Zitto: Ujenzi wa CHADEMA imara - Fuata misingi!

Zitto: Ujenzi wa CHADEMA imara - Fuata misingi!

Status
Not open for further replies.
ZZK hakuutaka Umwenyekiti kwa style hiyo unayosema, bali alipenda kuongeza ushindani, kumfanya anayegombea kuonesha cha ziada ili apewe nafasi na si kubebwa na historis tu. Na hicho ndo bado nakiona kwake japo kuna mambo hata mie huwa siyaelewi kwake
 
unaweza kuwa na misingi thabiti, lakini bila watu wa kuijenga - it will be like wasting time.... sawa Zitto?

misingi mizuri lazima iwe na utaratibu pia -- mfano mdogo tu makamanda wote wapo Arumeru wanapiga kampeni chama kifanye vizuri wewe upo dar unatangaza kuwania urais wa nchi -- hiyo ndiyo misingi ya uongozi bora unayoiongelea?
 
Chama ni wanachama,chama ni viongozi,chama ni vikao,chama ni umoja na mshikamano. BILA ya mambo hayo, chama kitakufa!
 
and who are you to answer that?? are you his pr or his secretary?? give me a break i didnt address the question to you

He is not running even on my circle, you should PM if the questions was specific to him... Just a food for thoughts Lady, nothing personal. Sorry for inconvenient
 
Kuona, kusoma na ukaelewa ni kipaji! Ukiweza kunielewakwa vema kwa hizi Quotes basi nawe una kipaji.
...Moja ya msingi wa CHADEMA ni ‘kujenga chama chenye kutoa fursa ambapo kila mtu, bila kujali asili na hali yake, anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake. Kwa mwanasiasa mwingine yeyote nafasi hii ilikuwa ni nafasi nzuri ya kujitengenezea fursa yeye mwenyewe kwa kuhamasisha ufuasi wa watu badala ya ufuasi wa misingi ya chama...
Mtela Mwampamba-Excerpt of his Post in TANURU LA FIKRA says:
Watanicheka, watanitukana, watanidhalau na kisha watakuwa wafuasi wangu na nitakuwa shujaa wao!
--
Molemo, Ben Saanane, Zitto
 
Last edited by a moderator:
Huyu jamaa anayeitwa ZITO ni mpuuzi sana, anaongelea misingi, wakati yeye ndie anayebomoa hiyo misingi.

Kaanzisha makundi, kila kukicha ni vituko, sasa anatamka kufuata misingi, misingi gani hiyo ambayo yeye ndiye m-bomoaji mkuu.

ZITO acha unafiki.
 
Tujikumbushe kidogo alafu tuendele kumtathmini huyu zito na mambo yanayoendelea ivi sasa.
 
ZZK anakipenda zaidi chama kuliko watu!, angemchukia Dr, saa hizi, Dr na kibaraka wake, wangekuwa wapi kwa njama za kupanga mauaji kupitia sumu ya panya?!. ZZK kupitia "sixth sense" iling'amua mpango huo, akakwepa katakata kukutana na huyo kibaraka!. ZZK as "bright as he is!", angeweza kukubali kukutana na huyo "assasin" na kujiavail himself ili ile sumu iwekwe, then angeondoka na sample!, unadhani madhalimu hao wangekuwa wapi?!.

Sikatai kuwa Dr amefanya and still anafanya kazi kubwa sana na nzuri ndani ya Chadema kuongoza M4C, ila Dr naye ni binadamu na sio malaika hivyo "he can make mistakes", tatizo ninaloliona hapo ni kwa baadhi ya watu kuabudu watu wakidhania watu fulani ni malaika!. Kembe no, ZZK haabudu watu ila "he is a human being", kosa lake kubwa ni kuwa "too frank!" na "too straight!", hakubalali kupelekwa pelekwa tuu kama "ling'ombe" hata kufanya kile asichokiamini!.

ZZK is a fighter anaeamini katika "head on collision" by "taking the bull by its horns" kwa kupambana naye face to face, and "not by the tail" kwa kuzunguka zunguka, na kupambana kwa kususa, kugoma, kutoka nje na kujidai hawamtambui JK! but at the end of the day, ni "Chai Ikulu", hawezi kutamka wazi kuwa "sometimes Chadema are wrong!" ila vitendo na kauli zitawajulisha wenzeke kuwa hakubaliani nao!, japo kisiasa ni kosa kwenda against "collective responsibilities" but you better stand alone on the right track kuliko kuswagewa kwenye collective resiponsibility na kuishia kuizamisha meli yote!.

I still stand with ZZK no matter what "that's what friends are there for!"
Pasco.

Ukapiga ukaua Zitto makosa yake wazi na akakiri bado utasimama naye ama kweli kweli wewe mpambe wa Lowaxsa mna lenu .Ngoja aondolewe Chadema uende naye .
 
Ukapiga ukaua Zitto makosa yake wazi na akakiri bado utasimama naye ama kweli kweli wewe mpambe wa Lowaxsa mna lenu .Ngoja aondolewe Chadema uende naye .

mkuu zuberi maghoa! Kama unamfatilia kwa umakini huyu pasco. Lazima utagundua vitu vifuatavyo:
1) anamtetea sana lowasa.
2)pia ajiweki mbali na zito katika kumtetea.
3)anaipiga vita cdm lakini anajitahidi kwa kujifichaficha kupigia chapuo ccm.
4)......
5)......

Kwa ayo na mengineyo jaribu kuunganisha dot.
 
Fuata misingi, sio watu, sehem ya pili: Vita dhidi yaufisadi.

Katika makala iliyopita tumeona namna kwa kupitiaMbunge wa Kawe CHADEMA ilivyoweza kutekeleza kwavitendo msingi wake wa kusimamia rasilimali za Taifa.Mbunge wa Kawe, Ndugu Halima Mdee, alifanikiwakupitisha hoja Bungeni yenye kutaka tathmini ya Ardhi naugawaji wa Ardhi hapa nchini. Ardhi ndio rasilimali pekeeambayo kila Mtanzania anaweza kufaidika nayo na hivyougawaji holela wa ardhi unatishia uwepo wa Taifalenyewe. Leo tunaendelea na mfano wa pili katikamfululizo wa makala 6 kuhusu ufuasi wa misingi ya chamabadala ya ufuasi wa watu kwenye chama.
Katika msingi ambao CHADEMA imejitambulisha nao kwakiasi kikubwa ni ule wa kupambana na ufisadi. Viongoziwa CHADEMA na hasa wabunge wake wamekuwa mstariwa mbele kuhakikisha kuwa vita dhidi ya rushwa,ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka inaendeleakuwa kipaumbele katika kampeni zake. Pamoja nakwamba juhudi za CHADEMA kuibua masuala ya ufisadihazijamaliza ufisadi, juhudi hizi zimewafumbua sanaWatanzania na hivyo nao kushiriki katika vita hii.
Kati ya mwaka 2007 na 2010 kumekuwa na maskandalimakubwa ya ufisadi yaliyoibuliwa na wananchi mbalimbalikupitia wabunge na vyombo vya habari. Mifano yamaskandali hayo ni pamoja na Wizi wa tshs 133 bilionikutoka Benki Kuu ya Tanzania, Wizi wa tshs 255 bilionikupitia kampuni ya Meremeta, wizi wa mabilioni ya fedhakupitia mfumo wa kuagiza bidhaa kutoka nje (Import Support), mkataba wa kuuziana umeme wa Richmond namauzo ya mgodi wa makaa ya mawe Kiwira. Kipindi hikikilikuwa ni kipindi ambacho Bunge lilikuwa linasubiriwakwa hamu maana kila mkutano wa Bunge ulikuwa namasuala nyeti ya kujadili kuhusu Taifa. Katika kuongozamapambano haya, wabunge wa CHADEMA ndio walikuwamstari wa mbele chini ya aliyekuwa Naibu Kiongozi waUpinzani Bungeni na Katibu Mkuu wa CHADEMA dkt.Willibrod Slaa.
Ndugu Slaa alikuwa anatekeleza msingi mmojawapo waCHADEMA wa uwajibikaji mbele ya wananchi. Alikuwaanatekeleza jukumu lake la kibunge la kuisimamia Serikalikwa vitendo kwa mwongozo wa misingi ya CHADEMA.Kwa kua Dk Slaa ni Mtanzania na ana ndugu na jamaahumu nchini, huenda kuna watu anao wajua ambaowalifaidi katika masuala haya. Na iwapo mbunge huyuangekuwa anajali maslahi ya watu binafsi ama angekuwamfuasi wa watu angeweza kufumbia macho masuala hayana Watanzania kwa kiasi kikubwa wasingepata fursa yakujua mambo haya.
Suala la EPA lilikuwa suala tete sana. Baada ya uchaguziMkuu wa mwaka 2005 na CCM kuibuka na ushindimkubwa sana wa asilimia 80 ya kura za Rais na hataBunge na kujizolea viti vingi sana Bungeni, siasa zaupinzani zilizorota kwa kukata tamaa. CHADEMA ilikuwaimeingiza wabunge wapya wanane kati ya wabunge wotekumi na mmoja alieingia Bungeni katika Bunge la Tisa.Ilibidi team hili jipya la wabunge wa CHADEMA lijipangesawa sawa kuhakikisha kuwa kazi ya Upinzani Bungeniinafanyika kwa ufanisi hasa ukizinagtia kuwa kambi yaUpinzani ndio unayofanya kazi haswa ya kuisimamiaSerikali. Kambi ya chama tawala mara nyingi hufanya kaziya kuishauri Serikali badala ya kuisimamia. Ufisadi waEPA ulikuwa ni mtihani kubwa sana kwa pande zote mbilindani ya Bunge.
Kwanza, ilibidi taarifa za awali za ufisadi huu kutafutwakutoka kwa walioshiriki kwenye ufisadi lakini wakawa namanunguniko kuwa hawakupata walichotaka, yaanimgawo wao. Mmoja wa waathirika aliandika ‘dossier’ nakuisambaza kwenye mitandao ya internet. Kwa ujasirimkubwa sana Dkt. Slaa alitumia nyaraka hizizilizopatikana kwenye internet kutaka majibu ya Serikalindani ya Bunge. Bunge la Bajeti la mwaka 2007 lilitumikakwa mafanikio makubwa sana kuhakikisha kuwa majibuya Serikali kuhusu wizi wa akaunti ya EPA yanapatikana.Chini ya dkt Slaa kambi ya upinzani iliandaa hoja binafsi ilikupata azimio la Bunge kuchunguza na kuchukua hatuadhidi ya ufisadi huu.
Pili, changamoto kubwa ilikuwa ni kuhakikisha ajendainasimama mpaka ukweli ujulikane. Spika wa Bungealipotishia kunyonga hoja ya EPA ndani ya Bungetulikwenda kwa wananchi kwa kuanzia Jangwani nabaadaye MwembeYanga tarehe 15 Septemba 2007.Jangwani dkt Slaa alieleza hoja yake kwa ufasaha naMwembeYanga alitangaza orodha ya Watanzania 11wenye kashfa za kujibu kwa vyombo vya sheria. Orodhahii tuliita ‘list of shame’. Hoja iliendelea kusimamiwampaka uchunguzi wa kina kufanywa na Serikali kuwekawazi watu na makampuni yaliyoshiriki katika kukwapuamabilioni haya ya fedha za Umma.
Moja ya kazi iliyo tekelezwa na CHADEMA kwa nguvukubwa ni kuelimisha wananchi kupitia mikutano ya habarina maandishi yetu. Dkt Slaa alilinganisha fedha hizi nanyumba za Walimu, madarasa, kilometa za barabara nk.Kila mkutano wa hadhara au wa ndani, wabunge waCHADEMA waliutumia kuhakikisha ujumbe huu unafikiawananchi kwa lugha wanayoielewa. Serikali nayo ilitumaMawaziri na Manaibu Mawaziri kwenda kwa wananchikuwaelemisha upande wao. Wananchi hawakuwaelewana maeneo mengine Mawaziri walizomewa na wananchi.Nchi ilikuwa imevimba. Wananchi walikuwa wamefura kwahasira. Katika kipindi hiki na miezi ilio fuata, maelfu yawatu walijiunga na chama chetu kwa kuamini kwamba nichama cha misingi yenye manufaa kwa Taifa, mbali navyama vyenye ushabiki na ufwasi yenye kunufaisha watubinafsi.
Somo kubwa tunalolipata hapa ni kwamba iwapo chamacha siasa kikiwa na umoja kwenye hoja ya msingi nakuisimamia kwa pamoja mafanikio yanakuwa ni makubwasana. Mafanikio ya vita dhidi ya ufisadi yalitokana nawananchi wote, bila kujali vyama vyao, kuona viongozi waCHADEMA kwa pamoja wakisimamia suala hili lenyemanufaa kwa Tanzania kama taifa, na kulieleza kwa kinakwenye mikutano mbalimbali. Iwapo wanachama auviongozi wa chama cha siasa wataendekeza ufuasi kwamtu mmoja mmoja, watapofushwa na ufuasi huo nakutoshiriki kupeleka ajenda ya chama mbele. Halikadhalika, iwapo wanachama au viongozi wa chama chasiasa wakiamua kusimamia ajenda za chama kutokana namisingi ya chama hicho badala ya kusimamia ufuasi kwamtu, chama hicho lazima kifanikiwe katika malengo yake.
Dk Slaa hakusimamia hoja hili kama mtu binafsi, au kamakiongozi wa wafuasi wake, alisimamia hoja kama kiongoziwa chama, na zaidi, kama Mtanzania anae simamiamisingi ya chama chake kwa manufaa ya taifa nzima.Misingi ya kupinga ufisadi iliyowekwa na dkt Slaa kwenyehoja ya EPA ndio ambayo wabunge tuliobakia waCHADEMA tunaiendeleza. Hoja ambazo zimeibukabaadaye kama ufisadi kwenye manunuzi ya mafuta yakuendesha mitambo ya umeme unaoendelea mpaka hivisasa na hata kashfa ya mabilioni ya Uswiss nimwendelezo ya misingi hii. Ujasiri wa kulitumia Bungekujadili masuala ya msingi ya Taifa ni moja ya urithimkubwa sana ambao Dkt Slaa ametuachia wabunge waCHADEMA katika Bunge la Kumi. Kupuuza ujasiri huukwa kupendekeza ufuasi wa watu binafsi ni faida kwawapinzani wetu wa kisiasa, na hasara kwetu sisi wenyewekama wabunge wa upinzani, na ni hasara zaidi kwa Taifaletu ambalo linategemea kua Bunge litasimamia serikali.
Ufuasi wa misingi ya CHADEMA unatuelekezakuhakikisha kwamba hoja yeyote yenye kuimarishamisingi ya chama inayotolewa na mwanachamamwenzetu inasimamiwa mpaka mwisho. Mwisho nikuhakikisha hatua stahili zimechukuliwa maana haitoshi tukuibua masuala Bungeni au kwenye mikutano ya hadharana kuacha yakielea. Mwisho ni pale ambapo ama sheriaimetungwa au wakosaji wamefikishwa kwenye mikono yasheria. Ufuasi wa watu hupofusha. Ufuasi wa misingi yachama hurutubisha chama cha siasa.
Katika makala ijayo, tutaona namna Mwenyekiti waCHADEMA, ndugu Freeman Mbowe aliimarisha chamakutoka nafasi ya tano katika vyama vya upinzani hadinafasi ya kwanza, kwakuweka misingi ya chama mbele yaufuasi wa watu binafsi.

Unaongea tofauti unatenda tofauti, matendo yako na kauli zako yanaonesha kuwa huelewi maana na dhana nzima ya "ufuasi wa misingi ya taasisi and not individuals ktk taasisi" kitendo cha chadema kuendelea kuchelewa kukufukuza uanachama inatokana na misingi dhaifu iliyopo ktk chama ambapo individuals wana nguvu kuliko chama, na kwa kuzingatia kuwa ulikuwa sehemu ya uongozi wa chama bila shaka ulichangia ktk ujenzi wa udhaifu huo.
 
mkuu zuberi maghoa! Kama unamfatilia kwa umakini huyu pasco. Lazima utagundua vitu vifuatavyo:
1) anamtetea sana lowasa.
2)pia ajiweki mbali na zito katika kumtetea.
3)anaipiga vita cdm lakini anajitahidi kwa kujifichaficha kupigia chapuo ccm.
4)......
5)......
Kwa ayo na mengineyo jaribu kuunganisha dot.
Mkuu Noeli (Happy Birthday!), ili kunielewa vizuri, usiwe mvivu wa kusoma, tafuta muda taratibu, nitembelee katika thread hizo halafu ndipo unirudie!.

1) anamtetea sana lowasa. -Kumbe umenisikia nikimtetea tuu Lowassa siku zote?. Hebu tafuta muda uusome utetezi wangu kwake hapa Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
2)pia ajiweki mbali na zito katika kumtetea-Siku zote huwa namtetea tuu Zitto, hebu nisome hapa-Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!. - JamiiForums
3)anaipiga vita cdm -Kwa hiyo Chadema huwa naipiga vita tuu!, sijawahi kuipongeza!-Hebu nisome hapa-Yametimia!, CCM Imechokwa!, Chadema Njia Nyeupe 2015 ... na hapa Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!..
lakini anajitahidi kwa kujifichaficha kupigia chapuo ccm. kwa hiyo CCM ndio huwa ninaipgia Chapuo siko zote!. Vipi chapuo hili CCM Imechokwa! na hapa CCM imechokwa mpaka basi!

Merry X-Mass
Pasco
 
Waarabu wasema hayo ni maneno ya haki lakini yaliobeba lengo ovu. Lau kama ni maneno yaliokuwa na lengo la ujenzi ungejitahidi kuzungumza mambo yanayopelekea hali aliyonayo sasa Mwanasiasa huyu ambayo hutokana na harakati haramu za viongozi wenzake hasa huyo MBOWE.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom