Hata mimi nimeliona hilo tatizo,halafu ni sugu kwa Yanga lakini kocha yupo na anaangalia tu.Kwa kifupi kwa mechi kama ya leo yanga kashinda lakini mimi mshabiki roho ilikuwa bado juu mpaka mpira ulivyoisha,na hata mechi ya marudiano sina imani kabisa kama anaweza kusonga mbele kwenye hatua ya...
Siyo wabovu kihivyo,labda kwasababu Chirwa,Makapu na Yondani watakuwa wameshamaliza adhabu.Hata kipa wao kasema kabisa wana uhakika wa kusonga mbele.Mimi kinachoniogopesha kwa Yanga siku zote huwa wanadharau hizi timu ambazo hazina majina
Naiona mechi ngumu sana tukienda Ethiopia kama mpira wenyewe huu wanaocheza Yanga sijui.Mwalimu naona ana mbinu hafifu sana halafu mzito sana kufanya mabadiliko kwa wachezaji ambao hawako vizuri uwanjani
Sana sana tumewaambia hawasikii,sasa tunaona mwishowe tuseje gombana wakati uwezekano wa kujirekebisha haupo.Hapo ndipo nilichukua uamuzi wa kumhamisha mtoto tu
Mimi niliwavumilia term mbili tu nikamhamisha mtoto haraka mno.Maana nilijaribu kuangalia mwenendo wao nikaona hapana,kwanza darasa lina wanafunzi wengi sana kiasi kwamba mwalimu kuwamudu watoto wote kwa ufasaha inakuwa ni ngumu.Halafu hawana diary kwa ajili ya mawasiliano ya mtoto na walimu
Hilo jambo hata mimi huwa wananiambia hivyo hivyo kwamba wameshapeleka namba wizarani kwahiyo kuna ugumu japo mimi mwanangu alikuwa darasa la pili.Mpaka sasa naendelea kusumbuana nao lakini mtoto hapo nilishamtoa namba itafuata baadaye
Mhamishe mapema sana,na suala la maji kweli kwa pale ni pasua kichwa nilishuhudia watoto wakinywa maji ya bomba nilichoka kabisa.Halafu huwa hawaruhusu mtoto kuja na maji ya kunywa kutoka nyumbani
Halafu walivyo watu wa ajabu siku ukienda kumhamisha mtoto pale wanakupeleka kwa mwalimu wao sijui ni mshauri au ni mwalimu wa taalum.Anaanza kukuhoji kwa unyenyekevu ooohhh tatizo liko wapi,ukishamwelezea anakwambia tupe muda tutajirekebisha na umwache mtoto aendelee kusoma hapahapa.Mimi...
Aliniacha hoi siku ya kikao cha wazazi,wazazi wakatoa kero zao na dukuduku likiwepo hilo suala la usafiri.Jibu alilolitoa ni kwamba sisi tumeona ile shule ni nzuri ndiyo maana tunapeleka watoto wetu pale vinginevyo kama tunaona huduma siyo nzuri tusingewapeleka pale.Lilivyotoka hilo jibu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.