Rais wa Djibouti, Ismael Omar Guelleh, ameshinda tena uchaguzi kwa asilimia 97.8 ya kura, na hivyo kujihakikishia muhula wa sita madarakani unaoongeza utawala wake kufikia miaka 27.
Katika uchaguzi huo uliofanyika Aprili 10, 2026, alikabiliana na mgombea mmoja wa upinzani, Mohamed Samatar, huku vyama viwili vikuu vya upinzani vikisusia uchaguzi tangu Mwaka 2016 vikidai kukosekana kwa usawa katika mamlaka za uchaguzi. Ushiriki wa wapiga kura ulikuwa 80.4%