Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Chongolo anaunguruma Dar es Salaam kujibu hoja za Bandari

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,318
24,214
29 Julai 2023
Dar es Salaam, Tanzania

MKUTANO WA KATIBU MKUU WA CCM, KUUTETEA KWA NGUVU MKATABA WA BANDARI

CCM yaanda mkutano uliowakusanya wana CCM kutoka mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam unaoendelea katika viwanja vya Kawe mjini Dar es Salaam

KISHINDO CCM KANDA YA MASHARIKI

Kama kawaida Katibu Mkuu wa chama kongwe dola cha CCM ameongozana na ujumbe wa makada katika kutetea mkataba wa bandari.

Na CCM hivyo imewaleta jukwaani majembe yao tegemezi kutetea mkataba ambao ni komredi Abdallah Hamis Ulega, Atupele Mwakibete, profesa Kitila Mkumbo, mwanasheria mbunge Jerry Slaa, mzee Stephen Masato Wasira a.k.a Tyson, wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa wakiongozwa na komredi Juma Gaddafi, Komredi Mwakitinya, Dr. Msengi, Dr.Fenella Ephraim Mukangara, Nikki wa II, wakuu wa mikoa Adam Malima, Albert Chalamila ...Abbas Tarimba, Songoro Mnyonge, Askofu Gwajima ...

Mjadala kuhusu bandari umekolea moto na huko Bukoba Kagera CHADEMA washangaa kuona haijawahi kutokea CCM kutembea nchi nzima kutetea mradi wa uwekezaji huko nyuma katika awamu za CCM mpya ya ubinafsishaji ya Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli ....

CCM tayari imefanya mikutano ya kikanda kama huu wa Kawe Dar es Salaam kule mjini Mbeya ambako ulikusanya wanaCCM wa mikoa jirani na Mbeya na pia kule kanda ya Kaskazini iliyokusanya mikoa kadhaa...

Leo jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa CCM komredi Daniel Chongolo ... profesa Kitila Mkumbo asifia mijadala mipana inayoendelea kuhusu mkataba wa bandari na hii ni demokrasia anasema mbunge wa Ubungo kada wa zamani wa CHADEMA ...

Hali kwa ujumla kwa wazito jukwaani na katika hadhara ya wanaCCM waliopo uwanjani ni sura za kinyonge, simanzi na za kukata tamaa ... shamrashamra hazipo watu wekosa utulivu wanazunguka zunguka hadi profesa Kitila Mkumbo anawashangaa waliohudhuria mkutano wa leo na kusema haufanana na ule wa kanda ya nyanda za juu kusini Mbeya au ule wa kanda ya kaskazini walioufanya vigogo hawa wa CCM ....
 
100% am sure hawez jibu facts ✔️

Stephen Masato Wasira anaingia kwa kuchukua mic na kutoa mistari kwa freestyle kawimbo waliouimba mwaka 1958 wakiwa chipukizi wa TANU youth league lakini watu hawaelewi.

Wote waliozungumza hadi sasa katika mkutano bado wameshindwa kutetea mkataba labda komredi Daniel Chongolo akifikiwa zamu ya kuzungumza atafanikiwa kushawishi hadhara ya wanaCCM.
 
SALAAM ZA RAIS SAMIA
Daniel Chongolo - Huko alipo Rais Samia amenihakikishia anafuatilia mkutano huu wa CCM Kanda ya Mashariki mwanzo mwisho
 
Mh huyu wanampa WAKATI MGUMU kwa kitu AMBACHO kineleweka. BUNGE haliwezi HATA SIKU MOJA kubariki mkataba usio na maslahi MAZURI kwa Nchi
 
Tatizo sio ujio wa kampuni toka Arabuni.

Tatizo ni vifungu vya kwenye huo mkataba haswa kifungu cha ukomo kutoelezwa kwa uwazi pia shughuli zingine zitakazofanywa na kampuni mbali na bandari hiyo tajwa ya Dar es Salaam.

Pia tulidanganywa ulipita mchujo wa zabuni kwa kampuni 8 tofauti ambazo hazitajwi ila ndani ya mkataba imeandikwa kupitia ziara ya Samia ya Dubai Expo 2020 alipokwenda mwezi March 2022 kwa contradiction kama hizi hata mtu asiye na ufahamu lazima ajenge maswali lukuki.
 
Vuta n'kuvute vyama vya siasa Tanzania kuhusu DP World​

George Njogopa
24.07.202324 Julai 2023
Vyama vya kisiasa nchini Tanzania sasa vimeanza kutumia majukwaa ya wazi na mikutano ya hadhara kuwashawishi wananchi juu ya kile kilichomo kwenye mkataba wa bandari kati ya nchi hiyo na kampuni ya kigeni ya DP World

Karata za vyama vya siasa kugeukia majukwaa ya wazi inakuja wakati wingu nene likiendelea kugubika hatma ya makubaliano ya mkataba huo ambao mjadala wake umegeuka mada inayotupiwa macho kila uchao.

Chama kikuu cha upinzani Chadema kikiwa na viongozi wake wakuu, kimeanza kuwaalika wanaharakati pamoja na vigogo wa sheria na viongozi wa dini, kuuchambua na kuukosoa mkataba huo huku kikizidisha lawama kwa serikali katika kile inachosema kuingia kwenye mikataba mibovu

Hoja zinazotolewa na chama hicho pamoja na wanasheria zinaakisi kile kinachoelezwa kuhusu baadhi ya vipengele kwenye mkataba huo kukosa afya kwa ustawi wa taifa, kama vile wawekezaji kuwa na usemi mkubwa kuhusu bandari za Tanzania.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema taifa linapaswa kuwa na usemi mmoja kupigania maslahi ya taifa na kukikosoa chama tawala CCM katika kile alichosema "kutengeneza mzigo usiobebeka”

Kwa mara ya kwanza mjadala kuhusu mkataba wa DP World umewakaribisha katika meza moja wanasiasa waliowahi kuhitilafiana huko nyuma.

Mwanasiasa wa zamani na aliyewahi kuwa kiongozi wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa alitumia jukwaa hilo hilo kuukosoa mkataba huo huku akiwahimiza wanasiasa wengine kurejea katika meza ya umoja kwa ajili ya kupaza sauti.,

"Tulialika vyama vingine na dakika za mwisho wakajitoa, tukiacha unafiki huu hii nchi haitabomolewa." Alisema mwanasiasa huyo ambae aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

Nacho chama tawala CCM kinazunguka katika maaeneo mbalimbali ya nchi kuunadi mkataba huo na kuweka msimamo wake kikisema kitaendelea kuutetea.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo anayezunguka na makada wake pamoja na maafisa wa serikali wakiwemo mawaziri ndiye anayeongoza ajenda ya kuusemea mkataba huo.

“Hatuna hofu wala shaka na kwamba jambo hili ni utekelezaji wa ilani ya CCM, wanaongaika kulifanya suala la bandari liwe la Samia, wameshindwa kusoma alama za nyakati.Tumewagundua na tumewajua pamoja na njia wanazozitumia,” alisema Chongolo.

Hayo yakiendelea bado haijajulikana nini hatma ya mjadala huo, na kile kinachosubiriwa na wengi ni kuona kwamba hoja za upande upi zitazingatiwa iwapo mjadala huo utafikia tamati.

Serikali ya Tanzania na Dubai ziliingia mkataba Oktoba 25 mwaka jana kwa ajili ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari (IGA).

Bunge limeshapitisha azimio la kuridhia ushirikiano huo kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World inayomilikiwa na Serikali ya Dubai.

Makubaliano hayo yalibainisha maeneo mahususi ya ushirikiano ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandariza bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maeneo ya maegesho na utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Source : DW
 
29 Julai 2023
Dar es Salaam, Tanzania

MKUTANO WA KATIBU MKUU WA CCM, KUUTETEA KWA NGUVU MKATABA WA BANDARI

CCM yaanda mkutano uliowakusanya wana CCM kutoka mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam unaoendelea katika viwanja vya Kawe mjini Dar es Salaam

KISHINDO CCM KANDA YA MASHARIKI

Kama kawaida Katibu Mkuu wa chama kongwe dola cha CCM ameongozana na ujumbe wa makada katika kutetea mkataba wa bandari.

Na CCM hivyo imewaleta jukwaani majembe yao tegemezi kutetea mkataba ambao ni komredi Abdallah Hamis Ulega, Atupele Mwakibete, profesa Kitila Mkumbo, mwanasheria mbunge Jerry Slaa, mzee Stephen Masato Wasira a.k.a Tyson, wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa wakiongozwa na komredi Juma Gaddafi, Komredi Mwakitinya, Dr. Msengi, Dr.Fenella Ephraim Mukangara, Nikki wa II, wakuu wa mikoa Adam Malima, Albert Chalamila ...Abbas Tarimba, Songoro Mnyonge, Askofu Gwajima ...

Mjadala kuhusu bandari umekolea moto na huko Bukoba Kagera CHADEMA washangaa kuona haijawahi kutokea CCM kutembea nchi nzima kutetea mradi wa uwekezaji huko nyuma katika awamu za CCM mpya ya ubinafsishaji ya Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli ....

CCM tayari imefanya mikutano ya kikanda kama huu wa Kawe Dar es Salaam kule mjini Mbeya ambako ulikusanya wanaCCM wa mikoa jirani na Mbeya na pia kule kanda ya Kaskazini iliyokusanya mikoa kadhaa...

Leo jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa CCM komredi Daniel Chongolo ... profesa Kitila Mkumbo asifia mijadala mipana inayoendelea kuhusu mkataba wa bandari na hii ni demokrasia anasema mbunge wa Ubungo kada wa zamani wa CHADEMA ...

Hali kwa ujumla kwa wazito jukwaani na katika hadhara ya wanaCCM waliopo uwanjani ni sura za kinyonge, simanzi na za kukata tamaa ... shamrashamra hazipo watu wekosa utulivu wanazunguka zunguka hadi profesa Kitila Mkumbo anawashangaa waliohudhuria mkutano wa leo na kusema haufanana na ule wa kanda ya nyanda za juu kusini Mbeya au ule wa kanda ya kaskazini walioufanya vigogo hawa wa CCM ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM/Serikali hawana historia nzuri ya mikataba ya kimataifa ,mingi ni ya kimangungo na hatimaye tunakuja kulipa mabilioni ,hata huu wa DP world nao ni wa kimangungo lazima tupigwe NDOIGE.
 
MwanaCCM Chifu Prince Mwaihojo Mwabipile - Awaasa Viongozi wa CCM

Back
Top Bottom