Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,519
- 870,049
- Thread starter
- #161
CC : chama mpangala
Mkuu nimepata kitu hapa asanteMkuu, unadhani kuwa kiongozi wa dini ndo kuwa na uwezo wa kufanya mambo hayo?? La hasha! Kwa mtazamo wangu na imani yangu naamini kuwa kila binadamu was born divine (hapa naongelea kila roho ya mwanadamu)...
bro mshana jr tatizo walio wengi awajajua kutofautisha uchawi na uchamunguSawa lakini naamini huo sio uchawi
Hama hilo kanisa haraka, watumishi wa zamani walihitaji hela za kuwatunza maana waliishi kanisani hapo hapo bila shughuli nyingine, na kilichofanya waishi kanisani bila shughuli nyingine ilikuwa nikuishi katika utakatifu Ili wawe karibu na Mungu muda wote na walifanikiwa kweli maana waliombea Nchi zao,Tarakilishi watumishi wa zamani ndo walitumia sadaka kadri MUNGU alivyoelekeza,walio wengi ni kujitajirisha tu na majumba na magari,kuna mtumishi mmoja huwa anapiga kabisa simu,anakwambia nahitaji hela nimlipie mwanangu ada naomba unisaidie ndo iwe sadaka yako,jamani ni sawa hii.?yani mtu unakwazika sana.unakuwa mzito hata kwenda kwenye ibada maana utakutana na huyo mtumishi,na alikuomba hela haujampa.
Bwana Yesu Kristo alimaliza yote pale msalabani. Mwanadamu anachotakiwa kufanya Ni KUOKOKA tu.Hilo somo gumu kama kiroho huko vizuri.utaona kama masihala,lakini ni jambo zuri sema changamoto iliyopo ni makuhani wetu na.mashekh uwezo wao wa kupambana katika ulimwengu wa roho ni mdogo sana.hawatofautiani na sisi.wengine wapo kwenye hizo huduma sio kwa wito kama ilivyokuwa kwa Walawi lakini wapo kimaslahi badala ya kuwa wapakwa mafuta wa Bwana.
Asante Sana Mshana JrUkiomba toba unamruhusu Mungu aingilie kati awatoe hayo madudu na aingie mwenyewe.
Katika toba utukufu wa Mungu unashuka; katik toba Mungu anakupigania; katika toba Mungu ana toa uhalali wa shetan na anakaa yeye.
Katika toba unapata ulinzi.
Toba ni kujishusha mbele za Mungu.
. kwa
Nakuunga mkono kwenye upande wa kufanya dua na ibada. Kwa mwenye imani, kuanza makazi mapya kwa kumuomba Mungu ulinzi, amani na baraka ni jambo jema. Ila pia ni muhimu kutokubali hofu au imani zisizo na msingi zitutawale. Nzambe na dua, pamoja na usafi na utunzaji wa mazingira, vina nafasi yake.Tuendelee na mtiririko wa mada zetu.
Kama kuna kitu kinapokea uchafu na najisi za kila aina basi maji na ardhi vinaongoza...lakini leo ningependa nijikite kwenye ardhi pekee kwakuwa ndio makazi yetu yalipo.
Ardhi inanajisiwa kwa kila namna kuanzia ukatili wa kutoa roho zisizo na hatia mpaka kuzikiwa wafu wenye kila aina ya ugonjwa...hata kama ni mzoga wa mnyama huachwa na kuozea juu ya ardhi.
Kabla hatujaupokea na kuutukuza uzungu mababu wa mababu zetu walifanya ibada za kila mwaka za kutakasa ardhi kuiondolea mabaya mabalaa na nuksi zote na kwakweli hili lilifanya kazi.
Mambo yamebadilika hatuna tena hizi mila hatuna tena hizi tamaduni na desturi za kutakasa ardhi iliyojeruhiwa matendo ya binadamu lakini basi tusisahau kufanya ibada kwa imani zetu za sasa kutakasa makazi yetu mapya na hata ujenzi ikibidi.
Kuna habari nyingi za watu kukutana na mambo ya ajabu ajabu mara wahamiapo kwenye makazi yao mapya au hata kwenye kutaka kuendelea na ujenzi au ukarabati.
Dunia imeharibika watu wamekuwa wengi lakini binadamu wanazidi kupungua wivu husuda kijicho roho ya kwanini vimewafanya watu Wafanye mambo ya ajabu kwenye ardhi makazi ya wengine.
Tuna viongozi wa dini zote kwa imani zetu tunaowaamini si vibaya kuwaalika wakafanya ibada na dua za utakaso kwakuwa huwezi kujua kwa akili zako mwenyewe hiyo sehemu Kilifanyika nini miaka iliyopita. ...hii ni kwa wale waamini.
Ibada na dua hizi husaidia mno kuyakinga makazi yako na nguvu hasi zozote zunazoelekezwa mahali hapo au ambazo tayari zipo