Sadio Mané atangaza kustaafu kuichea Senegal

Sadio Mané atangaza kustaafu kuichea Senegal

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,161
Reaction score
17,624
Baada ya Senegal kuondolewa kwa maumivu katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026 kufuatia kufungwa mabao 3-2 na Ubelgiji, nyota wa timu hiyo, Sadio Mané, ametangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa.

Sadio Mané.jpg

Mané (34), alitangaza uamuzi huo kupitia taarifa iliyochapishwa na gazeti la Senegal la Le Quotidien, akihitimisha safari ya miaka 14 akiwa na timu ya taifa ya Senegal.

"Fahamuni kwamba nilijitoa kwa kila kitu kwa ajili ya bendera hii. Nilitoa uwezo wangu wote na siku zote nilipigania taifa letu kwa moyo wangu wote," amesema Mané katika taarifa yake iliyochapishwa na Le Quotidien.

Katika kipindi hicho, Mané ameichezea Senegal mechi 130 na kujijengea heshima kama mmoja wa wachezaji bora kuwahi kuitumikia nchi hiyo. Miongoni mwa mafanikio yake makubwa ni kuiongoza Senegal kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2021.

Nyota huyo wa zamani wa Liverpool, ambaye alianza kujitangaza kisoka akiwa FC Metz nchini Ufaransa, anaondoka kwenye soka la kimataifa akiwa mmoja wa magwiji wakubwa katika historia ya soka la Senegal.
 
Huku kwetu Kuna mchezaji analazimishwa asistaafu wakati hakuna chochote alichoichangia timu yake ya taifa zaidi ya kuididimiza na kuzibia rizki vijana damu changa wapate nafasi.
 
Ametangaza kustaafu lakini itafika siku ataghaili kwa muda ili atumikie taifa.

Mi namtarijia kurudi kikosini muda sahihi ukifika.
Hata Messi alistaafu lakini tunamuona anapigania nchi yake.
 
Hongera kubwa sana kwake,Mane ammekuwa shujaa kulipigania taifa lake kupitia mchezo wa mpira wa miguu.
 
Back
Top Bottom