Kero ya Vidhibiti mwendo kwenye Mabasi ya Mikoani

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,433
12,282
Chinga One nawasalimu wana JF,

Baada ya Salam hizi napenda kutoa pongezi kwa Sumatra na Jeshi la Polisi Tanzania kwa jitihada wanazochukua kukabiliana na ongezeko la ajali barabarani na lakini pamoja na jitihada hizo imejitokeza kero ambayo abiria wengi wanailalamikia kutokana na Bus hizo kufungwa ving'amuzi ama vidhibiti mwendo vinavyolazmisha Gari zisitembee zaidi ya Spidi 80 ambayo kiuharisia kwa safari za Bus hiyo spidi ni ndogo mnooo.

Kwa sasa kusafiri mikoani imekuwa kama adhabu sehemu ambayo zamani ulikuwa unasafiri masaa 9 let us say Dar Iringa sasa hivi utasafiri masaa 15,inachosha mnoo yani kama unajambo lako unawahi kijijini kwenu sahau kabisa,nadhani kwa masafa ya Mbeya Dar au Dar Arusha siku hizi unaweza kusafiri saa 24,too much boring mazee,hata kama tunapambana kudhibiti ajari but sio.kwa namna hii.

Ushauri:Ni vyema wakaangalia upya swala hilo la Spidi 80 waweke hata 100 atleast mana safari za mikoani si lelemama.

Naomba niishie hapa kwa sasa.
 
Huo mwendo unatosha sana mkuu na umesaidia sana kupunguza ajali
 
Imesababishwa na mwendo kasi?
Haijasababishwa na mwendo kasi ila sehemu ilipotokea napafahamu kuna kimlima kakali kushuka kuingia mbalizi kama dereva uko na gari (lorry)yenye mzigo mkubwa usipokuwa makini gari inakushinda ndio kama hivyo unaweza sababisha ajali au ukaliangusha bondeni huko
 
Aisee spidi 80 ni kero mnoooo kwa abiria. Ni spidi ndogo na inachosha mnoooo. Mi naona dawa ni moja tufanye magari yote ya private, Serikali na mabasi yaende spidi 80 ndio watajua kero yake. Wao wanatembea spidi 160 ndio maana hawaoni kero yoyote ya spidi 80.

Binafsi reasonable spidi iwe 110 sio 80 iliyopo sasa. Hiyo spidi 80 ni ya enzi hizo barabara ni mbovumbovu.
 
Aisee spidi 80 ni kero mnoooo kwa abiria. Ni spidi ndogo na inachosha mnoooo. Mi naona dawa ni moja tufanye magari yote ya private, Serikali na mabasi yaende spidi 80 ndio watajua kero yake. Wao wanatembea spidi 160 ndio maana hawaoni kero yoyote ya spidi 80.

Binafsi reasonable spidi iwe 110 sio 80 iliyopo sasa.
Kabisa mkuu,unajua wanaotetea spidi 80 wengi wao hawajui na wasafiri wengi wamezoea bodaboda tu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom