Viongozi wetu wamekuwa wakialikwa Uturuki kila siku, Raisi wa Zanzibar amerudi wiki iliyopita tu kutoka Uturuki na Makamu wa raisi alikuwa anasubiri ndege irudi na yeye kuchukua ndege kwenda Uturuki je ni kitu gani cha kimaendeleo ambacho hawa marafikizetu wameshidwa kumwambia raisi wa zanzibar mpaka makamu anende ndani ya wiki moja tu!. Kuna mambo gani ya maendeleo yanaletwa na hawa jamaa na kama ni urafiki tu basi tuwe makini kusafiri kila siku!!!. Ninge penda kama ni kwenda kuongea na wafanya biashara lakini kama ni kupiga porojo za mapenzi hakuna sababu ya msingi ya kuwa na safari mbili za uturuki kwenye wiki moja!!!!