Mauaji ya Kutisha Tarime

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
6,148
7,002
Jamani kumejitokeza Mtu/ kikundi cha watu Wilayani Tarime kinachoua watu katika hali ya kusshtua na kushangaza sana, mimi binafsi nina taarifa za watu wawili waliouwawa jana na hao wauaji, jambo la kustikitisha ni kwamba wauaji hao tangu wameanza kuua yapata wiki moja sasa bado hawajakamatwa na hivyo kuwafanya wananchi kuwa na hofu kubwa na usalama wao.

Ni wito wangu kwa Jeshi la polisi kuongeza nguvu ya askari wenye utaalamu na Ujasiri kwasababu hali hii sasa inatisha kweli kweli..Polisi wa kanda maalum inaonekana bado hawajaweza kupata ufumbuzi wa mauaji haya...
Mtu mmoja asiyefahamika anatafutwa kwa tuhuma za mauaji Mjini Tarime, mtu huyo ambaye anafanya matukio ya ajabu ya mauaji leo majira saa nne asubuhi amewaua watu wanne katika Kijiji cha Kemakorere. Anafanya mauaji hayo kwa kutumia Bunduki, inasemekana mtu huyo akishaua hachukui kitu chochote bali huua na kutokomea kusikojulikana.

Mtu huyo haijajulikana kama ni mwanamke ama mwanaume kwa kuwa hajapatikana mpaka sasa.

Kamanda wa Polisi Mjini Tarime amethibitisha uwepo wa muuaji na mauaji hayo ambapo watu takriban saba wameshauwawa mpaka sasa.

Mji wa Tarime umejaa taharuki watu hawana amani...

Jeshi la Polisi linahaha mpaka sasa, kwani linafanya msako wa kufa na kupona kumpata mtu huyo....

Source: Morning Star Radio
 
Dah poleni na nyie huko polisi hamuwaogopi, wakija wanajeshi wanafanikiwa ila huwa siku hizi mambo ya siasa, wanapewa kashfa kibao.
 
wakiendelea kuua naomaba cheo cha unaibu IGP kifutwe haraka na waziri husika ajiuzulu maana ni shida tupu hizi
 
kisa cha mauaji ni nini? kama watakuwa wanawaua wachawi acheni waendelee na kazi sasa uchawi tanzania umekithiri kuna haja ya kutafutiwa ufumbuzi.
 
Jamani kumejitokeza Mtu/ kikundi cha watu Wilayani Tarime kinachoua watu katika hali ya kusshtua na kushangaza sana, mimi binafsi nina taarifa za watu wawili waliouwawa jana na hao wauaji, jambo la kustikitisha ni kwamba wauaji hao tangu wameanza kuua yapata wiki moja sasa bado hawajakamatwa na hivyo kuwafanya wananchi kuwa na hofu kubwa na usalama wao.

Ni wito wangu kwa Jeshi la polisi kuongeza nguvu ya askari wenye utaalamu na Ujasiri kwasababu hali hii sasa inatisha kweli kweli..Polisi wa kanda maalum inaonekana bado hawajaweza kupata ufumbuzi wa mauaji haya...

kaka mtu huyu ameanza kuua watu tangu mwezi novemba ktk kijiji cha murito huko nyamongo.
tangu wakati huo alikuwa akienda kijiji hadi kijiji.mimi nakaa ktk kijiji cha muriba kata ya muriba hivyo ninafahamu vizuri maeneo na hata baadhi ya watu waliouawa.,vifuatavyo ni baadhi ya vijiji alivyotekeleza mauaji,murito,bong'eng'e,genkuru,tagare,keisangora na nyamwaga!!!!. mwanzoni mwa mwezi huu police wakawadanganya wananchi kuwa wamemuua huko genkuru kumbe ni umbea mtupu
 
Kama mpaka idadi mnaijua kitu gani kinawashinda(vyombo vya usalama) kuwakamata.
Kwani kujua idadi ya waliouwawa inasaidiaje kuwakamata wauwaji, au we umeelewaje maana waliouwawa hadi hivi sasa wamefikia wanne.
 
kisa cha mauaji ni nini? kama watakuwa wanawaua wachawi acheni waendelee na kazi sasa uchawi tanzania umekithiri kuna haja ya kutafutiwa ufumbuzi.
Nani anamjua mchawi bwana, uchawi haundoki ila njia ya Mungu tu.
 
Mtu aliyedaiwa kuwa ni kichaa auwa watu nane huko Tarime,Mara
Mtu mmoja ambaye hajulikana jina lake anayesadikiwa kuwa ni kichaa huko Wilayani Tarime mkoani Mara anamiliki silaha adaiwa kuuwa watu nane mpaka sasa polisi wazibitisha.source clouds radio
 
Which is which...Geita na Musoma ni maeneo(Mikoa) tofauti kabisa.
 
Habari zingine utata kweli, hivi kichaa anaruhusiwa kumiliki silaha kama bunduki!
 
Mtu aliyedaiwa kuwa ni kichaa auwa watu nane huko Tarime,Mara
Mtu mmoja ambaye hajulikana jina lake anayesadikiwa kuwa ni kichaa huko Wilayani Tarime mkoani Mara anamiliki silaha adaiwa kuuwa watu nane mpaka sasa polisi wazibitisha.source clouds radio

Heading ni Geita na humu ndani ndo hivyo. Tulia na uandike vizuri ili ueleweka mkuu.
 
Mtu aliyedaiwa kuwa ni kichaa auwa watu nane huko Tarime,Mara
Mtu mmoja ambaye hajulikana jina lake anayesadikiwa kuwa ni kichaa huko Wilayani Tarime mkoani Mara anamiliki silaha adaiwa kuuwa watu nane mpaka sasa polisi wazibitisha.source clouds radio
Heading ya uongo content ni ukweli hata mimi nimeipata toka tarime.
 
Habari zingine utata kweli, hivi kichaa anaruhusiwa kumiliki silaha kama bunduki!

Si ndio nashangaa....eeh Mwenyezi Mungu tuepushe na 'vichaa' waliomilikishwa silaha....manake kumbe mbali ya ajali, tunaweza kumiminiwa risasi barabarani na 'vichaa'....
 
Jamani kumejitokeza Mtu/ kikundi cha watu Wilayani Tarime kinachoua watu katika hali ya kusshtua na kushangaza sana, mimi binafsi nina taarifa za watu wawili waliouwawa jana na hao wauaji, jambo la kustikitisha ni kwamba wauaji hao tangu wameanza kuua yapata wiki moja sasa bado hawajakamatwa na hivyo kuwafanya wananchi kuwa na hofu kubwa na usalama wao.

Ni wito wangu kwa Jeshi la polisi kuongeza nguvu ya askari wenye utaalamu na Ujasiri kwasababu hali hii sasa inatisha kweli kweli..Polisi wa kanda maalum inaonekana bado hawajaweza kupata ufumbuzi wa mauaji haya...

Bila kupiga marufuku Uganga wa tunguri msitegemee mauaji kuisha, hao wauaji hasa wanaokata vichwa wanawake wanatumwa na waganga wa kienyeji, hata serikali inajua lakini hawachukui hatua. Mimi binafsi nauchukia sana mkoa wa Mara kwa matukio yake ya Bagdad
 
Mmoja wa wahanga wa mtu huyu Katili ni Mhandisi wa Ujenzi Mwasi Matiko kwa kweli ni kitu cha ajabu sana ni mhimu kwa serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wauaji kama hawa hata kwa kuwanyonga hadharani...
 
Nimetoka asubuhi tarime kuja huku nyamongo nimepata taarifa kuwa wamemkamata huyo muuaji yaani inatisha
 
Back
Top Bottom