Zuio la mahindi kwenda Kenya tusiwatupie lawama Wakenya. Nchi yao inayo haki kulinda raia wake

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Inashangaza sana kuona watu wanailaumu nchi ya Kenya kuzuia mahindi toka Tanzania kuingizwa nchini humo.

Watu wengi wanailaumu Kenya kana kwamba haina mamlaka ya kulinda raia wake na mipaka yake.

Kama mahindi ya Tanzania au nchi nyingine yamepimwa mamlaka husika za Kenya na kuonekana yana sumu basi ni jukumu la Kenya kulinda afya za raia wake.

Ni jukumu la wataalamu wa Tanzania kutoa elimu namna ya kupambana na hili tatizo linalosababisha mahindi kuzalisha sumu. Sio kuleta visingizio vya kuonewa wivu wa kiuchumi.
 
Inasikitisha kuona wanachadema wanashangilia yanayoendelea baina yetu na majirani zetu Kenya.

Huu ni Ulofa wakupindukia na kukosa Uzalendo wa kupindukia.

Huwezi kumkuta Raia wa Marekani pamoja na tofauti za Kisiasa lakini linapokuja swala lenye maslai ya nchi yao huta kuta kuna vihoja kama huku kwetu.

Haya ni matunda ya siasa mbaya za upinzani kujaza wafuasi wao chuki kwa maslai yao ya kisiasa.

Na kutokana na Ufahamu duni wa Wafuasi bila kutumia Akili wanalipuka kama mazuzu na kuichukia nchi yao na Viongozi wao.

Mfano mzuri ni Ndugu zetu wa Libya. Walijazwa Sumu na wapinzani wa Mh Gaddafi kwamba Gaddafi ni MTU mbaya sana na katili sana. Na walibya kwa kutokutumia Akili hawakujua Ujanja wa wapinzani kwamba wanataka madaraka kupitia wananchi kwa kuwachonganisha na Rais wao je! Leo hawamkumbuki bwana Gaddafi?

Tuache Ujinga wa kisiasa wa kusapoti ujinga wakupindukia wa kishabiki.

Nchi yetu Tanzania ina History kubwa sana juu ya Majirani zetu. Wazee wetu walijitoa sana kupigania Uhuru wa Majirani zetu.

Tulitoa Ardhi Pesa vyakula na majeshi yetu kwenda kusidia nchi zao lakini Leo kutokana na Vizazi vya laana visivyojua history yetu ndio hao wanatumiwa na Mabeberu kutuchafua Watanzania kwa maslai ya mabeberu na kusahau kwamba Fimbo ya Mbali Haiui nyoka.

Tanzania ni nchi kubwa sana. Kenye wafanye wanavyofanya lakini siku zinakuja watakuja kuturamba miguu kutafuta msaada huu uhuni wao ni wamudatu.

Muda utaongea time will Tell. Tanzania itakuwepo na itazidi kuwepo na Mungu Atazidi kututhibitisha mbele ya Maadui zetu kwamba Tanzania niya Mungu na Mungu Anaishi Tanzania.

Natoa with kwa Viongozi wetu kwamba ni Muda wa kujipanga zaidi maana tayari Mungu wetu Amesha wadhihirisha Adui zetu na watajitokeza wengitu wa ndani na Nje ya nchi yetu.

Viongozi wetu ni Muda wa kusimama Imara na kumtegemea Mwenyezi Mungu Zaidi. Tusimbembeleze kila Atakae tufanyia figisu zozote tusonge mbele Mungu wetu Atatuinuliwa Marafiki waaminifu watakao tushika mkono nakutubariki kwa kununua mazao yetu.

Mungu ibariki Tanzania
🙏
 
Biashara za kimataifa hazifanyi kinyama hivyo, huwezi kukurupuka tena kwa nchi unayoitegemea kiuchumi ukata waya kama vile haitakuathiri pia. Walikuwa na muda wa kuongea na balozi au hata serikali.

Inawezekanaje wakulima wa Watanzania na Wauganda ghafla washinwe kulinda mazao yao? Kwani wameanza kuuza mazao yao nje leo? Ni muda wa sisi kuvaa mawani ya mbao
 
Biashara za kimataifa hazifanyi kinyama hivyo, huwezi kukurupuka tena kwa nchi unayoitegemea kiuchumi ukata waya kama vile haitakuathiri pia. Walikuwa na muda wa kuongea na balozi au hata serikali. Inawezekanaje wakulima wa Watanzania na Wauganda ghafla washinwe kulinda mazao yao? Kwani wameanza kuuza mazao yao nje leo? Ni muda wa sisi kuvaa mawani ya mbao
Umesoma jinsi mamlaka za Kenya zinavyopima chakula kinavyoingia nchini Kenya? Unadhani wameanza kupima hivi juzi.
 
Kabla ya kuchukuwa maamuzi haya kwanini mawaziri wa pande zote mbili hawakuitana kuangalia jinsi ya kutatua suala hili au jinsi ya kurekebisha tatizo hili 'JAMAA WAMEFANYA UHUNI MBAYA SANA"kwanza bidhaa zao nyingi hazina uhalisia halisi wa zao husika wakikwambia haya ni maziwa 100% full cream ujue ni 15% na 85% ni unga wa mihogo
 
Kabla ya kuchukuwa maamuzi haya kwanini mawaziri wa pande zote mbili hawakuitana kuangalia jinsi ya kutatua suala hili au jinsi ya kurekebisha tatizo hili 'JAMAA WAMEFANYA UHUNI MBAYA SANA"kwanza bidhaa zao nyingi hazina uhalisia halisi wa zao husika wakikwambia haya ni maziwa ujue maziwa ni 15% na 85% ni unga wa mihogo
Jikite kwenye mada.
 
Inasikitisha kuona wanachadema wanashangilia yanayoendelea baina yetu na majirani zetu Kenya.

Huu ni Ulofa wakupindukia na kukosa Uzalendo wa kupindukia...
Crown, unadhani ni ipi iliyobora! Kuzuia mahindi yasiuzwe nje bila kuangalia athari ya wazalishaji? na walalaji? Na hii ya sasa Kenya kuzuia mahindi yetu kwa hofu ya afya za walaji?
 
Back
Top Bottom