Habari za muda ndugu zangu.
Kwanza kabisa niipongeze serikali kwa juhudi za kuajiri hasa mwaka huu wa 2023, imejitahidi sana kuajiri vijana katika kada mbalimbali tofauti na za ualimu na afya sambamba na pongezi hizo naomba serikali kupitia wizara hasa TAMISEMI wawape maelekezo na miongozo...
daaah hongera sana mkuu,hakika Mungu ni mwema,ukawe mtumishi mwema maana wewe ni mingoni mwa watu tulioanza na huu uzi tangu mwanzo mpaka leo nakumbuka jinsi ulivyo na moyo wa uvumilivu,sijalamba asali ila nina furaha sana juu yako.
Sijui kama na wenzangu mmenoti ila upande wa adverts naona wameakaa kimwa kimya kwa mbaliii zikija ni post za managerial na zile za halmashauri ila post za officers naona hawaiti.sijui kuna nini kinatengenezwa.
Mkuu na wewe ni miongoni mwa wale barua zao za tangu mweI wa nne maana kuna mtu tulifanya nae mwezi wa pili kakuta barua ya mwezi wa nne mpaka nikasema inaonekana mzee alikuwa mgumu sana kusain barua
mkuu ujue kuingia oral sio mchezo yaan mimi huwa nahesabu ni kama bahati tu na ndio maana maandalizi ya oral huwa yanakuwa makubwa sanaa kwa sababu mule ndio kila kitu ila basi tu ukiwaza sana unaweza kuchanganyikiwa tu
Oral mojawapo niliyofanya nafasi zilikuwa 8 na written nilikuwa niongoni mwa top 4,hiyo nyingine nafasi zilikuwa 40+ na written nilikuwa miongoni mwa top 10. Stelingi
Kwa namna oral hizi mbilo nilivyojibu,daah basi sijui nilikwama wapi maana kila kitu nilifanya kwa usahihi ila yote tunamuachia Mungu maana huenda watu walifanya zaidi yangu.
Kinachouma mpaka watu wanadai matokeo ya oral ni kwa sababu mpaka kuingia oral yenyewe hiyo ni bahati tu
Kwan bwana mwifa kama una uelewa hebu tueleze hii inakuwaje maana nasikia sikia tu unakuta wanasema kuwa huenda mtu unakuwa ushapangiwa placement ila taasisi yako ikakaa hata miezi minne mbele ndio ikahitaji hao wafanyakazi
Mwifa hebu tueleze hii maana mfano kuna watu nilifanya nao oral mwaka jana mwezi wa 9 tulikosa placement lkn wakapata mwaka huu mwezi wa 6 taasisi ile ile japo nafasi za mwaka jana zilitoka zote,kuna watu nikafanya nao mwezi wa pili mwaka huu,yaan jamaa wote wakatoka nikabaki mimi pamoja na...
Pole masta,Mungu ndio anajua mapito yako brother...keep fighting bro,ukisema humu kuna watu watakukatisha tamaaa na kukuona mzembe ila hili la utumishi na mchakato nadhan kuna watu wameshapoteza matumaini kabisa na kupoteza imani na taasisi hii
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.