Si dhambi tukiwa na aina yetu ya demokrasia!

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
KWA NINI TUSIWE NA AINA YETU YA DEMOKRASIA?


Tafsiri ya demokrasia kama ilivyotolewa na Abraham Lincoln kuwa ni utawala wa watu kwa ajili ya watu inaukakasi hasa kama watu wengi ni wajinga basi ni kuruhusu wajinga kuchaguana.

Lakini demokrasia ikitafsiriwa kama uwepo wa uhuru wa watu ,haki za binasamu,usawa wa sheria na mambo mengine ikiwemo usawa wa matumizi ya rasilimali pamoja na uhuru wa watu kuamua mambo yao wenyewe huleta maana timilifu.

Si hivyo tu demokrasia inayoharibu misingi yetu kama taifa na isiyokua na mstari ambao kama taifa hatupaswi kuuvuka ni hatari mno kuliko kutokua nayo.Demokrasia isiyojibu changamoto yetu ni sawa na haipo..

Mipaka yoyote itakayochomekwa kwenye demokrasia haiwezi kuwa udhaifu wa demokrasia wa nchi husika isipokua ni matokeo ya nchi husika kuheshimu misingi na utamaduni wake kama ilivyo kwa Japani,Spain Uingereza na baadhi ya nchi zenye demokrasia "yao" inayotambua ufalme na umalkia katika kuongoza nchi na waziri mkuu kwa upande wa serikali.Kwa nini na sisi tusiwe na yetu inayozuia matusi,dhihaka,kejeli kinyume na utamaduni na misingi yetu kama taifa?


Demokrasia haiwezi kuwa sawa kwa nchi zote duniani.Tofauti za utamaduni,haiba,silka,hulka,tabia,misingi,malengo na historia katia ya nchi moja dhidi ya nyingine lazima ilete tofauti ya aina ya Demokrasia.

Sio bidhaa inayotoka nchi moja kwenda nchi nyingine kama ilivyozaliwa Anthems Ugiriki karne ya tano kabla ya Kristo bila kuangalia hali hali halisi ya nchi husika.

Demokrasia kama mfumo unaotoa uongozi ni hatari sana kwenye nchi zilizopungukiwa ustaarabu,zilozoathirika na rushwa,zenye wananchi wenye uelewa mdogo nakadhalika.Kwa nini hizi nchi zetu zenye shida ya kupata viongozi wanaochukia rushwa demokrasia yetu isitoe muda mrefu wa utawala kwa watu aina hii iwapo tunatambua wakiondoka kwa muda mfupi hatutompata mwingine kirahisi?

Ni wazi kuwa suala la muda gani mnafanya uchaguzi halipaswi kua sehemu ya sifa za demokrasia kinachopaswa ni kuona uchaguzi unafanyika tena ni wa haki.

Kwa kiwango cha umaskini wa nchi nyingi za kiafrika.Na ukubwa wa changamoto zake si sahihi kuwa na uchaguzi kila baada ya miaka 4 au 5.Si tu ufupi wa muda haumpi rais nafasi ya kukamilisha agenda zake lakini ni matumizi mabaya ya rasilimali kwa nchi hizo.

Zipo hoja kadhaa za kitafiti zenye kuhusisha maendeleo ya nchi na uwepo wa demokrasia.Lakini tafiti hizi zipo kimya kusema aina ya demokrsia ya nchi hizo zilizoendelea si sawa na demokrasia tunayoimbiwa tuifuate.Demokrasia ya nchi zilizoendelea zina mistari na maumbo tofuati tofuati yenye kuonesha mipaka.

Wengine wameiremba remba demokrasia yao na kuzalisha aina mpya ya demokrasia mfano "a two party consisting".nchini Marekani na kwingineko.

Japan wao wanayo yao "mult party bicameral parliamentary representative demokrasi" wananchi hawachagui mkuu wa nchi zaidi ya kiongozi wa serikali.Kama mkuu wa nchi hachaguliwi na wananchi huo ni mpaka kwa nini na sisi demokrasia yetu tusiiweke mipaka?

Lakini japani pia Kukumbatiana, kuhagi, kumshika mtu bega, mikono, kumwangalia mtu sanaaa, kutongoza, kuongea na simu kwenyr mhadhara au mbele za watu hairuhusiwi nchini japani.

Japani ingekua bara la Afrika makatazo hayo machache ingesemwa ni kukosekana kwa demokrasia.Afrika wanataka democrats isiyo na mstari ambao hautakiwi kuvukwa.

Ugiriki kama ilivyo Marekani kando ya SYRIZIA,vyama vinavyotawala siasa za nchi hiyo tangu 1980 ni viwili tu PASOK na ND
kuliko Tanzania ambayo kwa miaka 27 ya siasa za vyama vingi tumeviona vyama vikipokezana "ukubwa".

Uchaguzi wa mwaka 1995 NCCR MAGEUZI,Mwaka 200 chama cha wananchi CUF,mwaka 2005 CUF tena kuanzia mwaka 2010 mpaka sasa ni chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA.


Marekani inayoaminika kuwa ni baba wa Demokrasia tangu mwaka 1850 mpaka sasa licha ya kuwepo kwa vyama vingine kama kama Green Party,Libertarian Party,Constitution Party lakini vyama vilivyotawala siasa za Marekani ni viwili tu ,Democratic na Republican ingawa vipo vingine kama Libertarian Party,Green Party of United States na Constitution Party Kwa nini na sisi tusiwe na demokrasia yetu ?

Kama hata Marekani tunaoamini ni baba wa demokrasia duniani wana demokrasia yao iliyochora mstari kwa nini sisi hatuna?

Mei,1992(mwaka ambao mfumo wa vyama vingi ulianza Tanzania) katika mji wa Los Angels nchini Marekani kulizuka ghasia kubwa sana ambazo baadae zilisambaa kwenye majimbo mengine 20.

Sababu za vurugu hizo ni uamuzi wa mahakama ya Simi Valley ya jiji la Los Angels kuwaachia huru askari polisi wa nne waliompiga vibaya na kumjeruhi Marekani mweusi Bw Rodney King.

Hukumu hiyo iliyoonekana dhahiri ni sehemu ya ubaguzi wa rangi iliamsha hasira kwa wamarekani weusi walioamua kuchoma moto maduka,magari,nyumba na ofisi za serikali.Inadaiwa jumla ya watu 40 walipoteza maisha kwenye vurugu hizo na zaidi ya 2000 kujeruhiwa.

Ikumbukwe wanasiasa wengi wa Afrika kwenye mifano yao hupenda kuitaja Marekani kama baba wa Demokrasi.Kama.kuna nchi yenye demokrasia iliyokamilika pasi kuchora mstari kwa nini mahakama ilitoa hukumu ya namna ile?Kwa nini watu walipigwa?.

Inakuaje Marekani mahakama inatoa hukumu ya aina hii na bado ikawa ni demokrasia ,Tanzania kunyimwa dhamana kwa Freeman Mbowe aliyekaidi masharti halalai ya mahakama ionekane ni uvunjwaji wa demokrasia?

Inapodaiwa mipaka ya demokrasia ni sehemu ya kutetea misingi yetu kama taifa inayotufanya tuwe wamoja na kutambulika kama taifa.Kuliko kuivunja misingi hii ni bora tukawa na mstari katika demokrasia yetu.

Kama tunakiri Tanzania kama nchi ina upungufu wa kupata viongozi waadilifu kuna tatizo gani iwapo tukawa na demokrasia ambayo mara kiongozi wa aina hii akipatikana tukawa na namna ya kumtumia kwa mda mrefu kabla ya kuwa na uhakika wa kumpata mwingine?

Sote tunakubali kuwa,hayati Julius Kamabarage Nyerere ni moja ya rais bora pengine kuliko wote wa nne tuliopata kuwa nao.

Lakini hatutaki kukubali pia upo uwezekano wa ubora huu wa mwalimu umechangiwa na muda mrefu aliokaa madarakani kuliko rais yeyote yule kati ya wa nne anaolinganishwa nao.

Katika nchi ambayo ina ombwe la kupata viingozi wazuri lazima tuwe demokrasia inayotupa muda wa kutengeneza kiongozi mmoja baada ya mwingine.Lazima itupe muda mrefu wa kumtumia kiongozi bora anayepatikana kabla kama Mwl Nyerere alivyotumika miaka 25.

Hapa ndipo ninapounga mkono hoja ya mbunge wa Nchema ,Juma Selemani Nkamia.Tukijiridhisa kama nchi baada ya kwamba tumempata Nyerere mwingine kuna kuna tatizo gani la kupanua muda wa uongozi iwapo wote tunakumbuka tulivyohitaji kiongozi aina hii?.

Mara zote tupatapo nafasi tukumbushane kuwa,mataifa ya magharibi yamekua yakichukua hatamu za uongozi duniani katika nyanja za uchumi,siasa,ulinzi na kadhalika kwa kuzua suala la demokrsia kama moja ya haki za msingi.

Demokrasia ni sharti mojawapo la misaada na mikopo kutoka vyombo vya fedha na mataifa ya nchi wahisani.Kwakua sisi wenyewe tumeshindwa kuweka mstari wa demokrasia tuliyorithishwa,inatumika kama fimbo mara mataifa ya kimagharibu yanapotaka kupenyeza agenda zao.Ni muhimu tukawa na demokrasia yetu peke yetu itakayofafanuliwa kwa katiba na sheria zetu ili kukwepa mitego ya mataifa haya.

Noel Nguzo.

10/02/2019.
 
Yawezekana ukawa na jambo jema na wakati huohuo unataka kuhalalisha haramu.Haiwezekani.Umeuma,unanusa na kupuliza huku unachungulia kwa chati mnoo.Ujanjaujanja!
Kwa maana unataka kutuhabarisha kuwa;
-Una mahaba mazito na demokrasia
-Unataka nchi iwe na demokrasia ya kipekee duniani
-Unataka tuamini kuna "wateule wa Mungu" wanapaswa kutawala tu hadi tuhakikishe mbongo zao zi dhooful hali ndiyo tuwateme kama makapi ya chikichi
-Yawezekana unataka kwenda mbele zaidi hupendi chaguzi za kidemokrasia huku una mapenzi mazito nayo.Sijui imekaaje hii?
-Huamini katika demokrasia ya vyama vingi yenye vyama vingi zaidi ya viwili.Sasa sijui demokrasia gani hiyo iliyokaa kama pande mbili za nchi zinazopambana vitani bila kuwa na changamoto za kutoka kwa wengine?
 
Haya tunampa Sizonje miaka 100. Lakini hatuna katiba bora, utawala haulindi haki za raia, kumkosoa mtawala inakuwa ni dhambi kuu.

Wakati huo huo yeye akitoa maneno yenye ishara ya dharau, kebehi, majigambo na majivuno.
Kipindi tu hiki cha muda mfupi tumeona vituko vyake.
Sasa akipewa dahari si tutaona makosa kapu kwa magunia. Kama mnataka maana ya demokrasia kwa maana yenu, ni dhambi kutumia neno "demokrasia" mkasema mna demokrasia yenu ya kinyumbani nyumbani.

Hiyo itakuwa "demokrasia uchwara"
 
Back
Top Bottom