Zuio la usajili wa Polyclinics (Kliniki za Kibingwa) mpya katika mfuko wa bima (NHIF): Waziri Ummy Mwalimu atoe majibu

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
848
1,212
SINTOFAHAMU YA ZUIO LA USAJILI WA POLYCLINICS (KLINIKI ZA KIBINGWA) MPYA KATIKA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF): WAZIRI UMMY MWALIMU ATOE MAJIBU KWA WADAU

Kumekuwa na kilio cha Wadau katika sekta ya afya juu ya zuio la kusajili Vituo vya kutolea huduma maarufu kama Polyclinic na Specialized Polyclinic au Kliniki za Kibingwa katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, ambapo zuio hilo limelenga Kliniki mpya zilizoanza kutoa huduma mwanzoni mwa mwezi Aprili 2022.

Takwimu za Wizara ya Afya zinabainisha kwamba mpaka kufikia mwezi Machi 2022 kulikuwa na jumla ya Kliniki za Kibingwa 299 ambazo ni sawa na asilimia 3.3 tu ya vituo vyote vya kutolea huduma za Afya Nchini.

Ni zaidi ya mwaka umepita bila kuwa na taarifa yeyote rasmi kutoka Wizara ya Afya kuhusu sababu za kutokusajiliwa kwa polyclinics mpya katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kutoa fursa kwa Watanzania kupata huduma bora bila kikwazo chochote, hasa ikizingatiwa Vituo hivyo vinaendeshwa kwa mujibu wa Sera na Miongozo ya Wizara husika, na pia zimekidhi vigezo stahiki.

Kwa mujibu wa chanzo cha Wizara ya Afya, zaidi ya Kliniki za Kibingwa 150 zimekwama kusajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya licha ya Vituo hivyo kukidhi vigezo vyote vilivyoainishwa na Mfuko na kwamba baadhi yake vilishafanyiwa tathmini ya vigezo na kuonekana kuwa na sifa za kusajiliwa ili kuhudumia wanufaika wa Mfuko huo, lakini kinyume na matarajio mchakato huo ulisitishwa bila taarifa yeyote kutoka kwa Mamlaka.

Baadhi ya Wawekezaji na Watoa huduma wamedai kwamba baada ya kukamilisha taratibu zote za maombi ya usajili wa Mfuko waliamua kufuatilia maombi yao kupitia Ofisi za Mfuko na kujulishwa kwamba kuna zuio kutoka Wizara ya Afya juu ya usajili wa Polyclinics katika Mfuko wa Bima ya Afya.

Wadau waliendelea kupaza sauti zao na kudai kwamba wanadhani Wizara ya Afya imeshindwa kutambua juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani kupitia sekta ya afya kwa kuweka zuio bila kutoa taarifa kwa wadau juu ya sababu zake na pengine zuio hilo linalenga kutatua nini, na litadumu kwa muda gani.

Kwa kukizingatia kwamba vituo vinategemea zaidi ya asilimia 70% ya mapato yatokanayo na wanufaika wa Mfumo wa Bima kwa ajili ya uendeshaji, ni wazi kwamba zuio hilo limeathiri kwa kiwango kikubwa uendeshaji wa vituo na kupelekea baadhi yao kusitisha huduma na wengine kuendelea kwa kusuasua.

Ni dhahiri kwamba zuio hili limeathiri uwekezaji na wawekezaji kwa kuwa uwepo wa Bima ya Afya na Uhaba wa huduma za Afya ilikuwa moja ya kivutio vilivyochochea uwekezaji katika sekta hii.

Inatajwa kwamba kiwango cha chini cha gharama za uendeshaji wa polyclinic moja zinakadiriwa kufikia Tsh. Milioni 10 kwa mwezi , ambapo kutokana na kukosekana kwa huduma ya NHIF vituo husika vimekuwa vikihudumia wagonjwa wasiozidi watatu (3) kwa siku licha ya Watanzania wengi kuendelea kupata adha ya msongamano wakati wa kupata huduma katika Vituo vilivyosajiliwa na Mfuko wa Bima ya Afya.

Aidha tathmini imebainisha kwamba katika kipindi chote cha zuio, Polyclinics zimehudumia wagonjwa kwa kiwango cha chini ya ufanisi unaokadiriwa kufikia asilimia 90-97% licha ya kutumia kiasi cha takribani Tsh. Bilioni 18 kwa mwaka kugharamia malipo ya mishahara, kodi ya pango, kodi za kimamlaka na gharama nyingine za uendeshaji, ambapo gharama hii ni nje ya ile iliyotumika kufanya uwekezaji.

Kuendelea kwa zuio hili, inaweza kupelekea takribani Watanzania wasiopungua kumi (10) kwa kila polyclinic kupoteza ajira zao pale ambapo Vituo vitasitisha kutoa huduma, na hivyo kutengeneza ukosefu wa ajira wa takribani watumishi 1500, kiwango ambacho ni kikubwa sana ukizingatia hali ya upatikanaji wa ajira na changamoto zake.

Zaidi, imethibitika kwamba zuio hili linawanyima wanachama wa Mfuko wa NHIF fursa ya kupata huduma bora, za kibingwa , kitendo ambacho ni kinyume na sera na jitihada za serikali kuhakikisha huduma bora zinafikia wananchi.

Ni matumaini yetu kwamba uwepo wa Vituo vingi vya kutolea huduma za Afya Mathalani Kliniki za Kibingwa ambazo zimesajiliwa na Mfuko wa NHIF itakuwa ni fursa kwa Mfuko katika kuboresha huduma kwa wanachama wake, na hivyo kuvutia Makundi mengi zaidi kujiunga, na hatimaye Ukuaji wake.

Uwepo wa huduma bora, na za uhakika kwa Wananchi utasaidia kufanikisha adhma ya Serikali ya kuwa na Bima ya Afya kwa Wote.

Hivyo basi tunatoa wito kwa Wizara ya Afya kuingilia kati ili kunusuru hali hii mbaya, na hivyo kuinua hari na matumaini kwa wawekezaji wazawa, watumishi wa sekta ya afya na wananchi kwa ujumla.
 
Takwimu za Wizara ya Afya zinabainisha kwamba mpaka kufikia mwezi Machi 2022 kulikuwa na jumla ya Kliniki za Kibingwa 299 ambazo ni sawa na asilimia 3.3 tu ya vituo vyote vya kutolea huduma za Afya Nchini.
Ziendelee kuongezeka zaidi ni kweli bado hazitoshi
 
Kwanini hizi Polyclinic hazitaki kutambua umuhimu wa Taaluma zingine kama Pharmacy na Wauguzi. Mamlaka zilinusa harufu ya uchafu uliokuwa ukifanwa na vituo hivi vya afya vitoavyo huduma za kibingwa. Udanganyifu na ukiukwaji wa taratibu katika kujaza fomu za bima kwa mfano, mnatumia MDs, AMO na maafisa Tabibu ila form wanajaza Madaktari bingwa. Hayo madudu yenu ndio yamepelekea mfumo wa bimq ya Taifa kushindwwa kujiendesha kwa kutumia mapato ya ndani.
Siungi mkono zuio, ila nalaani jeuri na kiburi mlichonacho Madaktari linapokuja suala la masuala ya sera za Afya. Ni vyema mkajitafajari ili Boss akija kuwaondolea zuio mnasonga. Ahsanteni sana kwa huduma zenu, zinahitajika nyingi sana bila ila acheni kiburi.
 
Kuendelea kusajili hizo Polyclinic ni kuzidi kuharibu huduma katika hospitali za umma maana madaktari wengi wanatoa huduma chini ya kiwango katika hospitali za umma ili wagonjwa waende kuwafuata huko mitaani na wamekuwa wakishirikiana na wafanyakazi wasio waaminifu wa NHIF kuhujumu mfuko.
 
Ni wajibu wa mamlaka kuhakikisha compliance. Hatuwezi kuzuia kusajili biashara mpya kwa sababu ya malalamiko ya rushwa kwa wafanyabiashara. Ni wajibu wa Serikali kuchukua hatua kwa mtoa huduma anayekiuka miongozo na si kuzuia kusajili wapya.
 
Baadhi ya polyclinic wanajaza fomu za NHIF mara 2 huo ni wizi. Na Wala hawaonyeshi gharama/ bei zilitumika kwa mgonjwa husika

NHIF wana kitengo cha kushughulikia Fraud. Kuna wataalamu ambao wanatakiwa kuhakikisha mfuko unalindwa dhidi ya madai yasiyo halali. Changamoto ni uaminifu katika kazi zao. Inawezekana ni wanufaika.
 
Kuendelea kusajili hizo Polyclinic ni kuzidi kuharibu huduma katika hospitali za umma maana madaktari wengi wanatoa huduma chini ya kiwango katika hospitali za umma ili wagonjwa waende kuwafuata huko mitaani na wamekuwa wakishirikiana na wafanyakazi wasio waaminifu wa NHIF kuhujumu mfuko.
Mfuko unahujumiwa na watumishi wa NHIF kwa njia kadhaa;
1. Sera zinazopelekea kusajili wanachama ambao wengi ni wagonjwa kupitia vifurushi (.https://www.jamiiforums.com/threads/waziri-ummy-mwalimu-wanaokata-bima-ya-afya-wakiwa-wagonjwa-wanatishia-ustahamilivu-wa-mfuko.2047475/)
2. Mfuko kuwekeza fedha katika sekta ya nyumba kupitia Watumishi Housing cooperation. Miradi mingi inasuasua.
3. Kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu kama Benjamin Mkapa Na MOI, ambapo urejeshwaji wa fedha unasuasua.
4. Serikali kuchota fedha za mfuko na kushindwa kurejesha kwa wakati.
5. NHIF kukopesha fedha kwa watumishi wake kwa riba ndogo sana.
6. Baadhi ya watumishi wa mfuko kushirikiana na vituo binafsi kutenda rushwa.
 
Back
Top Bottom