Ukitaja Viongozi Wanafiki waliowahi kuihadaa Zanzibar Ukimtaja Maalimu Seif usimsahau na Dr.Bilal | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukitaja Viongozi Wanafiki waliowahi kuihadaa Zanzibar Ukimtaja Maalimu Seif usimsahau na Dr.Bilal

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Arafat, Jul 9, 2011.

 1. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Dr Mohammed Ghalib Bilal aliteuliwa kuwa CM wa Zanzibar 1995 na kushika madaraka hadi 2000 akiwa na Rais wake Salmin Almour a.k.a Komandoo. Kabla ya hapo alikuwa PS-Wizara ya Sayansi na Teknologia kuanzia 1990.

  Mwaka 2000 Bilal akiwa CM na Komandoo akiwa Rais wake walianzisha mpango kabambe wa kuitikisha serikali ya Mzee Ben, hadi Komandoo kujitokeza adharani na kutamka kuwa mtu yeyote anayedhani na kufikiria kuizua Zanzibar kujiunga na OIC anatikisa kiberiti, maneno na mienendo ya Komandoo na Bilal iliwa tia hamasa nakuwaadaha sana Wazanzibar walio wengi kiasi cha kujenga matumaini makubwa sana kwa Komandoo mwenyewe na msaidizi wake Dr. Bilal! Ni wakati huo ambapo Bilal na Komandoo pia waliwai kuota ndoto ya kupinda katiba ya Zanzibar hili kumuongezea Komandoo muda.

  Wakidai muda zaidi kwa ajili ya Zanziabar huru zaidi wakijifanya miaka kumi haikuwa tosha na pia walifikia hatua ya kujidai kuwa wakipata nafasi watabadili mfumo wa Muungano hili Zanzibar iwe huru zaidi hisiingiliwe na Serikali ya Muungano wanapotaka kufanya mambo yao ya kimataifa, Komandoo na Bilal waliendelea kujinasibu na hata pale mkakati wa kubadili katiba ulipo kwama Komandoo alitamka dhahiri kuwa Rais wa Zanzibar atakuwa Dr. Bilal iwe hisiwe na kuwa lengo kuu ni kubadili aina ya muungano ili Zanzibar ielekee OIC, hayo maneno yalifurahisha sana wengi wa Wazanzibari na kuendelea kuweka matumaini yao yote juu ya Dr. Bilal; Katika ile inayoitwa Zanzibar special CCM committe mchuano wa kura za Urais wa zanzibar ulikuwa ni kama ifuatavyo (Komandoo akiwa ndio Mwenyekiti): -

  1. Dr. Mohammed Ghalibu Bilal kura 44 (60%)
  2. Abdisalaam Issa Khatibu kura 13 (18%)
  3. Amani Abeid Karume kura 9 (12%)
  4. Kura zilizo aribika 8 (10%)
  Jumla ya kura zilikuwa 74. Ni baada ya CC-CCM kubadili hayo matumaini makubwa ya Wazanzibar hasa Wapemba juu ya Dr. Bilal na kumrejesha Karume kama mgombe wa Urais wa Zanzibar kwa ticket ya CCM ndipo Dr. Bilal na Maalimu Seif walipofanya muungano husio rasmi na kuperekea Wapemba kupiga kura za pamoja kumpinga Amani Karume wakimnadi kuwa hawezi kuleta mabadiliko ambayo Wazanzibar wanayataka na kuwa ni kibaraka wa Wabara, huu ndio uchaguzi ulioleta kinachoitwa na wapemba kama machafuko ya Zanzibar, ni vurugu zilizo asisiwa na matumani ya Bilal na Maalimu Seif wakiwadanganya Wazanzibar kuwa ama Seif au Bilal mmoja wao ndio lulu na matumaini ya Zanzibar na kuwa watakapo ingia madarakani OIC ni dakika chache tu! Dr. Bilal na Seif tokea hapo mwaka 2000 walipo chochea kuuwawa kwa Wazanzibari wenzao waliendele kuingia katika chaguzi bila kufua dafu; Dr. Bilal akiomba Urais wa zanzibar kupitia CCM na kuchujwa na Seif akiomba kwa CUF na kushindwa katika Uchaguzi kwa kile ambacho wengi tuna amini kuwa mara zote alikuwa anaibiwa kura.

  Maskini Wazanzibar kumbe Seif na Bilal si lolote walikuwa wanatafuta madaraka na shibe ya tumbo zao! Tuliamini wakipata nafasi kuna jipya! Wapo leo na mbona wamefunga midomo yao, wote wamepewa nafasi na Kikwete kwa makusudi kabisa! Mbona Dr. Bilal alipoapishwa tu alikimbia kula raha Mbuga za serengeti na kusaka na rumba USA? hayo ndio matumaini makubwa aliyowajengea wazanzibar juu yake?

  Kumbe muda wote Wazanzibar waliweka matumaini yao juu ya watu wawili wanafki na wenyewe tamaa ya madaraka kiasi cha kuperekea kuuwawa kwa vijana wengi tu wakipemba na wengine mpaka leo wamezamia UK.

  Tokea kupata nafasi ya Makamu wa Rais wa Muungano sijamsikia akiongelea tena OIC wala kubadili aina ya mfumo wa Muungano amefunga mdomo maana kishapata madaraka na hicho ndio kilikuwa shida yake.

  Ukitaja wanafki waliowai kuiadaha Zanzibar, wenye tamaa na uchu wa madaraka, ukimtaja Maalimu seif husimsahau na Dr. Mohammed Ghalib Bilal.
   
 2. B

  Bonny Makene Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Arafat, hoja zisizokuwa na mashiko hazina maana yioyote hapa. Umeandika makala ndefu umelinganisha viongozi wanaotokea Zanzibar ambao hawajawahi kufanana kwa hulka wala matendo. La muhimu nililolipata kwako ni kutafuta kutangaza uongo kwa lengo unalolijua, Dk Bilal ambaye nahusika naye hajawahi kutalii USA kama ulivyosema wala hajawahi kupoteza muda wake mbugani kama si ratiba za yeye kama kiongozi. Kumbuka Dk Bilal ni kiongozi wa Jamhuri ya Muungano hivyo yeye hayupo kwa ajili ya Zanzibar pekee bali kwa nchi nzima. Kitendo chochote cha kutaka kumtenga kiongozi huyu na Tanzania kwa msingi wa Uzanzibar utakuwa unaturudisha nyuma ambako hatutarudi yaani kumenya taifa letu ambalo lina mshikamano na umoja uliotukuka. Lakini kwa kuwa una lengo lako lililojificha katika makala yako nitaendelea kuja kukujibu katika mjadala wako huu na hatutakuacha kuudanganya umma. Nitasema kweli daima fitna kwangu ni mwiko.
   
 3. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama kuna mtu anamchukia Maalim Seif na kwamba hawajapata kushirikiana kwa lolote ni Dr. Muhammed Gharib Bilal.

  Hata sasa, kama kuna mtu hapendi Maalim Seif kuwa Serikalini au SUK yenyewe, mmoja ni Dr. Muhammed Gharib Bilal.

  Hapa wala sizungumzii habari za hadaa ya kila mmoja wao kama unavyodai.
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Makene Bilali ni Baba yako au Babu yako,sasa serengeti si alienda kutalii unakataa nini,na USA si alenda kwani uwongo????mimi si mzanzibar na sipajui huko lakini alienda,kwan jk alipobembea jamaika watz tulisemaje??na tunasemaje????hadi sasa hapa jf anaitwa mtalii,
   
 5. H

  HARD TALK Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Jul 10, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UTETEZI WA MASLAHI YA KICHAMA AU MASLAH BINAFSI NI ALAMA YA UBINAFSI AMBAO UNAWEZA KULITENGA TAIFA HILI AU KULIACHA KTK UJINGA KUTOKANA NA HUO UBINAFS.UTAIFA KWANZA KAMA KUNA UKWELI JUU YA ALICHOSEMA ARAFAT BASI ASHUKURIWE KIKWETE! LAKINI UONGO KTK HOJA HYO NI CHANGAMOTO INAYOTAKIWA KUCHOMWA MOTO! Labda hapo 2najifunza nini kutoka dr bilali principal alyepta wa udom zaid ya siasa chafu!
   
 6. B

  BondJamesBond Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wazanzibari wanaendelea kukejeliwa wanapotaka kujitenga....wabara wako bize na kusapoti mambo haya

  [​IMG]
   
 7. B

  Bonny Makene Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red, ndugu yangu jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Dk Bilal si kiongozi mbabaishaji ama mwenye kujenga chuki, ni kiongozi mwenye mapenzi mema na watu na ndio sababu amebaki kuwa kipenzi cha wengi si tu katika Zanzibar, Tanzania bali popote alipopata kuishi. Kwa msingi huo, utofauti wa yeye na Maalim Seif unabaki katika vyama vyao vya siasa tu lakini wanaunganishwa kwanza na Uzanziba na pia Utanzania. Si vema sana kutangaza chuki kwa watu ambao hawajakutuma kuwatangaza kuwa wanachukiana. Labda wewe ndiye unaowachukia hao wote wawili na unataka kuweka chuki zako kwa kutumia majina ya viongozi hawa.
   
 8. B

  Bonny Makene Member

  #8
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nadhani hoja hii mmejipanga kutafuta jambo, kwanza mlianza na Makamu kwenda USA kutalii sasa mnabadilika. Kama ingekuwa ni kwenda USA nisingeingia kukujibu nimetoa majibu pale mlipopotosha safari ile ya kuiwakilisha Tanzania UNAIDS na utalii. Pili nimezungumzia safari ya Dk mbugani Serengeti, hivi ulitaka aende Bahama, ama yeye kama kiongozi wa kitaifa anayemsaidia Rais unataka kumjengea mipaka ya yeye aende wapi ndani ya Tanzania. Akili yako inakutuma kuwa kila mtu akienda mbugani kazi yake ni kutalii? Tambua kiongozi wa kitaifa aina ya Dk Bilal si mtu anayesubiri majibu ya hoja mezani, kiongozi huyu alienda huko kwa lengo la kutafuta ukweli kuhusu barabara inayotakiwa kujengwa ambayo imekuwa kwa kipindi sasa na taarifa za wanaharakati wanaotumiwa kwa maslahi ya mataifa ya nje na sio ya Tanzania. Sikushangaa kusikia alikwenda kutalii huko Serengeti kwa kuwa katika zama hizi za siasa zisizotathmini namna njema ya kuendeleza nchi yetu kila jambo linageuzwa siasa kwa makusudi ili kutoa taswira hasi kwa viongozi wa wananchi dhidi ya wananchi wao. Bado naamini kama huu muelewa nimekujibu lakini kama una agenda nyingine ambayo naamini unayo ni bora uilete hapa ili tuijadili hiyo.
   
 9. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja. Ukisoma vema kisa cha rais wa Zanzibar kutolewa kilazima mwaka 1984 utagundua kisa ni Seif. Ukisoma kisa cha Wazanzibari wengi kufa 2001 kisa ni Seif. Ukisoma vema juu ya watu hawa wawili wala hupati taabu kukubaliana na mwandishi wa makala hii. Ila kuna wengine lazima wataipinga sana kwa kuwa wao ni wachumia tumbo. Watu walianza kuajiriwa na makampuni ya mafisadi ili watumie kalamu zao kuwatetea. Kisha wamepewa nafasi serikalini kuendelea kutumia nafasi zao. Watu hawa kamwe hawawezi kuusimamia ukweli. Daima watasimamia maslahi yao. Ndivyo tulivyo wanadamu.
  Ukweli utabaki kuwa ukweli hata kama utachukiwa kwa kiasi gani. Seif na Bilal ni zaidi ya wanafiki. Wanawahadaa Wazanzibari kwa maslahi yao binafsi.
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  then huyu mzee sio mwanasiasa, hajui siasa kutwa kuzunguka na wake zake!
   
 11. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Yaani bado leo hii kuna watu mnazungumzia Uzanzibar? Yaani hamtambui kuwa nchi kubwa zinaungana ili kukuza uchumi? Mkishaupata Uzanzibar kitakachofuata kutafuta Upemba na Uunguja ama nini? I think Mwalimu was right hoja hii inawauma sana wale waliotaka kuvunjika kwa muungano na wanaowaona viongozi hawa bado wanahubiri umoja. Muungano Daima na NSSF ndilo shirika bora kwa maslahi ya wafanyakazi. Ukweli ndio huo
   
 12. M

  MVUA GAMBA Senior Member

  #12
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mod Naomba nitangulize samahani usije nipa Ban, hIVI HUYU JAMAA ALITAKA Dokta atembee naye na aache wake zake? Hizi ni siasa za majitaka kabisa
   
 13. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Umedandia hoja na kuongea yasiyomo. Nani kakwambia tunahubiri Uzanzibari hapa? Usikurupuke kuchangia jambo kama hulielewi mantiki yake.
   
 14. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Umeajiriwa kwa kazi hiyo. Ndiyo inakuweka mjini.
   
 15. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Sikuwahi kufikiri kama huyu ndugu Bilal anatabia kama za bwana Seif.
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wewe ndio humjui Bilali.

  Kama kuna kiongozi mbaguzi mwenye kuweka mbele undugu na ubaguzi kama huyu jamaa. Kila anapoenda anaweka jamaa zake na ndugu zake wa karibu. Huyu ndio kiongozi wa wale waliokuwa wakipinga SUK kwa kigezo eti itaharibu dhana ya mapinduzi daima. Yeye na Shamhuna ndio waliokuwa viongozi wa waasi wa kupinga SUK kwa kuhofia maslahi yao yataharibika.
   
 17. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  siri ya muungano hii hapa

  swala la muungano huu wetu linatutafuna sana......

  nimesoma pdf hii toka CIA nimejua kuwa muungano ni batili kabisa.kweli nyerere alimzidi karume ujanja

  http://www.foia.cia.gov/CPE/ESAU/esau-28.pdf
   
 18. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  Punguza jazba kijana mada hii naamini ina lengo la kutibua Muungano na sie huku bara tutaulinda kwa nguvu zote na rais ajaye Membe anafahamu hivyo kwa hiyo hata mkitaka kuwachanganya hao viongozi mkidhani wana fikra finyu kuhusu muungano kamwe hamuwezi kuwabadili Tanzania itabaki milele. Viva Tanzania Viva
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Ongelea hoja za Msingi; Dr. Mbona kalala yale matumaini tuliompa yapo wapo? Mbona alituaminisha wakati wa Komandoo kuwa wanaweza kubadili aina ya Muungano ili Zanzibar ijiunge na OIC mbona Dr kimia sasa nini kimemsibu?
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kwanini huzumzii habari zao za kuwa adaha Wazanzibari kuwa wakipata nafasi wanaweza kuleta mabadiliko, mbona walijenga matumani makubwa sana juu yao na sasa wamepata nafasi hamna wanachofanya? Walitafuta nafasi kwa udi na uvumba wamepata sasa mbona hamna wanacho fanya?

  Kama hii ndio aina ya wanasiasa tuliona hauoni wananchni tunapotezewa muda bure na watu Wanafki ambao wanatumia hila kutimiza malengo yao ya kisiasa?
   
Loading...