Mtu mmoja asiyefahamika anatafutwa kwa tuhuma za mauaji Mjini Tarime, mtu huyo ambaye anafanya matukio ya ajabu ya mauaji leo majira saa nne asubuhi amewaua watu wanne katika Kijiji cha Kemakorere. Anafanya mauaji hayo kwa kutumia Bunduki, inasemekana mtu huyo akishaua hachukui kitu chochote bali huua na kutokomea kusikojulikana.
Mtu huyo haijajulikana kama ni mwanamke ama mwanaume kwa kuwa hajapatikana mpaka sasa.
Kamanda wa Polisi Mjini Tarime amethibitisha uwepo wa muuaji na mauaji hayo ambapo watu takriban saba wameshauwawa mpaka sasa.
Mji wa Tarime umejaa taharuki watu hawana amani...
Jeshi la Polisi linahaha mpaka sasa, kwani linafanya msako wa kufa na kupona kumpata mtu huyo....
Source: Morning Star Radio