CCM nao kufanya Mkutano Jangwani jijini Dar Jumamosi hii 09-June-2012.....

Watanzania hawadanganyiki wanataka vitendo ccm haiwezi kuwaambia wananchi kila cku maisha bora kwa kila mtanzania wakati maisha magumu kila kukicha.Na wataenda kuchukua hizo kanga na tsh 5000 zao kwani watu wanashida lkn mwisho wao umefika hakuna binadamu wa tanzania asiyeifahamu ccm kwa hiyo hawahitaji kuwashawishi watu kwa maandamano na mikutano bali watekeleze ahadi zao za maisha bora kwa kila mtanzania.
 
Tunaomba mfike kwa wingi wakaazi wa dar,ubwabwa utakuwepo pia chama kimeandaa kofia kanga na t shirts za bure!
 
Yule mhamasishaji wa CDM alifanikisha sana mkutano. Nawashauri CCM wasimsahau Lusinde kwa shughuli hiyo.
 
Mustakbali wa Taifa? labda watajikita kujibu hoja za CHADEMA, wakidhani watanzania hawaoni!
Hapo wategemee kusikia Mwitikio wa Nguvu ya Umma! Peopleeeeeezzzzzzzz!!!!!!!!!!
 
Utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na watazungumzia mustakabali wa taifa.
Source: tbc1

Hata mimi nimesikia kitu hicho kutoka kwa mzee mmoja huwa wanakodi maroli yake kubeba wananchi kwenda kwenye mikutano yao, ila wanadai mpaka jana JK alikuwa haja confirm kuwepo.
 
Hivi leo kuna mtanzania asiyejua mstakbar wa taifa hili chini ya uongozi wa ccm?.For sure Tanzania chini ya ccm ni kuelekea kuzimu maana all indicators(muungano,wizi wa madini,polisi mabomu na risasi zidi ya wananchi,religious extremisms na CCM) leading us to a total collapse as a nation.
 
siku chadema walipofanya mkutano tbccm walituonyesha mechi ya kirafiki naomba siku hiyo wasiache kutuonyesha mechi ya kirafiki hatakama ni marudio....CCM wanacheza ngoma ya chadema wakitoka dar waende kusini
 

Kitu cha kuangalia kama nembo ya huo Mkutano

* Njano na kijani Uwanja Mzima

- T-Shirt za Njano;
- Khanga za Njano & Kijani;
- Vilemba vya Njano na Kijani;
- Kofia za Kijani au Njano;
- Malori ya Mchanga au Vicoaster vyabeba watu kwa nguvu toka Vingunguti Magurumbasi au toka Nyuma
ya Sunguratex.
- Kama Mama ntilie hawapo basi kuna masinia ya Wali, Maharagwe na Nyama ya Ng'ombe Saafi na Maji.


HAPO MKUTANO NI MTAMU HASWA WENGI HATUSIKII, USINGIZI MNONO UNAITA - NI KAMA TUMEENDA SHORT SHOPPING KWENYE MALL.
 
Nina bahati mbaya leo na hizi posts za hawa jamaa naona kikao cha baraza wameona ndo njia mbadala,imeandikwa katika profesio ya Misa HAKIKA MNAJUA MTAKUFA.:laugh:
 
dah ... wanaopenda ubwabwa haya tena .... nafasi ndiyo hii
 
nasikitika kuona ccm imegeuka kuwa chama cha COPY & PASTE hawana ubunifu tena wa kufanya siasa. Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza
 
Back
Top Bottom