Ruge Mutahaba ametufundisha kujitafuta

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
250
KIFO CHA RUGE MUTAHABA KITUFUNDISHE KUJITAFUTA.

Mimi ni mmoja kati ya mamilioni ya watanzania waliofatilia kwa ukaribu sana mazishi ya aliyekua mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliyefariki February 26,2019.

Katika siku tano nilizofatilia mazishi yake nimemsikia mtu mmoja tu aliyeandika kwenye akount ya Facebook kuwa atamkumbuka marehemu kwakua alikua"anampiga vizinga".Jacob Mbuya ndiye pekee aliyekiri hadharani marehemu alikua anampa pesa.

Wengine wote niliowaona Ruge wanamkumbuka kwa alivyoyagusa maisha yao kwa kuzifanya ndoto zao kuwa kweli iliyo hai.MarehemuRuge hakua mbunge,waziri,mkuu wa mkoa,balozi wala mkuu wa wilaya lakini amezikwa kuliko viongozi wengi watakavyozikwa.

Iwe ni kweli msiba umepewa"promo"kubwa kuliko uhalisia ama si kweli ,lililomuhimu tumeona,tumesikia,tumesoma watu wengi wakionesha hisia zao kwa marehemu kuliko mazishi mengi tuliyopata kuyashuhudia hapa nchini.

Ruge hakutafuta mafaniko duniani alitafuta ukubwa tu.Kuna tofauti kati ya ukubwa na mafanikio
Je ukubwa ni nini?Ni umaarufu?ni ushawishi?ni wingi wa pesa na magari ya kufahari?.Eddo kumwembe anapopost tripp zake za ndege kila mwisho wa wiki ni ukubwa au mafanikio?.

Ili uwe mkubwa unapaswa kufanya jambo kwa kusudi ya kulifanya jambo lenyewe.Ndio maana unaweza kutafuta picha ya Ruge Mutahaba akiendesha gari ukaiokosa lakini ukitaka aliyokaa na watu utazipata zaidi ya laki.Ukitafuta aliyekaa kwenye ndege unaweza ukaikosa lakini nyingine ukazipata.Haina maana Ruge hajawahi kupanda ndege lakini kwakua alikua anatafuta ukubwa sio mafaniko picha ya kwenye ndege si sehemu ya malengo ya akifanyacho ndio maana hata kama aliwahi kupiga hatujawahi kuiona.

Kuna watu hawakua na pesa lakini walikua wakubwa dunia nzima,kundi hili wapo wakina Bobby Marley,Martin Luther King,Julius Caesar,Walt Disney,Julius Nyerere,William Shakespeare.Licha ya kutokua matajiri dunia inawakumbuka mpaka kesho.

Tafuta ukubwa.Kuna tofauti kati ya ukubwa na mafanikio.Hebu wakumbuke watu hawa Stephen Van Rensselaer,Alan Rufus,William De Warrene.Hawa walikua miongoni mwa matajiri wakubwa duniani.Walikua maarufu kweli kweli duniani lakini walipokufa na majina yao yakafutika.Ukubwa ni zao la idadi ya watu uliowafanya wafike au kukaribia walipotaka kufika wakati ukiwa hai.Ni tunda la muda ulioutoa kutumika kwa wengine ukiwa hai.

Hata wewe watu wengi unaowakumbuka ni wale uliotumia muda mwingi ukiwa nao.Muda ni kitu cha thamani ambacho kama utakitoa kwa wanaokuzunguka hautosaulika mapema.Toa muda wako kwa faida ya wengine hasa marafiki,wafanyakazi wako,ndugu na jamaa kila kila mara.

Kuwa mtu wa kutoa zaidi kuliko kupokea.Watu unaowakumbuka sana ni wale waliokupa zaidi kuliko uliowapa.Inaposemwa kutoa haina maana matoleo ya pesa ama vitu vya thamani .Ruge alitoa heshma,upendo,msaada,ushauri na mengine anayoweza.

Jichukue na jipeleke siku yako ya mwisho ambayo utakua kwenye jeneza.Jaribu kufikiria wewe na maisha yako ya kupenda rushwa nini kitaandikwa kukuhusu?.Watakaokua wanalia watalia kwa sababu umekufa mapema?umeacha watoto au uliwauzia haki zap kwa fedha ulizonunulia magari ya kifahari?

Maisha sio kula ,kuzaa na kusubiria kufa.Kwakua tumependa kuishi basi haihuzunishi tukifa.Kiwango cha huzuni utakachokiacha duniani baada ya kifo chako kitategema tabia yako ya kusaidia bila kupoteza hamu ya kujitolea wakati ulipokua hai.Kadri maisha yako yatakavyowagusa watu wengi ndivyo alama yako baada ya kufa inavyozidi kuwa kubwa.

Inashangaza kuona Nandy analia kiasi cha kushindwa kuimba mbele ya jeneza la Ruge lakini hajui kwa nini anamlilia Ruge.Laiti angejua sababu inayomliza kwa uwezo na alipofika sasa angelikua amekwisha tengeneza Nandy mwingine.Hajui kwa sababu ana hofu ya kupitwa na tamaa ya kuwa wa kwanza.Ruge angekua na hofu hii machozi ya Nandi yasingechafua kitambaa.

Ni mambo gani upo tayari kuyanya ili yawe alama yako hapa duniani?Ni historia gani unataka isomwe kwenye mazishi yako?Kama wewe ni mchambuzi mzuri wa michezo kama Shafii Daud ukifa hujatengeneza mchambuzi hata mmoja ilihali uwezo ulikua nao hiyo ni dosari itakayoondoa alama ya maisha yako baada ya kifo chako.

Nimemuona Elizabeth Michael "Lulu" akiuza nguo zake ili apate pesa za kuwasaidia wasiojiweza.Nimemuona Haji S.Manara akianzisha taaisisi ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi.Hivi ndivyo ukubwa unavyotengenezwa.

Nina hakika kila star wa kitanzania akiamua ana uwezo wa kusaidia watanzania wawili mpaka safari.Roma Mkatoliki azalishe Roma wake wawili,Maulidi Kitenge azalishe Vitenge wengine.Kingwendu Kingwendulile asaidie vijana wa Kibada.

Kuliko kushinda kwenye mitandao kuonesha mali mnazomiliki,ni bora kuonesha unavyosaidia.Hakuna picha hata moja uliyopost instagram uliyopiga ukiwa unaangalia mpira kwenye uwanja wa Old Trafford itakuja kukuzika.Picha uliyopost Facebook ukiwa juu ya ndege sio alama yako baada ya kufa.

Wapo wengi sana wameshaondoka duniani lakini wewe bado upo sio bahati mbaya una jukumu hujalimaliza duniani.Una kila kitu,una pesa,una watoto,una mali za kutosha na unahisi umeridhika na maisha uliyonayo JE UPO TAYARI KUFA LEO?

Noel Nguzo.
3/3/2019.
 
sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,200
2,000
Ameacha legacy..umegusa vitu vya msingi sana..ni kweli Ruge aliamini maisha yake na mafanikio ni vyake..lakini aliangalia awasaidieje wengine wafikie mafanikio yake.. hata aliowasaidia wakawa bize kutuonyesha mafanikio yao zaidi kuliko yeye aliewawezesha kufikia pale..Kitu ambacho Ruge alifanya ni kuwanyima watanzania ya kumjua ye ni nani..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
alibaaliyo

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
401
500

Njundelekajo umeandika vyema kuhusu Ruge. Nashauri uandike kitabu kumhusu mtu huyu. Itakuwa kumbukumbu nzuri. Nakala nyingine sambaza internet

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom