Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 16,863
- 62,390
Mohammed Saidi Alsahaf anacheeeeka, amepata warithi katika nchi moja ya wadanganyika!
Kitu kipya kupokea Maduhuli nakuita Gawio sio!Tatizo Zitto anawaambia matahira wasiotaka jifunza kitu kipya
Tcra wanafanya Biashara gani hadi watengeneze Faida yakupeleka HazinaKweli ujinga wetu wananchi tumegeuzwa mtaji kwa wanasiasa. Nani mkweli hapa kati ya ZZK na JPM? Maana kwa masikio na macho yangu nimemsikia rais MAGUFULI akitoa mf. TAZAMA hawajawahi kutoa hiyo faida hata mwaka mmoja na leo wamejikongoja kwa 600 ml huku TCRA, TANAPA na NCCA wakiwa vinara wa hizo faida kama mashirika ya umma.
Tatizo jamaa yenu anakosea mengi kuliko hayo mnayodhani anapatiaJIWE PIGA KAZI NIMEIFUATILIA HOTUBA YOTE HUYU MPOTOSHAJI TU MASHIRIKA YALITEGWA VZRI KABISA NA MPANGO KUNA YANAYOTOA MADUHURI KWA SABABU YANAFANYA HUDUMA NA YANAYOTOA GAWIO KWASABABU YANAFANYA BIASHARA NA JIWE KASEMA KUNAMAKAMPUNI TANGU KIPINDI CHA NYERERE HAYAJAWAHI KUTOA ILA YAMETOA KWA MARA YA KWANZA KWA AWAMU HII PIA KAAGIZA KWA MSAJIRI WA HAZNA KAMA KUNA MASHIRIKA AMBAYO HAYATOI GAWIO KWA SERIKALI BODI ZAKE ZIVUNJWE AMA YAFUGWE YEYE HAANGALII SHIRIKA ANAANGALIA PESA KAMPUNI AMBALO HALICHANJII HALINA MAANA YEYOTE KWAKE NI BORA LISIWEPO ZITTO THIS IS CHEAP BWANA TAFUTA HOJA KUNTUU NA HII YA KUSUBIRI JIWE AFANYE KITU NDOYO MPATE CHA KUONGEA KUNA SIKU ATABAHATISHA MRADI NA UKAFANYA VIZURI ATA KUPROVE WRONG WATU WAKUONE KILA UNACHOONGEAGA NI CHA UWONGO HADI HAO WANAOKUSUPPORT WAKUGEUKE NA JIWE AONEKANE MNAMSINGIZIAGA TU PILI MKUMBUKE KUTOA CREDIT KWANI JIWE SI KILA KITU ANAKIKOSEA KILA KUKICHA KUPINGA TU ASEE MIMI KWA LEO JIWE KWENYE %100 NIMEMPA 48 ZAKE SIO KILA SIKU KUPINGA TUU
Hivi hawa washamba kwanini wanpenda sifa za kijinga hivi na kurusha live shughuli za kawaida za serikali?Na Zitto Kabwe
Kwamba Mashirika ya umma nchini yanamkabidhi Rais cheki za magawio (dividends) ya faida zao ni ama Ofisi ya Rais inafanya Siasa au hawajui maana ya gawio.
Tukiwa Bunge la 9, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC na baadaye PAC) ililishauri Bunge kufanya marekebisho ya Sheria ya baadhi ya mashirika ya umma Ili kiwango fulani cha Mapato ghafi (turnover) kitolewe Serikalini kama maduhuli ya Serikali.
Serikali ya wakati huo ilikubali na Sheria zikabadilishwa na kutenga 15% ya Mapato ghafi ya Taasisi za Umma kuwa Mapato ya Serikali kuingia Mfuko Mkuu wa Hazina. SIO FAIDA maana mashirika haya mengi hayana faida. Faida ya TCRA ni nini? Ama EWURA? Ama TANROADS?
Kusema Rais anakabidhiwa gawio la faida ya mashirika ya umma ni ulaghai ambao hauna maana yeyote, kwani Taarifa za Ukaguzi za Mashirika hayo zitaonyesha kuwa hakuna faida (na hivyo hakuna gawio), na hivyo kuumbuka kwa Serikali yenyewe.
Kinachotolewa ni nini? Haya ni maduhuli tu, ama ni kodi maalumu ambayo imewekwa kwa mashirika kwa kiwango cha 15% ya Mapato ghafi. Maduhuli au kodi hii imekuwa ikilipwa miaka yote ya nyuma. Sielewi ni kwanini sasa Rais amewaleta mbele wakuu wa mashirika Eti kutoa gawio! Gharama za kuwaleta hao wakuu wa hizi taasisi hazikupaswa kuingiwa kabisa, kwani kodi hizo hukatwa moja kwa moja kuingia Mfuko Mkuu wa Serikali. Sielewi hizi hadaa ni za Nini?
Ni muhimu pia kueleza kuwa kuna hoja ya Ukaguzi ya CAG kuhusu makato haya kwa baadhi ya taasisi. Kwamba makato haya yanapaswa kuwa ‘Tax deductibles’ - yaani wakati wa kukokotoa kodi ya Mapato ya baadhi ya Mashirika malipo haya yanapaswa kuondolewa kwanza.
Hata hivyo TRA wamekuwa hawafanyi hivi na hivyo kukuta mashirika kama TANAPA, NCAA, TPA nk yanalipa Fedha zaidi ya yanavyopaswa kulipa na kusababisha shughuli zao za msingi kushindwa kutekelezwa.
Watanzania msihadaiwe leo, hatupokei gawio, bali tunapokea maduhuli tu.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Julai 23, 2018.
Huyu Jamaa simuelewi kabisaaaa yuko upande upi?Na Zitto Kabwe

Nashauri Zitto akamatwe na kushitakiwa kwa uchochezi wa kumdhalilisha rais wa JMT.Sasa kama siyo gawio bali ni maduhuli kwanini ofisi ya Rais imeruhusu hili kufanyika tena kwa mbwembwe nyingi mno? Nani mkweli katika hili, ni Zitto au Rais?
Kama Rais anadanganya, lengo lake ni kumdanganya nani?? Na kama Zitto hayuko sahihi lengo lake ni nini?? Mimi nafikiri tunahitaji ufafanuzi wa kina kuhusu hili jambo.
Cc. Pascal Mayalla
Rise of fascismNashauri Zitto akamatwe na kushitakiwa kwa uchochezi wa kumdhalilisha rais wa JMT.
Rais wa nchi ni kama baba kwenye familia, sio mtu, huyu ni an institution, na kwa mujibu wa katiba yetu, rais wetu hawezi kukosea ndio maana jashitakiwi. Hata kama Zitto ni mkweli na hayo ni maduhuli na sio gawio, kama rais kasema ni gawio, then ni gawio!.
Haiwezekani rais wetu aseme kitu hiki halafu atokee mtu mwingine, ambishie rais!.
P.
Ufafanuzi gani unaoutaka tena?Sasa kama siyo gawio bali ni maduhuli kwanini ofisi ya Rais imeruhusu hili kufanyika tena kwa mbwembwe nyingi mno? Nani mkweli katika hili, ni Zitto au Rais?
Kama Rais anadanganya, lengo lake ni kumdanganya nani?? Na kama Zitto hayuko sahihi lengo lake ni nini?? Mimi nafikiri tunahitaji ufafanuzi wa kina kuhusu hili jambo.
Cc. Pascal Mayalla
Zitto yuko sawa, hujasikiliza pekeyako.Zitto nahisi hakusikiliza vizuri kakimbilia kuandika na kupotosha watu. Imesemwa wazi, kuna walio toa gawio hasa wenye muundo wa kampuni na shareholding structure mf. Kadco. Baada ya hapo ikatangazwa yanakuja mashirika yanayotoa maduhuri mf. Tcra, ewura na wengine. Tofauti imesemwa wazi kwa waliosikiliza na ikatajwa kuwa ni 15% ya mapato kulingana na sheria. Zitto hoja huna tena.
Hilo nalo swali?Mkuu Zitto kiukweli nilikuwa nakusanya taarifa za jambo hili , kiukweli ni kama umeniwahi , hongera sana .
Swali la kujiuliza ni kwanini serikali inataka kuendesha nchi kwa uongo ?
Salary Slip na vibendera wenzako njooZitto nahisi hakusikiliza vizuri kakimbilia kuandika na kupotosha watu. Imesemwa wazi, kuna walio toa gawio hasa wenye muundo wa kampuni na shareholding structure mf. Kadco. Baada ya hapo ikatangazwa yanakuja mashirika yanayotoa maduhuri mf. Tcra, ewura na wengine. Tofauti imesemwa wazi kwa waliosikiliza na ikatajwa kuwa ni 15% ya mapato kulingana na sheria. Zitto hoja huna tena.