Zitto utapotea, achana na Rais Magufuli!!

Zitto utapotea, achana na Rais Magufuli!!

Unashindwa kuelewe kuwa kazi moja ya upinzani ni kuwafanya wananchi waijue serikali yao Na viongozi wao Na kuweka wazi makosa ya serikali ili serikali ijirekebishe zito yupo sahihi kuwaambia wananchi hili wamjue huyu tabia za uongozi wake wamsome Fulani.
 
Unashindwa kuelewe kuwa kazi moja ya upinzani ni kuwafanya wananchi waijue serikali yao Na viongozi wao Na kuweka wazi makosa ya serikali ili serikali ijirekebishe zito yupo sahihi kuwaambia wananchi hili wamjue huyu tabia za uongozi wake wamsome Fulani.
Nalijua hilo but sio kila siku attack attack haaah hizo ni dalili za kupotea !!
 
Namkumbuka Zitto Zuberi Kabwe wa 2005-2010 na ninamlinganisha na huyu wa sasa mmmmhhh hadi inauma sana tukiendelea kupoteza vijana kama huyu wengine miaka ijayo kuna kazi kubwa sana ya kuja kulikomboa taifa hili!!

Nimekuwa nikijiuliza hivi Zitto ni nini kimempata??

Yuko wapi Zitto aliyeibua sakata la mgodi wa Buzwagi?

Yuko wapi zitto aliyekuwa akipigania masilai ya wanyonge bungeni kupitia ununuzi wa Rada??

Zitto aliyeungana na Dr slaa juu ya Richmond yuko wapi??

Zitto huyu huyu anayetuhumiwa kwa kuwa na mali zisizolingana na kipato chake ??

Zitto huyu huyu ambaye milija yake imezibwa pale NSSF?

Zito amekuwa mtu tena wa kupiga dili na kuakikisha kila kitu amekipata kanunua majumba mazuri ,Magari mazuri,kila kitu kamiliki leo hii kabaki na kazi moja tu ya !!

Kila siku kuiponda selikari ya Rais magufuli!!!

Hivi hakuna mazuri ya kumpongeza Rais magufuli ni kumponda tu ? Hata akipongeza anapongeza kwa unafiki!!

Kama kweli Wewe ni mzalendo unapigania masilai ya watanzania njoo ujibu maswali yafuatayo!!

Wewe si dictator??

Na ulivyo dictator ulipofika tu ACT wazalendo ukapewa cheo cha kiongozi mkuu wa chama hivi uoni kwamba ilo ni tatizo la kupenda madaraka?

Kwani kulikuwa hakuna watu wengine mpaka upewe wewe hicho cheo uligombea na nani?

Sasa hivi professor Mkumbo anawashauri wapinzani mbadilishe njia za kupambana na selikari ya Rais magufuli lakini hata ushauri usikii imekuwa sikio la kufa!

Na juzi tu mama Anna ametofautiana na wewe waziwazi kuusu mwaliko uliotolewa Dodoma !!

Mbili kwanini uliondoka chadema kwa kutaka uwe mwenyekiti uoni hapo kuna tatizo la udikiteta kutaka cheo kwa nguvu? Kwanini ukusema wazi wazi ila ukaanzisha mtandao ndani ya chama?

Ulishamsikia magufuli anagomea cheo ndani ya chama toka amejiunga na CCM hata cha mwenyekiti wa shina??

Leo hii unatoka na kumfananisha rais magufuli na Putin wa Russia hivi hoja yako ya Jana kwamba watu wamsome Putin ina faida gani kwa taifa?

Kuna faida gani kwa wananchi wa Ujiji??
Hivi unafikiri wananchi wa vijijini wanaweza kaa wasome vitabu au wapekue Internet kwa vifulushi vipi hivi hivi vya wanyonyaji Voda,Tigo na Airtel?

Baada ya kuishauri selikari ilifufue shirika letu la TCCL ili tupate affordable bundle wananchi waweze kupata Internet ilivyo bora na kuepukana na makampuni ya wanyonyaji upo tu kukosoa !!

Mkuu Zitto tulikuheshimu sana lakini sasa your politically finished!!

Baada uungane na Magufuli mpeleke kiwanda cha nyavu za kuvulia Dagaa ujiji ??unaangaika eti wananchi wamsome Putin Hivi mwananchi wa kawaida wa ujiji atakuelewa kweli??


Kwanza tu nikufaamishe taarifa nyingi unazozisoma kwenye mitandao kuusu Putin kama hazitoki Russia ni za kupika kutoka nchi za magaribi!!

Nchi za magaribi hazimpendi Putin kwa sababu analeta mabadiliko ya kweli uko Russia!!

Ni kiongozi imara asiyeteteleka kama alivyo Magufuli hivyo vyombo vya habari vya magaribi haviwezi kumpamba hata kidogo Putin ni kiongozi imara kama alivyo Magufuli!!

Ushauri kwako kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo!!

Watu unaotakiwa kubishana nao ni Mkuu wa mkoa Kigoma,Mkuu wa willaya jimboni kwako,Mkurugenzi jimboni kwako na spika wa ubunge Hao ndio size yako!!

Hakuna mtu anayeupata Urais kwa kumponda Rais aliyeko madarakani hapa Afrika nikukumbushe lazima tuambiane ukweli!!

Tanzania- Professor Lipumba aliponda ameenda,
Kenya-Raila Odinga aliponda huyo anakwenda,
Uganda-Kiza Besige aliponda anakwenda,
Zimbabwe- Morgan Shangelai aliponda amekwenda !!

Mifano ipo mingi tu ila nikushauri pigania masilai ya wananchi wako wa ujiji na Tanzania!!

Nasikitika tunapoteza nguvu kazi za Taifa hasa vijana tuliokuwa tunawategemea wanatoweka taratibu.

Asanteee.
Nchi haiendeshwi kwa kujipendekeza. Kumuelewa zitto mpaka utoa akili za utumwa na uwe huru
 
Tanzania- Professor Lipumba aliponda ameenda,
Kenya-Raila Odinga aliponda huyo anakwenda,
Uganda-Kiza Besige aliponda anakwenda,
Zimbabwe- Morgan Shangelai aliponda amekwenda !!
Zambia - Fredrick Chiluba aliponda, akawa rais
Malawi - Bakili Muluzi aliponda, akawa rais
DRC - Laurent Kabila aliponda, akawa rais
 
Magufuli kufananishwa na putin kuna tatizo gani kwani?.
Putin ni mmoja wa viongozi wazuri sana duniani,maana hana undumilakuwili yule
Na kama umesoma vizuri nimewafananisha vizuri lakini tatzo la mwenzetu anatumia njia hiyo kupotosha!!
 
Nalijua hilo but sio kila siku attack attack haaah hizo ni dalili za kupotea !!
Wewe utakuwa Na matatizo au labda upo kwenye ajira za buku Saba MTU kusema ukitaka kufahamu uongozi Wa Fulani msome Fulani ni ku attack MTU hapo wewe unamwandama zito bure tu
 
To me Zitto atabaki kuwa mmoja wa nguzo imara za upinzani na ukuaji demokrasia nchini.Pamoja na mapungufu aliyonayo ila bado ni mmoja wa wanasiasa bora kuwahi kutokea Tanzania.Ndiye aliyefungua milango kwa vijana kufanya siasa.Zipo motions kubwa bungeni alizisimamia na kuleta tija kwa taifa.Nashauri wakati tunambeza ila pia tusisahau na mema mengi aliyofanya kupitia bunge la tisa na kumi.
 
Zitto amekuwa mtu wa majungu tu. Kama anataka wananchi wamuheshimu na wamkubali kama rais mtarajiwa lazimaaje na solution sio kulalamika tu kila siku. Watu tumeshaanza kukuchoka ausomeki umekuwa unadandia kila kitu njoo na new vision zako ili tuone tofauti yako na viongozi wengine.
 
Mwanasiasa makini alishindwa kuwashawishi wananchi walau wampe majimbo mawili??
Makini sana na watu wana muamini yeye ndio sababu pamoja na kufukuzwa chadema na kuvuliwa ubunge amerudi tena bungeni sa sasa kwa JIMBO KUBWA LA MJINI tofauti na kule alipokuwa mwanzo. Wanamuamini yeye si mtu mwingine.
 
Tatizo la Zitto siku zote ni kutafuta sifa bila kujali maslahi mapana ya wananchi. Mwenzie Magufuli hatafuti sifa bali amejikita kwenye mambo ambayo anaona yana manufaa kwa wananchi anaowaongoza. Hajali kama atasifiwa au la.

Ifike mahali wanasiasa waangalie mahitaji ya wananchi maana mwisho wa siku na wao wakishika madaraka watapaswa kushughulikia shida za wananchi.
 
Zitto amekuwa mtu wa majungu tu. Kama anataka wananchi wamuheshimu na wamkubali kama rais mtarajiwa lazima haje na solution sio kulalamika tu kila siku. Watu tumeshaanza kukuchoka ausomeki umekuwa unadandia kila kitu njoo na new vision zako ili tuone tofauti yako na viongozi wengine.
Mkuu asante
 
Kama kwa kumkosoa JPM mtu atapotea basi watapotea wengi nchi hii kwa maana atakosolewa tu hata kuna wakati na yeye mwenyewe atajikosoa
 
Back
Top Bottom