Mkuu,saini zimesha patikana tena kwasasa ni zaidi ya 73....Kwa vile imebaki siku 4 napendekeza hivyo, lakini la msingi apate hizo sahihi 70 akomae nazo hadi bunge lijalo!
siamini kama ccm na wabunge wake wanaweza kumpigia kura waziri mkuu ya kutokuwa na imani naye (vote of no confidence)achilia mbali raisi wao, na kama unavyojua raisi wako naye hawezi kuvunja bunge...hana uwezo wala maamuzi hayo, atavunjaje ili uchaguzi urudiwe wakati inajulikana kuwa hawezi kurudi pale magogoni? si bora afabye liende?
then hii ya kuvunja bunge huwa nu kama timing, especiaally kama chama tawala hakina wabunge wengi lakini kinakubalika mtaani...so ikitokea risk ya vote of no confidence, maybe kwa sababy za kisisasa au kishabiki...raisi kwa kujua kuwa anakubalika mtaani, anaweza kuvunja bunge...
Kama sahihi anazo, si angepeleka leo?Mwanakijiji
Nakubaliana na wewe kuhusu technicalities za kanuni kuwa akiwasilisha J3 spika anaweza kuitishwa kikao cha bunge maalum kwa lengo la kuitupilia mbali hoja ya Zitto na ikawa tabu kuirudisha tena kabla ya miezi 6. Lakini kama serikali ina haja ya kuitupilia mbali itashindwa nini kufanya hivyo kwenye bunge la bajeti.
Mimi nafikiri hii motion iendelee na moto wake (supu hunywewa ingali ya moto), kama sahihi zimetimia nashauri J3 Zitto aamukie kwenye mlango wa spika kuonyesha yuko na wabunge wako serious na issue yenyewe. You never know bwana wabunge walioweka sahihi zao watafikiriaje, wabunge ni binadamu wanaweza kurubuniwa ku-withdraw sahihi zao. Serikali pia inaweza kutumia huo mwanya kuvunja nguvu ya umoja huo. Kumbuka hizo sahihi si za CDM pekee kuna za CUF na za CCM.
Faida ya ku-file J3 ni pamoja na kuipa pressure serikali kutekeleza matakwa ya wabunge ambayo ni pamoja na mawaziri wale watano kujiuzulu. Pressure hii inaweza kumfanya PM mwenyewe kuchukua maamuzi magumu au kushauriwa na rais kufanya hivyo. Lakini jambo hili likiachwa kupoa linaweza kuipa ahueni serikali na kuanza hata kuwanyanyasa wabunge wa CCM walioonyesha kuunga mkono. Tusiwape chance, kwenye mpira unapoona opponent wako amechoka usibweteke ongeza mashambulizi unaweza kumtoa kwa knock out.
JK kumteua waziri mkuu mpya (Dk Asha Rose Migiro)......?Labda JK ateue waziri mkuu mpya kitu ambacho ni kigumu sana kutokea.
Lakini zaidi watu wasije wakachanganya vitu viwili - kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Ili hoja iweze kuletwa Bungeni zinahitajika asilimia 20 tu ya wabunge (ndipo namba ya kura 70 inapokuja). Kura 70 HAZIWEZI kumuondoa Waziri Mkuu; zinaweza tu kufanya hoja iletwe Bungeni. Baada ya kuletwa bungeni na wabunge kupiga kura inahitajika asilimia 50+1 kwa Bunge kupitisha Azimio la kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Hii ina maana ili azimio lipitishwe ZINAHITAJIKA kura 178 na siyo 70!
mwanakijiji, kama ni macho huenda unayo manne, kama ni masikio nadhani yako 4 pia, ubongo kawaida umegawanyika sehemu kuu tatu lakini wewe sina hofu, wewe ni sehemu sita. Hii inapelekea wewe kuwa na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo, wengine wakifikiri mbili wewe unafikiri zaidi.
HOJA YA ZITTO KWELI SIO KUPIGA KURA BALI NI KUWASILISHA HOJA BUNGENI.
USHAURI WAKO WAKIUFANYIA KAZI, WATAFANIKIWA"So, kwa sasa nashauri a strategic withdrawal ya hoja hii!!"
Sahihi zimeshatimia na kumwagika lakini ilipangwa hadi J3 ndipo wawasilishe, kumbuka kuna taratibu zingine pia na kukusanya supporting documents huwezi kupeleka majina tu bila maelezo ya hoja yenyewe.Kama sahihi anazo, si angepeleka leo?
Mimi nadhani wajibu wa chama cha upinzani kama chadema kufanya mambo kwa maslahi ya umma na kujenga imani kwa umma kuwa wanao uwezo wa kuform serikali inayowajibika pia siasa za kujenga umaaru kupitia madudu ya chama tawala usiwe msingi wa chadema, chadema itaendelea kujipatia umaarufu kwasababu inajenga misingi ya uadilifu na uwajibikaji wa viongozi!Hayo yote yakifanyika na ikachaguliwa teem mpya makini,,je CDM watashika dola 2015/2020?
Sijaelewa nia ya upinzani ni nini hasa.
1.Ni kuombea Mungu chama tawala kizidi kuboronga na wao (wapinzani)kujikita kueielezea jamii madudu hayo na kuomba ridhaa?
2.Kuikosoa serikali ili iende sawa na (chamatawala) kuendelea kushika hatamu?
JK kumteua waziri mkuu mpya (Dk Asha Rose Migiro)......?
So, kwa sasa nashauri a strategic withdrawal ya hoja hii!!
Hayo yote yakifanyika na ikachaguliwa teem mpya makini,,je CDM watashika dola 2015/2020?
Sijaelewa nia ya upinzani ni nini hasa.
1.Ni kuombea Mungu chama tawala kizidi kuboronga na wao (wapinzani)kujikita kueielezea jamii madudu hayo na kuomba ridhaa?
2.Kuikosoa serikali ili iende sawa na (chamatawala) kuendelea kushika hatamu?