Bill nakupongeza na kukushukuru sana kwa hili. Laiti ningekuwa Dar ningeshiriki mkutano huo. Benki hii imenitendea maumivu makali sana kati ya mwaka jana na mwaka huu hadi ikanibidi kuachana nayo kinamna kwa kuhamisha mshahara wangu.
Nasubiri yatokanayo kasha nitachangia maana wanaudhi...
Ningekuwa Insane nisingeingia humu kwa kuficha ID NI KWELI TUMEMTEMBELEA HOSPITALI YA LUTHERAN HAPO ARUSHA na kama ungekuwa na hamu ya kufahamu ukweli na sio kukimbilia kushabikia taarifa kwa kuwa zinagusa unalolipenda bila shaka ungetafuta chanzo cha taarifa kingine kikakueleza vema.
Tumetoka kumuona muda si mrefu na kwa maelezo ya daktari anayemtibu katika hopitali ya Selin hana hata mchubuko wala jeraha licha ya kuwa yeye anasema anaumia sana
[/B]
Yaani mtu mwenye akili uchukue quote ya Jussa kuhusu mazungumzo ya Dk Salmin? JF inazidi kukosa heshima na kwa mwendo huu inaanza kujizika kaburini
Wakuu acheni ndoto, juzi tu nilikuwa Musoma Mjini na wananchi wa jimbo hilo zuri waliniomba nami nigombee Ubunge mwaka 2015 na wananikubali kweli. Sasa hizi siasa za kutuma watu wakusemee humu JF inachekesha sana lakini hakuna tatizo nawakaribisha wagombea wote wanaotamani kunisindikiza. This...
Nilitegemea ungekuja na thread ya kutaka kujua nafasi ya Makamu wa Rais katika Katiba mpya lakini kwa kujifanya umefanya utafiti wa kuwa Makamu aliyepo anafahamika amamla umeenda choo cha nje, maana umeanza kwa kumtaja jina hali inayoonyesha kuwa unamfahamu na hawa unaotaka wamjadili...
Sina shaka naanza kukuelewa wewe uliyeleta mjadala huu! Una haki ya kujadili Katiba na hilo hakuna mwenye uwezo wa kukuingilia lakini kama nia ni kuchafua watu, bila shaka hauko juu ya sheria
Kama kuna falsafa ambayo binadamu hakupata nafasi ya kuitambua ama kuielewa haraka ni kuhusu maisha. Binadamu asiyejiuliza kuhusu yeye kuwa nani na kwa nini yuko alipo na kwa nini anafanya afanyalo bila shaka atakuwa ni binadamu wa pekee. Inawezekana binadamu wa aina hii akawa amebarikiwa maono...
Kiongozi kwani ungeandika tu website haijabadilishwa kuna tatizo gani? Naona taarifa unazo na si za uongo lkn unashambulia website na wana ICT wa UDOM kwa kutaja jina la Makamu wa Rais ambaye ahusiki na mabadiliko hayo. Busara ni jambo jema sana katika maisha. Nawasilisha.
Tangu nianze kusoma post hii uliyoileta hapa nilipata maswali kadhaa na kisha kugundua yafuatayo:
1. Ninakufahamu na hukutegemea nijitokeze kukujibu hapa, nakufahamisha tu kuwa sina uoga katika kuzungumzia ukweli hata kama utakuchoma na hata kama utatoa tafsiri kama ambazo umeweka hapo...
Ndugu yangu nadhani hoja hii mmejipanga kutafuta jambo, kwanza mlianza na Makamu kwenda USA kutalii sasa mnabadilika. Kama ingekuwa ni kwenda USA nisingeingia kukujibu nimetoa majibu pale mlipopotosha safari ile ya kuiwakilisha Tanzania UNAIDS na utalii. Pili nimezungumzia safari ya Dk mbugani...
Hapo kwenye red, ndugu yangu jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Dk Bilal si kiongozi mbabaishaji ama mwenye kujenga chuki, ni kiongozi mwenye mapenzi mema na watu na ndio sababu amebaki kuwa kipenzi cha wengi si tu katika Zanzibar, Tanzania bali popote alipopata kuishi. Kwa msingi huo...
Arafat, hoja zisizokuwa na mashiko hazina maana yioyote hapa. Umeandika makala ndefu umelinganisha viongozi wanaotokea Zanzibar ambao hawajawahi kufanana kwa hulka wala matendo. La muhimu nililolipata kwako ni kutafuta kutangaza uongo kwa lengo unalolijua, Dk Bilal ambaye nahusika naye hajawahi...
Hoja hizi zinazohusu masuala ya Taifa na umuhimu wa watu kuungana zinahitaji watu kufahamu tulipotoka na tunapokwenda. Mwanakijiji nakushukuru kuibua hoja hii, kusigana mawazo kuhusu muungano si hoja hatuwezi kuwa na hoja moja hayo tunayoyaita matatizo ama kero ni muhimu kuzipima lakini...
Raıs wa Zanzıbar alıkuwa Uturukı kwa mwalıko wa nchı hıyo na Makamu wa Raıs ameenda kumwakılısha Raıs katıka mkutano wa Umoja wa Mataıfa unaohusu Maendeleo ya Nchı Maskını. Kazı hızı mbılı...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.