Ngeleja ananitia kichefuchefu maana kweli anatufanya wapumbavu kutudanganya makali yanapungua ilihali ndio yakaongezeka mara dufu haujui muda gani umeme upo. Anatutia hasara sana hasa kwa wanaotafuta kipato kidogo kwa kutumia umeme, kama hakuna umeme hauna pesa ya kula nyumbani
Haya itabidi siku hiyo nivae tena, maana mwenzenu nimechoka kweli kweli na hii nchi umefika wakati wa kufanya maamuzi wala tusiogope maana tunapelekeshwa ovyo na wachache
Labda niulize kwanini wamechagua tarehe 3? Mi naona mbali sana maana sasahivi hali inazidi kuwa tete hali ni mbaya zaidi kwanini tusiamue hata kesho? Mi nimeanza leo kabisa kuvaa nyeusi maana nyumbani kwangu walinirudishia umeme masaa 4 tu tena usiku wakati nimelala halafu wakauchukua tena. Wiki...
Hao watoto waliovishwa maboya kama hawajui kuogelea inakuwa ni ngumu kujiokoa, maana wamekaa majini masaa mengi sana. Ila kama wangeokolewa mapema idadi ya waliokufa ingepungua
Ni sababu za kiusalama, mi nafikiri angekwenda kukaa kwa wakubwa wenzake huko kuliko na usalama kuliko kutufungia njia wananchi wa kawaida kisa usalama wake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.