"Sisi Tunakula Sadaka, Maisha Yetu ni Sadaka”
Mtumishi wa Mungu Mchungaji Victoria Joseph wa Life Center International Bible College pamoja na wengine wamesema kuwa wao kama viongozi wa dini, endapo amani itatoweka kutokana na kelele za mitandaoni, watakosa sadaka.
Wakizungumza na waandishi wa habari, viongozi hao wamewahimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025 kwa maslahi mapana ya nchi, huku wakikemea vikali wale wote wanaotaka kuvuruga amani kwa sababu zao...