Fuata misingi, sio watu, sehem ya pili: Vita dhidi yaufisadi.
Katika makala iliyopita tumeona namna kwa kupitiaMbunge wa Kawe CHADEMA ilivyoweza kutekeleza kwavitendo msingi wake wa kusimamia rasilimali za Taifa.Mbunge wa Kawe, Ndugu Halima Mdee, alifanikiwakupitisha hoja Bungeni yenye kutaka tathmini ya Ardhi naugawaji wa Ardhi hapa nchini. Ardhi ndio rasilimali pekeeambayo kila Mtanzania anaweza kufaidika nayo na hivyougawaji holela wa ardhi unatishia uwepo wa Taifalenyewe. Leo tunaendelea na mfano wa pili katikamfululizo wa makala 6 kuhusu ufuasi wa misingi ya chamabadala ya ufuasi wa watu kwenye chama.
Katika msingi ambao CHADEMA imejitambulisha nao kwakiasi kikubwa ni ule wa kupambana na ufisadi. Viongoziwa CHADEMA na hasa wabunge wake wamekuwa mstariwa mbele kuhakikisha kuwa vita dhidi ya rushwa,ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka inaendeleakuwa kipaumbele katika kampeni zake. Pamoja nakwamba juhudi za CHADEMA kuibua masuala ya ufisadihazijamaliza ufisadi, juhudi hizi zimewafumbua sanaWatanzania na hivyo nao kushiriki katika vita hii.
Kati ya mwaka 2007 na 2010 kumekuwa na maskandalimakubwa ya ufisadi yaliyoibuliwa na wananchi mbalimbalikupitia wabunge na vyombo vya habari. Mifano yamaskandali hayo ni pamoja na Wizi wa tshs 133 bilionikutoka Benki Kuu ya Tanzania, Wizi wa tshs 255 bilionikupitia kampuni ya Meremeta, wizi wa mabilioni ya fedhakupitia mfumo wa kuagiza bidhaa kutoka nje (Import Support), mkataba wa kuuziana umeme wa Richmond namauzo ya mgodi wa makaa ya mawe Kiwira. Kipindi hikikilikuwa ni kipindi ambacho Bunge lilikuwa linasubiriwakwa hamu maana kila mkutano wa Bunge ulikuwa namasuala nyeti ya kujadili kuhusu Taifa. Katika kuongozamapambano haya, wabunge wa CHADEMA ndio walikuwamstari wa mbele chini ya aliyekuwa Naibu Kiongozi waUpinzani Bungeni na Katibu Mkuu wa CHADEMA dkt.Willibrod Slaa.
Ndugu Slaa alikuwa anatekeleza msingi mmojawapo waCHADEMA wa uwajibikaji mbele ya wananchi. Alikuwaanatekeleza jukumu lake la kibunge la kuisimamia Serikalikwa vitendo kwa mwongozo wa misingi ya CHADEMA.Kwa kua Dk Slaa ni Mtanzania na ana ndugu na jamaahumu nchini, huenda kuna watu anao wajua ambaowalifaidi katika masuala haya. Na iwapo mbunge huyuangekuwa anajali maslahi ya watu binafsi ama angekuwamfuasi wa watu angeweza kufumbia macho masuala hayana Watanzania kwa kiasi kikubwa wasingepata fursa yakujua mambo haya.
Suala la EPA lilikuwa suala tete sana. Baada ya uchaguziMkuu wa mwaka 2005 na CCM kuibuka na ushindimkubwa sana wa asilimia 80 ya kura za Rais na hataBunge na kujizolea viti vingi sana Bungeni, siasa zaupinzani zilizorota kwa kukata tamaa. CHADEMA ilikuwaimeingiza wabunge wapya wanane kati ya wabunge wotekumi na mmoja alieingia Bungeni katika Bunge la Tisa.Ilibidi team hili jipya la wabunge wa CHADEMA lijipangesawa sawa kuhakikisha kuwa kazi ya Upinzani Bungeniinafanyika kwa ufanisi hasa ukizinagtia kuwa kambi yaUpinzani ndio unayofanya kazi haswa ya kuisimamiaSerikali. Kambi ya chama tawala mara nyingi hufanya kaziya kuishauri Serikali badala ya kuisimamia. Ufisadi waEPA ulikuwa ni mtihani kubwa sana kwa pande zote mbilindani ya Bunge.
Kwanza, ilibidi taarifa za awali za ufisadi huu kutafutwakutoka kwa walioshiriki kwenye ufisadi lakini wakawa namanunguniko kuwa hawakupata walichotaka, yaanimgawo wao. Mmoja wa waathirika aliandika ‘dossier' nakuisambaza kwenye mitandao ya internet. Kwa ujasirimkubwa sana Dkt. Slaa alitumia nyaraka hizizilizopatikana kwenye internet kutaka majibu ya Serikalindani ya Bunge. Bunge la Bajeti la mwaka 2007 lilitumikakwa mafanikio makubwa sana kuhakikisha kuwa majibuya Serikali kuhusu wizi wa akaunti ya EPA yanapatikana.Chini ya dkt Slaa kambi ya upinzani iliandaa hoja binafsi ilikupata azimio la Bunge kuchunguza na kuchukua hatuadhidi ya ufisadi huu.
Pili, changamoto kubwa ilikuwa ni kuhakikisha ajendainasimama mpaka ukweli ujulikane. Spika wa Bungealipotishia kunyonga hoja ya EPA ndani ya Bungetulikwenda kwa wananchi kwa kuanzia Jangwani nabaadaye MwembeYanga tarehe 15 Septemba 2007.Jangwani dkt Slaa alieleza hoja yake kwa ufasaha naMwembeYanga alitangaza orodha ya Watanzania 11wenye kashfa za kujibu kwa vyombo vya sheria. Orodhahii tuliita ‘list of shame'. Hoja iliendelea kusimamiwampaka uchunguzi wa kina kufanywa na Serikali kuwekawazi watu na makampuni yaliyoshiriki katika kukwapuamabilioni haya ya fedha za Umma.
Moja ya kazi iliyo tekelezwa na CHADEMA kwa nguvukubwa ni kuelimisha wananchi kupitia mikutano ya habarina maandishi yetu. Dkt Slaa alilinganisha fedha hizi nanyumba za Walimu, madarasa, kilometa za barabara nk.Kila mkutano wa hadhara au wa ndani, wabunge waCHADEMA waliutumia kuhakikisha ujumbe huu unafikiawananchi kwa lugha wanayoielewa. Serikali nayo ilitumaMawaziri na Manaibu Mawaziri kwenda kwa wananchikuwaelemisha upande wao. Wananchi hawakuwaelewana maeneo mengine Mawaziri walizomewa na wananchi.Nchi ilikuwa imevimba. Wananchi walikuwa wamefura kwahasira. Katika kipindi hiki na miezi ilio fuata, maelfu yawatu walijiunga na chama chetu kwa kuamini kwamba nichama cha misingi yenye manufaa kwa Taifa, mbali navyama vyenye ushabiki na ufwasi yenye kunufaisha watubinafsi.
Somo kubwa tunalolipata hapa ni kwamba iwapo chamacha siasa kikiwa na umoja kwenye hoja ya msingi nakuisimamia kwa pamoja mafanikio yanakuwa ni makubwasana. Mafanikio ya vita dhidi ya ufisadi yalitokana nawananchi wote, bila kujali vyama vyao, kuona viongozi waCHADEMA kwa pamoja wakisimamia suala hili lenyemanufaa kwa Tanzania kama taifa, na kulieleza kwa kinakwenye mikutano mbalimbali. Iwapo wanachama auviongozi wa chama cha siasa wataendekeza ufuasi kwamtu mmoja mmoja, watapofushwa na ufuasi huo nakutoshiriki kupeleka ajenda ya chama mbele. Halikadhalika, iwapo wanachama au viongozi wa chama chasiasa wakiamua kusimamia ajenda za chama kutokana namisingi ya chama hicho badala ya kusimamia ufuasi kwamtu, chama hicho lazima kifanikiwe katika malengo yake.
Dk Slaa hakusimamia hoja hili kama mtu binafsi, au kamakiongozi wa wafuasi wake, alisimamia hoja kama kiongoziwa chama, na zaidi, kama Mtanzania anae simamiamisingi ya chama chake kwa manufaa ya taifa nzima.Misingi ya kupinga ufisadi iliyowekwa na dkt Slaa kwenyehoja ya EPA ndio ambayo wabunge tuliobakia waCHADEMA tunaiendeleza. Hoja ambazo zimeibukabaadaye kama ufisadi kwenye manunuzi ya mafuta yakuendesha mitambo ya umeme unaoendelea mpaka hivisasa na hata kashfa ya mabilioni ya Uswiss nimwendelezo ya misingi hii. Ujasiri wa kulitumia Bungekujadili masuala ya msingi ya Taifa ni moja ya urithimkubwa sana ambao Dkt Slaa ametuachia wabunge waCHADEMA katika Bunge la Kumi. Kupuuza ujasiri huukwa kupendekeza ufuasi wa watu binafsi ni faida kwawapinzani wetu wa kisiasa, na hasara kwetu sisi wenyewekama wabunge wa upinzani, na ni hasara zaidi kwa Taifaletu ambalo linategemea kua Bunge litasimamia serikali.
Ufuasi wa misingi ya CHADEMA unatuelekezakuhakikisha kwamba hoja yeyote yenye kuimarishamisingi ya chama inayotolewa na mwanachamamwenzetu inasimamiwa mpaka mwisho. Mwisho nikuhakikisha hatua stahili zimechukuliwa maana haitoshi tukuibua masuala Bungeni au kwenye mikutano ya hadharana kuacha yakielea. Mwisho ni pale ambapo ama sheriaimetungwa au wakosaji wamefikishwa kwenye mikono yasheria. Ufuasi wa watu hupofusha. Ufuasi wa misingi yachama hurutubisha chama cha siasa.
Katika makala ijayo, tutaona namna Mwenyekiti waCHADEMA, ndugu Freeman Mbowe aliimarisha chamakutoka nafasi ya tano katika vyama vya upinzani hadinafasi ya kwanza, kwakuweka misingi ya chama mbele yaufuasi wa watu binafsi.