Zambia kuzuia Mahindi kuingia Tanzania ni kutowapenda Wakulima Wake?

SOVIET UNION

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
454
1,273
Zambia wana upungufu wa Chakula na kwa sasa hawaruhusu Nafaka kutoka nje ya mipaka ya nchi yao hii ni ili kulianda Walaji wa ndani, kwa hio ni kwamba Mahindi ya Wakulima wa Zambia ni ya Umma?

Linapo kuja swala la Usalama wa Chakula hakuna cha hii ni mali private wala nini, huwa kinacho angaliwa ni usalama, ndio maana nchi kubwa kama India huwa wanapiga ban kuuza ngano nje, nchi za Asia kuna wakati huzuia uuzwaji nje wa nafaka ili kulinda walaji.

Kwa sasa Tanzania Wakenya wanazunguka na Gari zao zenye number za Kenya yumba kwa nyumba kununua mahindi na Mpunga, Hakuna nchi yoyote ina huu utaratibu wa Foreigners kuruhusiwa kuzunguka nyumba kwa nyuma huu utaratibu uko kwa nchi ya Vilaza tu.

Hali ya Chakula sio nzuri kabisa mwaka huu na huenda ikawa mbaya sana kuliko hata mwaka jana na still Bashe anakuambia tunajitosheleza kwa chakula kwa asilimia , 100+

Zambia wanahofia inaweza tokea ghasia endapo bei ya chakula itapanda sana, Sema Tanzania sisi Mazezeta hata kikipanda namna gani hakuna wa kupanua mdomo.

Na kumbuka ni jukumu la Serikali kulisha raia wake, ni jukumu.

Screenshot_20230524_095344_com.facebook.katana.jpg
 
Kwa hiyo zambia wameamua kokomaa wakenya wasipate mahindi, kama wametoa vibali kwa nini wayazuie?
 
Nilishangaa sana kuona wakenya wanatembea mashambani kununua nafaka, nikabaki najiuliza hivi huu ni utaratibu gani?? Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Zambia wanaangalia maslahi ya nchi yao hawana walamba asali kama huko TZ, yanapokuja maslahi ya nchi Rais unatakiwa kuwa na kauli.
 
Ngoja waajiriwa wa Bashe waje kukutukana. Baadhi yao walinishambulia kweli jana kwenye uzi wao fulani hivi. Kisa tu nilitofautiana nao mtazamo kuhusu hili sakata.

Yaani wanataka kuwalazimisha Zambia ambayo ni nchi huru, kuwa na akili na mitazamo kama za kwao.
 
Kwani chakula ni Mali ya Serikali wao ndio walilima au walimsaidia vipi mkulima.
Mkulima haruhusiwe kuuza popote,panapo pesa chakula uagizwa toka popote Duniani,ndo kazi ya wafanyabiashara
 
Wakenya ndio wamesababisha wakulima wetu kuwa na maendeleo we uoni enzi ya JK nyumba za nyasi zilikuwa zikifutika nchini kwa Kasi ya 4G sababu ya plate number za Kenya.
Gari za friji za Kenya zinaingia shambani zinapatikia matunda unapewa pesa cash au walikuwa wanachumbia mazao yaani kabla ya kuvuna wanakupa chako nusu wakija kuvuna unamaliziwa hela yako.
Mazao Sio Mali ya serikali mkulima haruhusiwe kuuza popote atakapo.
Tunaishi kwa kutegemeana misimu ya mavuno,thus yakiadimika mazao nchini yanaletwa toka nchi zingine.
Kwani ujaona parachichi toka Burundi,ujaona embe toka Mombasa, ujaona Michele toka India na Pakistan.
 
Zambia wana upungufu wa Chakula na kwa sasa hawaruhusu Nafaka kutoka nje ya mipaka ya nchi yao hii ni ili kulianda Walaji wa ndani, kwa hio ni kwamba Mahindi ya Wakulima wa Zambia ni ya Umma?

Linapo kuja swala la Usalama wa Chakula hakuna cha hii ni mali private wala nini, huwa kinacho angaliwa ni usalama, ndio maana nchi kubwa kama India huwa wanapiga ban kuuza ngano nje, nchi za Asia kuna wakati huzuia uuzwaji nje wa nafaka ili kulinda walaji.

Kwa sasa Tanzania Wakenya wanazunguka na Gari zao zenye number za Kenya yumba kwa nyumba kununua mahindi na Mpunga, Hakuna nchi yoyote ina huu utaratibu wa Foreigners kuruhusiwa kuzunguka nyumba kwa nyuma huu utaratibu uko kwa nchi ya Vilaza tu.

Hali ya Chakula sio nzuri kabisa mwaka huu na huenda ikawa mbaya sana kuliko hata mwaka jana na still Bashe anakuambia tunajitosheleza kwa chakula kwa asilimia , 100+

Zambia wanahofia inaweza tokea ghasia endapo bei ya chakula itapanda sana, Sema Tanzania sisi Mazezeta hata kikipanda namna gani hakuna wa kupanua mdomo.

Na kumbuka ni jukumu la Serikali kulisha raia wake, ni jukumu.

View attachment 2633069
Nenda kawaulize wao, hii ni Tanzania. Au km vp kahamie huko
 
Nilishangaa sana kuona wakenya wanatembea mashambani kununua nafaka, nikabaki najiuliza hivi huu ni utaratibu gani?? Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Zambia wanaangalia maslahi ya nchi yao hawana walamba asali kama huko TZ, yanapokuja maslahi ya nchi Rais unatakiwa kuwa na kauli.
Ungeshagaa km wanaiba, kununua maana ni biashara, muuzaji anauza. Kanunue wewe ujiwekee akiba. Unataka wakulima wakuwekee akiba? Mbn mipambavu hivyo?
 
Zambia wapo sahihi.

Ila kuna makampuni yalishalipia mahindi FRA kipindi kile ambacho walikuwa wameruhusu.

Waachie basi mahindi kwa wale waliolipia kipindi kile. Kisha waendelee na ban yao.

Maana hela zimekwama serikalini mwao na mahindi hawataki kutoa.
 
Usalama wa Chakula Ni katika ngazi mbili, ngazi ya Kaya na ngazi ya taifa (NSRF) hapo ndio Kuna jukumu na wajibu wa kutunza Chakula kulingana na uhitaji, upatikanaji, matumizi na uwezo.
Kilimo Ni biashara, haiwezekani mtu awekeze kwenye kilimo halafu avune uniwekee ukiritimba wa kuuza kwa Nani kwa Bei nzuri, eti serikali inalinda Chakula. Mimi nilivuna natenga kiasi cha kisio langu la matumizi kwa kiaka 2 - 3.

Cha ziada nauza kwa yeyote mwenye Bei nzuri.
Kama hifadhi, ya chakula/nafaka ya taifa, jirani yangu, mnunuzi toka mkoa mwingine au toka nchi ya jirani mradi ana Bei nzuri kwetu Ni mteja mzuri na Ni motivation kwa kilimo.

Kuweka zuio la kuuza nafaka kwa nchi jirani Ni uonevu kwa wakulima.Karibuni
Tujifunze Kuweka akiba ngazi ya kaya wakati wa kuvuna na Bei zikiwa chini. Vinginevyo tukutane sokoni.
 
Kwani chakula ni Mali ya Serikali wao ndio walilima au walimsaidia vipi mkulima.
Mkulima haruhusiwe kuuza popote,panapo pesa chakula uagizwa toka popote Duniani,ndo kazi ya wafanyabiashara
Mambo huwa hayaendi hivyo, hizo kauli za kudai "mkulima aruhusiwe kuuza chakula popote" ni za kisiasa na haziwezi kupata nafasi kwenye nchi ambazo wapo makini na uchumu wake.

Regulations ni lazima ziwepo.
 
Kwani chakula ni Mali ya Serikali wao ndio walilima au walimsaidia vipi mkulima.
Mkulima haruhusiwe kuuza popote,panapo pesa chakula uagizwa toka popote Duniani,ndo kazi ya wafanyabiashara
Hata wakulima wa KAHAWA kule Kagera wanaruhusiwa kuuza uganda?
 
Viongozi wetu hasa yule Bashe asiyekuwa na lepe la aibu wala chembe ya Uzalendo wanaruhusu wageni kuingia mpaka uvunguni mwetu kununua chakula chote sisi tubakie na njaa.

Wananunua hapa wanapeleka nje halafu wanarudisha tena kutuuzia kwa bei juu.

Huyu Bashe hatufai .

Ila kwakua mwenye mamlaka anatukomesha anaendelea kumfuga tu.
 
Njaa mnajitakia wenyewe, kulima hamtaki, ardhi ipo ya kutosha. Wengine wakilima muwapangie bei how? Mnajua ametumia gharama kiasi gani? Mwache auze ambako anaona atarudisha pesa aliyowekeza.
 
Zambia wana upungufu wa Chakula na kwa sasa hawaruhusu Nafaka kutoka nje ya mipaka ya nchi yao hii ni ili kulianda Walaji wa ndani, kwa hio ni kwamba Mahindi ya Wakulima wa Zambia ni ya Umma?

Linapo kuja swala la Usalama wa Chakula hakuna cha hii ni mali private wala nini, huwa kinacho angaliwa ni usalama, ndio maana nchi kubwa kama India huwa wanapiga ban kuuza ngano nje, nchi za Asia kuna wakati huzuia uuzwaji nje wa nafaka ili kulinda walaji.

Kwa sasa Tanzania Wakenya wanazunguka na Gari zao zenye number za Kenya yumba kwa nyumba kununua mahindi na Mpunga, Hakuna nchi yoyote ina huu utaratibu wa Foreigners kuruhusiwa kuzunguka nyumba kwa nyuma huu utaratibu uko kwa nchi ya Vilaza tu.

Hali ya Chakula sio nzuri kabisa mwaka huu na huenda ikawa mbaya sana kuliko hata mwaka jana na still Bashe anakuambia tunajitosheleza kwa chakula kwa asilimia , 100+

Zambia wanahofia inaweza tokea ghasia endapo bei ya chakula itapanda sana, Sema Tanzania sisi Mazezeta hata kikipanda namna gani hakuna wa kupanua mdomo.

Na kumbuka ni jukumu la Serikali kulisha raia wake, ni jukumu.

View attachment 2633069
Kama wananunua mahindi au nafaka kwa bei ya soko ni sawa lakini uwalazimishe wakulima wauze mazao yao kwa walaji wa ndani kwa bei ndogo eti kwa kisingizio cha usalama wa chakula wa ndani ! Kwani hao wakulima ni manamba wao hao wanaotaka wapate chakula kwa bei rahisi ?? Huwa wanasaidiwa nini na nani wakati wanalima mashambani kwao ??!! Ni kawaida kwa Serikali kutoa ruzuku katika bei za chakula ili wananchi wake wapate chakula kwa bei nafuu !! Wanunue chakula kwa bei ya soko kisha wawauzie wananchi kwa bei ya chini !!
 
Back
Top Bottom