Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Nimekuwa nikikosoa sana kuwa viongozi wetu wengi hawana ujasiri wa kuutetea Muungano wazo wamebakia kulalamika pembeni; na wale wanaosimama kuutetea wanautetea kwa minajili ya kisheria kuwa "ni uhaini kuvunja" au ni makosa na wengine wako tayari kusema "tuuvunje tu yaishe". Dr. Bilal amefanya utetezi japo kidogo lakini utetezi wa kwanza ambao binafsi unanipa matumaini kuwa wapo watu wenye kuthubutu kuutetea Muungano bila aibu au kuwaogopa watu. Je, nani mwingine atajitokeza kuutetea Muungano wetu? Je wataweza kusimama na kuutetea kwa hoja kweli na siyo vitisho au kejeli?
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, amesema itatokea hasara kubwa iwapo Wazanzibari watakubali kuuvunja Muungano.
Akiwahutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la tawi la CCM Mwera Misufini Wilaya ya Magharibi Unguja, alisema mabadiliko ya Katiba yasiwe chanzo cha kuzorotesha Muungano.
Alisema marekebisho hayo ya Katiba lengo lake kubwa ni kuimarisha Muungano ambao umeleta faida kubwa ikiwemo kujenga umoja wa kitaifa.
Aliongeza kuwa kuwepo kwa kasoro ndogo ndogo katika Muungano isiwe kigezo cha kutaka kuuvunja wakati Serikali za Muungano na Zanzibar zilidhamiria kumalizia kero zilizobakia baina ya pande mbili za Muungano.
Hasara kubwa itatokea endapo wananchi wakikubali Muungano uliopo baina ya Tangayika na Zanzibar kama utavunjika, alisema.
Alisema kwamba yapo mataifa mengi yamekuwa yakifika nchini kujifundisha Muungano ulioasisiwa na marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume.
Dk. Bilal alisema sio vyema kuuchokonoa Muungano au kubeza kutokana na kasoro ndogo ndogo zilizopo na badala yake amewataka wananchi kutumia uhuru wa Kikatiba wa kutoa maoni wakati ukifika ili kuimarisha Muungano huo.
Viongozi wetu waliopita waliona mbali na kuamua kuleta Muungano kutokana na kutambua faida zake na wananchi wa pande zote mbili wamekuwa wakinufaika na Muungano wetu, alisema.
Aidha, alisema wakati huu si wa kufikiria kuukataa Muungano, wakati mataifa mengi duniani yameamua kila taifa litakuwa likijitegemea.
Huu sio wakati wa kufikiria kuukataa Muungano, wakati mataifa mengi duniani wameamuwa kuungana kwa malengo ya kuunganisha nguvu za kiuchumi, alisema.
Aahidi waliochomewa moto vibanda kuhudumiwa
Serikali ya Muungano itashirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuhakikisha kuwa taratibu za umiliki wa ardhi zinafanywa haraka ili kuwawezesha wananchi waliochomewa moto vibanda vyao katika maeneo ya Pwani Mchangani, mkoa wa Kaskazini Unguja kupata sehemu ya kudumu ya kufanyia biashara.
Ahadi hiyo ilitolewa juzi na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi hao aliposimama kwa muda kwenye kambi yao iliyoko maeneo ya mpakani mwa Pwani Mchangani na Kiwengwa kuwapa pole.
Dk. Bilal alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaelewa matatizo hayo na kwamba itafanya kila jitihada kuhakikisha wanapewa maeneo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za biashara.
Serikali inaendesha shughuli zake kwa kufuata Katiba. Hivyo, mtahudumiwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi, alisema.
Hata hivyo, aliwataka wawe na subira wakati serikali ikifanya taratibu za kupata maeneo mengine.
Dk. Bilal alisema nchini Tanzania kuna uhuru wa kufanya kazi mahali popote pale mradi mtu havunji sheria na kusema hakuna atakayenyanganywa uhuru huo.
Dk. Bilal alitoa ufafanuzi huo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Kaskazini B, Riziki Juma, kuwa wilaya imetenga maeneo hayo ya mpakani mwa Pwani Mchangani na Majeta kwa ajili ya wahanga wa moto lakini hawawezi kuyatoa mpaka Wizara ya Ardhi Zanzibar ikamilishe taratibu zake za umiliki wa ardhi katika maeneo hayo kwa kuogopa waisonekane wavamizi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Kaskazini B, tayari wametoa taarifa kwenye ofisi ya Maafa na Msalaba Mwekundu kuhusu tatizo hilo ili liweze kushughulikiwa.
Wananchi zaidi ya 50 ambao wengi wao ni wenye asili ya Tanzania Bara, walichomewa moto vibanda vyao vya biashara katika maeneo ya Pwani Mchangani na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwezi huu.
Wakati huo huo, Mahakama ya Mkoa Mfenesini Mkoa wa Kaskazini Unguja, imewaachia kwa dhamana washtakiwa wote wanaotuhumiwa kuchoma moto maduka na nyumba zilizokuwa zikimilikiwa na wafanyabiashara wenye asili ya Tanzania Bara.
Washtakiwa hao saba waliachiwa kwa dhamana na Hakimu Faraji Shomari Juma, baada ya kufikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo, mjini Zanzibar jana.
Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka, Omar Khalfan Sururu, alidai kuwa watuhumiwa walichoma moto mabanda katika kijiji cha Pwani Mchangani Zanzibar Mei 6, mwaka huu.
Hata hivyo, washtakiwa wote walikana mashtaka yote 17 waliosomewa.
Washtakiwa hao ni Haji Ame Iddi (45), Talib Faki Ame (60), Mohammed Haji Sheha (21), Mohammed Masoud Afadhali (21), Mwinyi Abdallah Msanifu (22), Hassan Makame Chande (21) na Thabit Muombwa Thabit, wakazi wa Pwani Mchangani Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
CHANZO: NIPASHE