Rushwa ni chanzo cha mauaji Tarime

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,527
Katika wilaya ya Tarime rushwa imekithiri sana, matajiri wamekuwa wakipoka haki za masikini waziwazi, vyombo vya utoaji haki vimekuwa vikikandamiza haki za wasio na pesa waziwazi, ukiishi Tarime kama huna pesa kuwa mpole maana huku haki yako inapokwa waziwazi tena ukiwa unaona.

Tarime mtu anaweza kukunyang'anya kiwanja chako ambacho unakimiliki halali na usimfanye chochote, ukikimbilia huko ukaishia ukawa kesi wewe na habari zako zikawa zimeishia hapo.

Kuna kesi nyingi sana za mauaji zinafanywa na watu wenye "ukwasi" lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa, matajiri wengi wa Tarime mikono yao inanuka damu za watu na hakuna hata mmoja aliyewahi kufungwa, wanaishia tu kukamatwa baada ya siku chache wanakuwa huru, hii imezoeleka miongoni mwa wanatarime.

Ukitembelea maeneo mengi ya Tarime kama vile Tarime mjini, Sirari, Nyamongo mauaji mengi yamefanywa na hakuna mtu aliyewahi kuwaajibishwa, wauaji wote hurudi mtaani na kuendelea kutamba, huku Tarime ukishindana na kigogo kufukuzia mchepuko ukamshinda mbinu anakumaliza tena mchana kweupe na baada ya muda unamuona mtaani akiwa huru.

Takukuru na TISS ichunguzeni Tarime vinginevyo mauaji haya yataendelea kila siku endapo wahusika watakuwa hawachukuliwi hatua.
 
HOME SWEET HOME

TARIME NI WILAYA YENYE MAENDELEO SANA, NI WILAYA CHACHE SANA NCHINI ZINAZOWEZA SIMAMA NA TARIME KIMAENDELEO.

VIONGOZI FUATILIENI HAYO KUEPUSHA UONEVU NA MAUAJI
 
Back
Top Bottom