Hii ndio tatu bora ya vyama vya upinzani ambavyo vilipata misukosuko mikubwa kutoka katika vyombo vya dola

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,880
12,320
Habari zenu wana JF wenzangu.

Ndugu zangu, najua hapa JF tuna vijana wengi ambao walianza kufuatilia na kujiunga na mambo ya kisiasa miaka ya 2010, 2015, 2020 hadi leo 2023.

Vijana hao ambao wengi wao ni Chadema, wakifuatiwa kwa mbali na ACT Wazalendo, wanaamini kwamba vyama hivyo viwili ndio vyama pekee vilivyowahi kukumbana na misuko suko mingi kutoka katika vyombo vya dola toka mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa nchini kwetu.

Sasa vijana hawa kwa kweli hatuwalaumu kwa sababu hawajui, na hawakuwahi kujua misuko suko waliyowahi kukumbana nayo wapambanaji wa vyama vingine na vyama vyao kwa ujumla.

Ndio maana mimi niliekulia katika mageuzi na kushuhudia misuko suko mbali mbali ya kisiasa kati ya vyombo vyetu vya dola na vyama hivyo nimeamua kuja kutoa darasa kwa wadogo zang wa leo wasijua hili wala lile kuhusu siasa zetu na mapambano yake. List ya tatu bora ya vyama hivyo vilivyowahi kukumbana na misuko suko hiyo iko hapo chini.

3. NCCR Mageuzi - Chama hiki ndio kilikuwa chama kikuu cha kwanza cha upinzani kukumbana na mikiki mikiki mikubwa kutoka katika vyombo vya dola tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe nchini kwetu.

Nyumbani kwetu chama hiki kilikuwa kama vile ndio dini yetu. Kuanzia kwa baba mwenye nyumba, mama, sisi watoto hadi na mfanyakazi wetu wa ndani tulikuwa NCCR Mageuzi.

Kwa wale ambao walikuwa wakifuatilia siasa zetu miaka ya 90 bila shaka wanalifahamu hili. Mikiki mikiki kati ya dola na chama hicho ilikuwa mingi hadi kupelekea wazee wa suit nyeusi kupenyeza watu wao katika chama hicho, ambao nao walifanya kazi yao kwa ustadi mkubwa hadi kupelekea chama hicho kusambaratika vibaya before hata ndoto zao za kushika nchi mwaka 2000 hazijatimia.

Pamoja na yote, lakini kabla ya kusambaratika kwa namna fulani chama hicho kilikuwa kinapewa muda fulani wa kufanya siasa zake, mikutano yake na kutangaza sera zake bila bughuza yoyote.

2. Chadema - Chama hiki ambacho naweza kusema ndio chama kikuu cha upinzani kwa sasa kilianza kukumbana na misuko suko mbali mbali mnamo miaka 13 au zaidi iliyopita.

Misuko suko iliyokumbana nayo Chadema ni pamoja na wafuasi wao kupewa vilema vya kudumu baada ya mapambano mbali mbali na vyombo vya dola, wafuasi wengine pamoja na viongozi wa chama hicho kama kina Mbowe kufungwa, maandamano kadhaa kuzuiliwa nk.

Ila pamoja na yote hayo, lakini chama hicho bado kilikuwa kinapewa muda wa kufanya siasa zake huko mwembe yanga Tandika na kutangaza list of shem bila bughuza yoyote kutoka serikalini.

Leo hii chama hicho kimekuwa na ushirikiano mkubwa na chama tawala kupitia maridhiano yao ya kisiasa ambayo yamepelekea viongozi wa vyama hivyo viwili (CCM & CDM) kuwa kama ndugu.

1. CUF - Chama hiki ambacho kiliwahi kuwa chama kikuu cha upinzani kwa muda wa miaka 10. Ndio chama kilichowahi kukumbana na mikiki mikiki mingi kuliko chama kingine chochote kile. Yani ile mikiki mikiki ya kufa mtu.

Chama hiki naweza kusema enzi za utawala wake kama chama kikuu cha upinzani ndio chama pekee ambacho kilijenga uadui mkubwa sana na vyombo vya dola.

Tofauti na vyama vingine ambavyo vilikuwa vinapewa muda wa kufanya siasa zao vizuri, kwa CUF hiyo haijawahi kutokea. Kila mkutano uliofanywa na Cuf lazima ulikumbana na misuko suko ya mabomu ya machozi, haijalishi mkutano huo ni wa amani au vinginevyo.

Yani kila mkutano wa chama hicho ulipofanyika, uchukuliwa tu kama ni wa kuvunja amani. Ndomaana muda mungine ulikuwa unakuta mkutano unafanyika vizuri, lkn ikifika bado pengine dakika 2 au 1 mkutano uishi ghafla mtaanza kusikia risasi imepigwa juu na hapo hapo wazee wa kazi kuanza kurusha mabomu ya machozi kusambaratisha watu na kuharibu mkutano.

Tena kibaya zaidi chama hichi kilibanwa sehemu zote za muungano i mean Bara na Visiwani. Yani maalim anachezea kichapo zenji na Lipumba anachezea kichapo buguruni au jangwani.

Chama hiki kilionekana kama vile kimeanzishwa kwa lengo la kuharibu amani yetu. Hivyo jitihada zote zilifanyika kuhakikisha hakishiki dola, wala kuwa na wabunge wengi bungeni.

Katika kuonesha uadui mkubwa uliyopo kati ya dola na chama hicho mwaka 2001 kila mkongwe anafahamu kilichotokea kule Zenji afu baadae likatengenezwa chezo la mapanga ambalo lilichangia kwa kiasi kikubwa kukisambaratisha chama hicho.

Kwahiyo tunapozungumzia wapambanaji waliopambana haswa na vyombo vya dola, basi vijana wa Cuf wakiongozwa na msemo wao wa jino kwa jino ndio waliokuwa mstari wa mbele haswa kupambana hadi ikapelekea wengi wao kuuwawa, kutiwa ulemavu, kufungwa, na wengine kutoroka nchi.

Karibu wakongwe wenzangu, muongeze na nyie yale mnayoyajua.

ACT Wazalendo kimeanzishwa kipindi kizuri. Maana toka kuanzishwa kwake mpaka leo bado hakijakumbana na misuko suko yoyote, japo kiongozi wao anajaribu kutuaminisha kuwa chama chake kinafuatiliwa na vyombo vya dola (sijui kwa lipi)

Kwa ACT Wazalendo kufuatiliwa na vyombo vya dola bado sana. Maybe miaka 20 ijayo, lkn sio leo wala kesho. Nakataa kabisa.
 
Siasa ni sayansi ya mahesabu makubwa sana muda sahihi ndio kigezo kikuu Cha kufanya maamuzi ya mageuzi.

Afrika Kuna unafiki mkubwa sana ukisoma historia mabeberu hawa kuwapa wapinganiaji Uhuru wa Tanganyika kesi za ajabu ajabu kama leo hii chama Cha ccm Kila uchwao ni kuwapa kesi za ajabu vyama vyenye mawazo mbadala
 
Back
Top Bottom