Ibada za kutakasa ardhi/makazi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,904
Tuendelee na mtiririko wa mada zetu.

Kama kuna kitu kinapokea uchafu na najisi za kila aina basi maji na ardhi vinaongoza...lakini leo ningependa nijikite kwenye ardhi pekee kwakuwa ndio makazi yetu yalipo.

Ardhi inanajisiwa kwa kila namna kuanzia ukatili wa kutoa roho zisizo na hatia mpaka kuzikiwa wafu wenye kila aina ya ugonjwa...hata kama ni mzoga wa mnyama huachwa na kuozea juu ya ardhi.

Kabla hatujaupokea na kuutukuza uzungu mababu wa mababu zetu walifanya ibada za kila mwaka za kutakasa ardhi kuiondolea mabaya mabalaa na nuksi zote na kwakweli hili lilifanya kazi.

Mambo yamebadilika hatuna tena hizi mila hatuna tena hizi tamaduni na desturi za kutakasa ardhi iliyojeruhiwa matendo ya binadamu lakini basi tusisahau kufanya ibada kwa imani zetu za sasa kutakasa makazi yetu mapya na hata ujenzi ikibidi.

Kuna habari nyingi za watu kukutana na mambo ya ajabu ajabu mara wahamiapo kwenye makazi yao mapya au hata kwenye kutaka kuendelea na ujenzi au ukarabati.

Dunia imeharibika watu wamekuwa wengi lakini binadamu wanazidi kupungua wivu husuda kijicho roho ya kwanini vimewafanya watu Wafanye mambo ya ajabu kwenye ardhi makazi ya wengine.

Tuna viongozi wa dini zote kwa imani zetu tunaowaamini si vibaya kuwaalika wakafanya ibada na dua za utakaso kwakuwa huwezi kujua kwa akili zako mwenyewe hiyo sehemu Kilifanyika nini miaka iliyopita. ...hii ni kwa wale waamini.

Ibada na dua hizi husaidia mno kuyakinga makazi yako na nguvu hasi zozote zunazoelekezwa mahali hapo au ambazo tayari zipo
 
Hilo somo gumu kama kiroho huko vizuri.utaona kama masihala,lakini ni jambo zuri sema changamoto iliyopo ni makuhani wetu na.mashekh uwezo wao wa kupambana katika ulimwengu wa roho ni mdogo sana.hawatofautiani na sisi.

wengine wapo kwenye hizo huduma sio kwa wito kama ilivyokuwa kwa Walawi lakini wapo kimaslahi badala ya kuwa wapakwa mafuta wa Bwana.
 
Hilo somo gumu kama kiroho huko vizuri.utaona kama masihala,lakini ni jambo zuri sema changamoto iliyopo ni makuhani wetu na.mashekh uwezo wao wa kupambana katika ulimwengu wa roho ni mdogo sana.hawatofautiani na sisi.wengine wapo kwenye hizo huduma sio kwa wito kama ilivyokuwa kwa Walawi lakini wapo kimaslahi badala ya kuwa wapakwa mafuta wa Bwana.
Kwa hili lazima ujiridhishe na Kiongozi unayemtaka ogopa mno hawa kileo hawa wenye matangazo ya huduma zao kila pembe ya majiji na miji
 
Hilo somo gumu kama kiroho huko vizuri.utaona kama masihala,lakini ni jambo zuri sema changamoto iliyopo ni makuhani wetu na.mashekh uwezo wao wa kupambana katika ulimwengu wa roho ni mdogo sana.hawatofautiani na sisi.wengine wapo kwenye hizo huduma sio kwa wito kama ilivyokuwa kwa Walawi lakini wapo kimaslahi badala ya kuwa wapakwa mafuta wa Bwana.

Kiukweli alichoandika Mshana nakubaliana nacho
Ila sasa hao viongozi wetu Wa kiroho Bob Luse kaandika ukweli kabisa
 
Back
Top Bottom