Zitto utapotea, achana na Rais Magufuli!!

Zitto utapotea, achana na Rais Magufuli!!

Mtoa mada umeumia kwa ZITTO kuondoka kuwa kibaraka wa ccm. 2005-2010 Zitto aliweka mkataba na JK wa kutomsema vibaya baada ya Kumuingiza kwenye kamati ya uchunguzi wa mikataba ya madini. Nikukumbushe pia hakuna kiongozi wa Upinzani aliyeshinda urais kwa kumsifia au kujipendekeza kwa Rais wa chama tawala,hakuna
Mkuu wapo wakwanza ni Uhuru Kenyatta Kenya!!
 
Zito ni mwanasiasa msomi.Ni kijana wa kwanza kuingia kwenye siasa akiwa mwakilishi wa jimbo mwenye umri mdogo katika vyama vingi.Vijana wengi waliingiwa hamasa nao wakaingia katika siasa za uwakilishi.Anasema Putin asomwe,hii ni hoja,mwingine atasema msomeni Hitler.Hawa ni viongozi walioongoza mataifa yao kwa mitindo yao.Unapowasoma unalinganisha au kutofautisha na kile kilichopo.Aje mwingine aseme msomeni Nyerere,atasomwa ili kufahamu ulinganifu au utofauti kati ya wawili.
Mkuu ukuelewa hoja yangu hatuwezi elewana
 
Huku Lowassa pale Zito,hawa ni wapinzani wana hoja zao.Huwezi kuonekana ni imara bila kuwa na wapinzani.Hoja hujibiwa kwa hoja,mfano kwa mfano kwa mfano.Siasa ndivyo zilivyo.
Lowassa tena daaah
 
Kila mmoja anaowajibu wa kuhoji na kutoa maoni, japo wanasema "mkubwa/ baba hakosei ", je kila analofanya mkubwa lipo sawa? Mtoa mada umemchambua Zitto pasipo kuchambua hoja alizotoa Zitto, kumbuka kuwa kila binadamu anakosea hivyo ni jukumu letu kukosoa pale ambapo tunaona si sawa.
 
Katika uhalisia kuna mengi mazuri yamefanywa na Magufuli na tunamwombea hivyo aendelee kufanya yaliyo mazuri sababu ni kazi yake sio kwamba anajitolea,tunamlipa kwa hayo,lakini kayika yote mazuri aliyoyafanya wanachojaribu kuhoji upande wa pili na kuonekana wako kinyume nae ni namna gani hayo yameweza kuleta kile watanzania wanahitaji au zaidi ni kuteka hisia za wananchi na kuwafurahisha mwisho wa siku tunaendelea kubaki na miaka yetu 50 ya uhuru wa ufukara,Hili ni jambo liko wazi kila mtu humu analijua na kujadili kila siku sasa hata wewe tunaweza kukutilia mashaka una yako binafsi na Zitto pamoja na kasoro za Zitto pia
Umeongea jambo la msingi, chukulia mfano suala la bodaboda kulipia ushuru na ilihali wanasema wanataka vijana wajiajiri.
 
Sawa lakini nimekwambia anampongeza kwa unafiki tu!!
Unataka ampongeze vipi ili ujue si unafiki? Nafsi ya Zito unatembea nayo wewe? Unataka kusema kila analofanya Magu lipo sahihi? Maana ya upinzani ni ipi kwa mtazamo wako?
 
Usaliti, unafiki, uchu wa Madara , yote yanafaa kuwa majina ya Zitto Kabwe.
Mimi si mfuasi wa Zitto, lakini kama ni uchu wa madaraka kwa nini hakusema agombee urais 2015? Je, ni haki Mbowe kuwa M/kiti kwa kipindi chote hicho? Tusimshambulie mtu kwa hisia.
 
Zitto ashakua basket case.
Methinks, Zitto alikuwa hana hoja toka awali ila kuna watu ndani ya serikali walikuwa wanampa skendali ili aziongee na kumjenga kisiasa. Kwa kipindi hiki, zitto hatokuwa na hoja yoyote anayobeba maji zaidi ya vijimaneno vya mtaani na vya kuokoteleza. By the way, Putin is doing great job hasa huko Syria.
Huoni kama hao watu walikuwa hawana sehemu ya kusemea zaidi ya kumtafuta mtu wa kuyasemea yale? Sidhani kama zilikuwa "skendal" kama ulivyosema maana ukweli wake ulitufanya wengi kuijua serikali, pia kumbuka unaweza kupewa jambo uliseme na usipokuwa mtu makini hutaweza kulisemea.
 
Daa nimekukubali mkuu umeona mbali,ukiona mtu sasa ivi anamponda na kumwandama jpm ujue ni miongoni mwa wapiga dili waliobanwa na kufungiwa mirija yao ya ulaji,zitto uko kimaslahi zaidi aliona wakina mbowe wanagawana ruzuku yeye anapata kidogo akawakimbia akaona anzishe chama chake uenda kikakua na ruzuku itaongezeka kasi ya jpm inakiua chama amechanganikiwa.

Wakosoaji wanamsaidia sana Rais kufanya maamuzi sahihi kwa maendeleo ya nchi yetu kuliko unavyofikiri wewe. You just don't know what you are saying...... Tungeishi katika dunia ambayo kila kitu unachofanya unashangiliwa tu basi ingekuwa hatari sana....
 
(1)Kuna asiyependa madaraka hasa kwa wanasiasa?
(2)Asimkosoe Rais hata akikosea?
(3)Kuna asiyetaka kumiliki mali nyingi kadri iwezekanavyo?
(4)Eleza ni jambo gani la maana imefanya serikali hii tangu kuingia madarakani na kuleta matokeo chanya moja kwa moja kwa sisi wananchi wa kawaida?
 
Unataka ampongeze vipi ili ujue si unafiki? Nafsi ya Zito unatembea nayo wewe? Unataka kusema kila analofanya Magu lipo sahihi? Maana ya upinzani ni ipi kwa mtazamo wako?
Mi sijakataa but anakuwa mjuaji sana kujifanya kila jambo analijua kuliko watanzania wote
 
Basi ungejikita kuchambua hoja ambazo unaziona si sawa kuliko kuzungumzia maisha binafsi ya Zitto.
 
(1)Kuna asiyependa madaraka hasa kwa wanasiasa?
(2)Asimkosoe Rais hata akikosea?
(3)Kuna asiyetaka kumiliki mali nyingi kadri iwezekanavyo?
(4)Eleza ni jambo gani la maana imefanya serikali hii tangu kuingia madarakani na kuleta matokeo chanya moja kwa moja kwa sisi wananchi wa kawaida?
Hivi wewe hayo madawati yaliyotolewa nchi nzima kwanini yalisgindikana miaka 50
Hivyo vitanda muhimbili vimepatikana ndani ya muda gani
Pesa zilizookolewa kwa kulipa wafanyakazi hewa ni ngapi??

Jiulize hayo mambo ndo uludi kukoso!!
 
Acha papara mtoto mzuri.
uludi=urudi.
kukoso=kukosoa.
(i)Sasa basi, matibabu bora sio vitanda tu tena vikiwa vimepelekwa Muhimbili pekee wakati Tanzania nzima hospitali zina upungufu mkubwa wa vitanda. Isitoshe hata leo hii nenda pale uone wagonjwa wanavyoendelea kulala watatu watatu.

(ii) Madawati yatawekwa wapi au chini ya mwembe togwa? Japo Serikali imetumia nguvu kubwa iliyojaa vitisho kadhaa kuhusiana na uchangiaji wa madawati bado lengo halijatimia na halitatimia kwa namna wanavyoenenda.

(iii) Fedha zimeokolewa kwa watumishi hewa,je hicho kiasi kimeelekezwa wapi katika huduma ya moja kwa moja za wananchi!?

Yote tisa kwanini Serikali imekomalia kuongeza kodi za kuzidi kutuongezea mzigo watumiaji/walaji wa mwisho wa Huduma/bidhaa?
Vipi kuhusu Mawaziri/Viongozi waliongia mikataba ya madini na gesi na mengineyo inayotuingizia hasara kila siku kwa Taifa?

Modes of Operand ya Serikali iko na mistakes kibao.
 
Mkuu hayo nda anatakiwa kuyasema Zitto sasa sio mambo ya Putin
 
Back
Top Bottom