musrhidi haikufungwa na AS VITA goli tano kwa sababu ni mbovu la hasha,imefungwa goli tano kwa sababu Pascal Wawa wa Simba analipwa kwa kumkaba Eliudi Ambokile wa Mbeya City wakati Dharles Mondia Kalonji wa AS VITAL amepambana sana na Mbwana Samatta wa Genk enzi hizo.

AS VITA wana Emmono Eddy Ngoy wa Vital kakichapa sana dhidi Tressor Mputu aliyefanyiwa majaribio Arsenal ilihali James Kotei miaka yote anapambana na sure Boy wa Chamanzi wakati Yannick Bangala Litombo wa AS VITAL mshahara analipwa kwa kupamba na Tropiler Sunzu wa Zambia aliyecheza mataifa ya Afrika.

Zahera ambiwe ligi ya Kenya imezalisha Victor Wanyama(Totteham Hotspur) Macdonald Mariga aliyecheza fainali ya klabu bingwa ulaya,Johana Omollo anayesumbua Ubelgiji,Denis Oliechi aliyesumbua ligi kuu Ufaransa,Clinton Miheso ligi kuu ya Finland,Lawrence Olumu anayekipiga Malaysia,

Ligi hiyo imemtoa Brian Mandela anayecheza Afrika Kusini na dhidi ya ligi inayocheza Yanga iliyowatoa Hassan Kesi aliyepo Zambia, James Msuva wa Morocco,Himid wa Misri,na mwingine wa Botswana.Ligi ya Kenya inatoa wachezaji wanasumbua Ulaya sio vilabu vya Afrika kama sisi.



Mwaka 2017 mcheaji wa Azam raia wa Ghana Yakubu Mohamed alitoa ushauri kwa wachezaji vijana nchini mwake kupitia kituo cha radio cha Ghana Fox 97.7 FM kuwa kama wana malengo na safari yao ya mpira basi wasifikirie kuja kucheza Tanzania kwa sababu ligi ya Tanzania ni dhaifu mno na iliyokosa ushindani.

Yahaya alikua akijibu swali toka kwa mtangazaji aliyeuliza anaionaje Ligi ya Tanzania kwa kuilinganisha na ligi ya Ghana.Zahera ambiwe hata wachezaji wenye wanajijua kama wanmacheza ligi dhaifu.



James Kotei wakati anafanya mahojiano na mitandao inayojihusisha na mchezo wa soka nchini Ghana ya Ghana Soccernet na Soka 25 east Com amesema ligi ya Tanzania ina pesa nyingi na ratiba nzuri inayofanana na ligi kuu ya uingereza huo ndio ubora wake lakini haina vipaji kulinganisha na wachezaaji wa ligi nyingine.Na hili pia Zahera aambiwe.



Zahera aambiwe wachezaji wengi wa kitanzania wanapata namba kwenye baadhi ya timu kwa kubebwa na kanuni tu inayoweka kikomo katika idadi ya usajili kwa wachezaji wa kigeni na kanuni hii inayowadumaza wachezaji hawa.





Noel Nguzo.R.

23/1/2019.
 
Kweli kabisa wachezaji wetu hata physique yao mbovu sana nahisi huwa hawafanyi mazoezi ya kukupa mwili nguvu pia lishe duni
 
Hapana,ni mtoto wa Mama yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mara Yakubu Mohammed then anabadilika nakuwa Yahaya!! Propaganda zako zime fail na matokeo ya leo yameku umbua. Mbona michuano ya CECAFA upande wa vilabu Tz ina dominate. Ligi ya Tz inaweza isiwe ngumu kwa Africa ila kwa ukanda huu iko vizuri. Gor Mahia inaongoza Ligi ya Kenya imetolewa na Mbao ata top 6 haipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara Yakubu Mohammed then anabadilika nakuwa Yahaya!! Propaganda zako zime fail na matokeo ya leo yameku umbua. Mbona michuano ya CECAFA upande wa vilabu Tz ina dominate. Ligi ya Tz inaweza isiwe ngumu kwa Africa ila kwa ukanda huu iko vizuri. Gor Mahia inaongoza Ligi ya Kenya imetolewa na Mbao ata top 6 haipo

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi Mkuu,mbona unanishambulia Mimi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara Yakubu Mohammed then anabadilika nakuwa Yahaya!! Propaganda zako zime fail na matokeo ya leo yameku umbua. Mbona michuano ya CECAFA upande wa vilabu Tz ina dominate. Ligi ya Tz inaweza isiwe ngumu kwa Africa ila kwa ukanda huu iko vizuri. Gor Mahia inaongoza Ligi ya Kenya imetolewa na Mbao ata top 6 haipo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kenya Gormahia ligi ina mechezo 8.Tanzania mech 22 mpaka sasa....Taja wachezaji iliyotoa kuthibisha ubora wake. Tuna ligi maarufu sio bora
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom