Zitto tena kachafua hali ya hewa bungeni

Niliiona kama kauli ya kimbea flani hivi, HEAVY amebadilika anajifanya ndo kila kitu kwenye siasa, alikuwa tishio zaman. Wasiwasi wangu ni kuwa anaweza akadhani anatumika kuarbu chama kumbe wanamtumia yeye kujiaribia binafsi. Kiukweli TL ana uwezo wa uelewa ukimlinganisha na Nzito,mara kadhaa TL ameitwa kutoa mawazo kwenye tribunals za kimataifa,hoja ya Nzito ya mwandiko ni ya kitoto na haikuwa na jipya. Tunanmwangalia mwanasiasa huyu kijana tunapata dalili mbaya juu yake. Mda unao jirekebishe.
Tatizo la zito ni njaa!uNAJUA MUDA WOTE CCM WANATAFUTA PAKUSHIKA ILI WATOKE KTK HUU MSIBA WAO UTAKAO MALIZIKA RASMI 2015.Zitto ni mtoto wa Tisa kati ya watoto 11 ameishi maisha duni sana hivyo kauli zake ni kutaka apate pakutokea sasa maadam nao sisiemu wanataka kutoka mikononi mwa chadema hivyo wamemwambia tutoe tukutoe!But kuondoka zito ni sawa na van persie kuondoka arsenal maana majembe yapo kibao!Valisha Gamba zitto valisha Gwanda Mwandul!!Chezea Nyakyusa wewe???????
 
twendeni tukachangie mambo ya maana kwenye Thread nyingine....


i agree with you 100%, hii forum is on the attack of Zitto only, vimezidi sasa, kwani mtu akijitangazia kugombea Uraisi imekuwa nongwa au utadhani kachoma vatican au maaka. go zitto go
 
..nadhani ilikuwa ni utani tu, nothing more than that.

..kwa upande mwingine Zitto anapaswa kujirekebisha mwenendo wake ili kurudisha imani ya mwakereketwa wa CDM.
 
Ni kijana, anatafuta cheap popularity. Haendi mbali kwa approach ya siasa za kujibizana na kujaribu kuonyesha kuwa wanasiasa wenzie hawana maana
 
Mzee vipi??? Mbona Povu linakutoka Kwenye Ujinga??? ....Hakika Hujaelewa ....Alicho ongea ni Utani ambao umewafika wachache ambao Message ile inawahusu....huwez elewa kilakitu Kuna kitu cha Msingi ungetumia Mda wako Kuandiki Hili Gazeti kwenye vitu muhimu.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
mkuu HON MP nashukuru sana kwa kuileta hii issue,
Kwakweli nimesikitishwa sana na maneno ya zito na mpaka sasa baada ya kurudia rudia kutazama mchango wake naomba kusema kuwa hapakua na utani hata kidogo bali kuna msukumo wa malengo au visasi fulani ambavyo tungeomba atueleze bila kujishahua...Kwa nini nasema hivyo

1.Kwa wataalamu wa lugha na viashiria mwili (body language), statement ya zito ilikua na stress mwishoni katika sentensi ambacho ni kiashirio cha msisitizo na umaanishaji.

2.tonation aliyotumia zito ini ya kimamlaka na kutoa taarifa wala haikua tonation inayomaanisha mzaha.mzaha gani unamaliza sentensi kwa high pitch na si low??high pitch mwisho mwa sentensi inamaanisha msisitizo wa ulichosema.

3.Mara zote mzaha /utani wowote unaolenga ukweli muhusika hataji jina kwa sababu anafahamu moja kwa moja kuwa mlengwa anafahamu nani anazungumziwa. kama Zito anajua tundulisu ana mwandiko mbaya na tundulisu anajua kuwa kampa zito mchango wake,hapakuwa na ulazima wa kutaja jina la lisu.KWA NINI KAFANYA IVYO??

WANACHADEMA WENZANGU CCM walikuwa wanawaogopa hivihivi mafisadi mpaka wakawa mna mtandao mkuuubwa uliowashinda sasa, TUMWAJIBISHE HUYU JAMAA KABLA HAJATUMALIZA. kama una shoka kata mbuyu mapema kabla haujakua mkubwa or else..........
 
Aliyeambiwa mwandiko wake mbaya yupo kimyaaa sie wengine ndo jasho linatutoka jamvini, waarab wa pemba wanajuana kwa vilemba!
 
mhhh basi haya mambo sijui yataisha lini kila kona ZZK ila nazan sasa inatakiwa atulie kwani hali inavyoonekana sasa hivi yuko kwenye kipindi kigumu ndio maana inafika kipindi anatoa kauli ambazo watu wanatafsri katika negative attitude ....angalia upepo kaka ZZK na upime kila kauli unayotoa kwa sasa
 
Naomba niulize, hivi kauli kama hiyo huwa inaingia kwenye hansard?
 

To the public? for what reason? Huyu siku 3 zilizopita aliwataja MAFISADI wa Tanesco hakumtaja ZITTO KABWE sababu

Haamini kuwa Mwanachama Mwenzake ni Sisimizi wa ulaji Mchafu; wa kiuhaini wa kulaghai nchi nzima...

Yeye ni kubwatuka - Oh Mwandiko Mbaya... Yeye chochote ni Ubwatukaji... NDIO APEWE URAIS????
Namwomba Mhe Antipas Lisu atulie asiwe na jaziba mbona safari bado ni ndefu???

 
Vichekesho viko hivyo?

Jokes ni relative. Inategemea uko wapi, na uko na nani. Wengine wanataka mpaka mtu afunge matambara tumboni, jambo ambalo mini naona ujinga. Mwingine political commedy ya mtu kama Jonathan Mann, haelewi, anaelewa za Mr. Binn. Mwingine comedi kwake ni ya Masanja mkandamizaji... Wakati mwingine yapaswa uwepo katika mazingira fulani kuelewa utani wenyewe. Any way, mimi nina muandiko mbaya, na nimetaniwa sana kuhusu hilo.. sioni ajabu. Suala ni kwamba, kwani hayo matamshi yamefanya nini haswa mpaka yakuzwe hivyo? yamemtuhumu mtu rushwa? yamemtuhumu mtu si msomi? nini haswa?
 
Kuna watu wanauliza body language yake au muonekano wake ulikuwaje wakati anasema hayo? Na wengine wanasema mbona baadaye kaonyesha kutabasamu kwa hiyo ilikuwa utani n.k. Nataka niwajibu kuwa hakika Mnafiki (a double agent) lazima akudanganye, yaani muonekano wake wa nje ni tofauti sana na kilichopo rohoni mwake.

Mzandiki anakuuwa huku anakuchekea na ndicho anachoonekana!

Pili wengine wamesema ni utani wa kibunge (whatever that means), lakini hata mwenyekiti wa session kamsahihisha na kumshushua kuwa hayo ya kushindwa kusoma ni yake hayawahusu maana walikabidhiana wao. Utaona hata Bungeni maneno hayo hayakuwa na tija.

Tatu . Kwa nini yeye kila mara aonekane ni tofauti na wenzake? Inasikitisha sana huyu ndugu tuliyemwamini sana
 
i agree with you 100%, hii forum is on the attack of Zitto only, vimezidi sasa, kwani mtu akijitangazia kugombea Uraisi imekuwa nongwa au utadhani kachoma vatican au maaka. go zitto go

mkuu upinzani umetusaidi sana, mimi ni shabiki wa zito hapo kabla lakini kwa hili amedhiirisha yeye hana uchama anatafuta sifa binafsi, kwa kauli ya leo amedhiirisha amechukua rushwa, ana sababu gani ya kuponda kimemo cha kambi yake wakati amekataa kuusoma? Haandamwi kwa sababu ya uraisi ni kwa kushambulia tim yake,
 
Watu hamna hata matani mbona ya kawaida kabisa haya...Tena ingekuwa vizuri sana kama isingekuwa Utani ikiwa mwandiko wa Lissu ni mbaya sana hauzomeki..Binafsi yangu siamini mwandiko wa Lissu ni mbaya isipokuwa ndivyo tufanyavyo mujini (matani) ktk mazungumzo..
 
Narudia tena waheshiwa wote waaminifu wa chadema wawe makini na Zitto ni mamluki huyu.Waendelee kumtega na kufichua ufisadi wake ili ajifie kisiasa mwenyewe kwa upopo wake.Nashukuru Mungu anaendelea kumuumbua, siku nyingi tu huyu bwana alijiongesha lakini kutokana na ushabiki usio na macho akaendelea kudanganya kambi ya upinzani.Tangu enzi ya Chacha Wangwe huyu Zitto alishaonye upopo wake.Watanzania tuwe makini na watu hawa maana ndio wanaotucheleweshea ukombozi wa nchi yetu.
 
Narudia tena waheshiwa wote waaminifu wa chadema wawe makini na Zitto ni mamluki huyu.Waendelee kumtega na kufichua ufisadi wake ili ajifie kisiasa mwenyewe kwa upopo wake.Nashukuru Mungu anaendelea kumuumbua, siku nyingi tu huyu bwana alijiongesha lakini kutokana na ushabiki usio na macho akaendelea kudanganya kambi ya upinzani.Tangu enzi ya Chacha Wangwe huyu Zitto alishaonye upopo wake.Watanzania tuwe makini na watu hawa maana ndio wanaotucheleweshea ukombozi wa nchi yetu.
 
Zittoooo! Duh! ila ninachomsifu haachi server ya JF na tuhuma zake zisizo na majibu ili vizazi vijavyo vijue mtizamo wake!
 
Bado hajakomaa.

Still Young and Foolish (hili siyo tusi, ni usemi wa kawaida wa kimombo)
 
Back
Top Bottom