Ziara ya Mhe. Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba Mkoani Simiyu imekonga mioyo ya wana-Simiyu. Katika mazungumzo na wananchi mbalimbali, wengi wameeleza kuvutiwa na namna Waziri Mkuu anavyokemea uzembe na wizi, pamoja na kusisitiza hatua za kubana matumizi ili fedha hizo zielekezwe katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande mwingine, wananchi hao wamesema utatuzi wa kero za wananchi papo kwa papo umesaidia wanyonge kupata haki zao. Kwa mtazamo wao, wameuita huo ni “Umagufuli mtu.”
Mmoja wa wananchi hao ananukuliwa akisema:
“Tumepata Magufuli mpya hapa. Haya tunayoyaona mbele ya macho yetu yanatukumbusha ule uongozi wa kusimamia haki na kukemea uzembe. Ona Maswa, wanyonge wamepata haki yao. Ona Bariadi na Itilima, tumeshuhudia kwa macho yetu.
Kuna baadhi ya watendaji ambao wamekuwa wakiwadhulumu wananchi na kuwanyima haki zao kwa makusudi. Lakini Waziri Mkuu anapofika, anawasikiliza wananchi, anachukua hatua na kutatua kero zao papo kwa papo. Huu ndio umagufuli wenyewe.
Sisi wananchi tumeona kwa macho yetu. Tumepata Magufuli mpya hapa. Huyu ni kiongozi anayesimama upande wa wanyonge na kutetea haki zao. Huyu ndiye Mtetezi wa Wanyonge.”
Tunajua haya ambayo tumeanza kuyasikia kwamba magenge yenye nguvu hayamtaki Waziri Mkuu na yanapambana kuhakikisha anaondoshwa au kumdhibiti kuelekea 2030. Tuseme tu, sisi wanyonge tutamwombea kwa Mungu.
Huyu ndiye Mtetezi wa Wanyonge.