Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,052
- 17,036
Hapa hata Taifa Stars itapata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia au Wadau mnasemaje?
Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amesema shirikisho hilo litajadili uwezekano wa kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia la mwaka 2030 kutoka timu 48 hadi 64. Amesema pendekezo hilo litajadiliwa na kamati husika baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia la 2026, akisisitiza kuwa mashindano hayo yanapaswa kutoa fursa kwa mataifa mengi zaidi kushiriki.
Infantino amesema kuongeza idadi ya timu kutazipa nchi ndogo motisha ya kuendelea kuimarisha soka lao, huku akieleza kuwa mfumo wa timu 48 uliotumika mwaka 2026 umeonyesha mafanikio makubwa. Kombe la Dunia la 2030 linatarajiwa kufanyika katika nchi sita za mabara matatu, zikiwemo Morocco, Hispania, Ureno, Uruguay, Argentina na Paraguay.
Hata hivyo, pendekezo hilo limeibua mjadala, huku Rais wa UEFA, Aleksander Čeferin, na Rais wa CONCACAF, Victor Montagliani, wakilipinga wakisema linaweza kudhoofisha ushindani wa mashindano na kupunguza umuhimu wa michuano ya kufuzu.
Kwa upande mwingine, viongozi wa soka wa Amerika Kusini, akiwemo Rais wa CONMEBOL Alejandro Domínguez, wanaunga mkono wazo hilo wakiamini litatoa nafasi kwa mataifa mengi zaidi kushiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia.